Posts

Showing posts from 2012

CERVICAL CANCER

Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-Dec-12/00:45:48 Imesemekana mjini Kibaha kumekuwepo na tatizo kubwa la kansa ya shingo ya uzazi, ambapo katika kila mwaka watu 500,000 wanaogundulika kuwa na kansa ya shingo ya uzazi 275000 wanakufa kila mwaka. Msimamizi wa Kitengo cha kansa ya shingo ya uzazi kituo cha afya mkoani mjini Kibaha, BI. JULIETH SANGA amesema tatizo hilo kwa sasa ni kubwa kwa kiwango cha asilimia 50.9/100,000 na vifo vinavyosababishwa navyo ni wastani 37.5/100,000. BIBI.SANGA amebainisha kuwa kutokana na takwimu hizo ugonjwa huo umekuwa tishio kwa kinamama na mzigo kwa wanaougua na wanaouguza kwani Tanzania imekuwa iko juu kulinganisha na nchi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla wake. BIBI. SANGA amefafanua chanzo cha ugonjwa huo ni kuanza mapenzi katika umri mdogo na hasa wanapokutana na mwanaume mwenye virus vya PAPPILOMA wanaoishi katika mwili wa mwanaume bila kumletea madhara. Amesisitiza hatari ya maambukizi inazidi kwa mwanamke kuwa na wapenzi wengi, ma...

KANSA YA SHINGO YA KIZAZI TISHIO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-Dec-12/00:45:48 Imesemekana mjini Kibaha kumekuwepo na tatizo kubwa la kansa ya shingo ya uzazi, ambapo katika kila mwaka watu 500,000 wanaogundulika kuwa na kansa ya shingo ya uzazi 275000 wanakufa kila mwaka. Msimamizi wa Kitengo cha kansa ya shingo ya uzazi kituo cha afya mkoani mjini Kibaha, BI. JULIETH SANGA amesema tatizo hilo kwa sasa ni kubwa kwa kiwango cha asilimia 50.9/100,000 na vifo vinavyosababishwa navyo ni wastani 37.5/100,000. BIBI.SANGA amebainisha kuwa kutokana na takwimu hizo ugonjwa huo umekuwa tishio kwa kinamama na mzigo kwa wanaougua na wanaouguza kwani Tanzania imekuwa iko juu kulinganisha na nchi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla wake. BIBI. SANGA amefafanua chanzo cha ugonjwa huo ni kuanza mapenzi katika umri mdogo na hasa wanapokutana na mwanaume mwenye virus vya PAPPILOMA wanaoishi katika mwili wa mwanaume bila kumletea madhara. Amesisitiza hatari ya maambukizi inazidi kwa mwanamke kuwa na wapenzi wengi, ma...

WAZAZI WATAKA KURUDISHIWA MALI ZAO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/25-Dec-12/22:57:12 Wanachama wa wa Jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi mjini Kibaha wamemtaka mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kuirudisha shule ya wazazi ya Sekondaro Kaole iliyopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani kurudishwa kwa mikononi mwa Jumuiya hiyo. Akizungumza katika kikao cha Baraza la Jumuiya ya wazazi kata ya Kongowe mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya jumuiya hiyo kata ya Kongowe, DR. NASSORO KAZAMBO ameitaka serikali ya chama cha mapinduzi kurudisha shule hiyo kwa jumuiya ya wazazi ili kutoa fursa kwa jumiya hiyo kuingia ubia na mashirika mbalimbali ili kuziendesha shule hizo. DR. KAZAMBO amesema kitendo cha kupora mali za jumuiya ya wazazi na baadaye kubezwa kuwa ni jumuiya ambayo haitoshi hilo halikubaliki na hasa ikizingatiwa kuwa jumuiya hiyo ni tajiri na kinachosokana ni usimamizi wa mali hizo na kwa kuingia ubia na watu mbalimbali katika kuzisimamia na kuziendesha. Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mjin...

GREETINGS

HAPPY XMAS & NEW YEAR

X MAS

Ben Komba/Pwani-Tanzania/24-Dec-12/18:14:46 Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Pwani limesema kuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mkoa na halmashauri zake katika kipindi hiki cha Krismas ambapo leo kutakuwa na misa za mkesha tayari kwa sikukuu hiyo ya kuzaliwa mwokozi YESU KRISTO kama inavyoaminika na mabilioni ya wakristu ulimwenguni Akiongea na mwandishi wa habari hizi msemaji wa Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani, INSPEKTA ATHUMAN MTASHA ambapo amesema siku kama hizi kunakuwepo na mikusanyiko ya watu wengi hasa maeneo ya makanisani na baa. INSPEKTA MTASHA amewataka wazazi kutotoka wote majumbani kuepuka kutoa fursa kwa wahalifu kufanya madhara, na ameaasa kama watu watatoka itakuwa vyema anayebaki nyumbani kuwa na simu iwapo tatizo lolote litakalojitokeza atoe taarifa linapotokea tatizo. Akizungumzia kuhusiana wenye magari amewataka madereva kupaki maeneo ambayo yapo salama na kuheshimu sheria za usalama barabarani katika kipindi hiki cha sikukuu kutokana na baadhi...

BENKI YA VIJANA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-Dec-12/09:58:38 Vijana mjini Kibaha watafaidika kutokana na hatua ya kuanzishwa benkia ya vijana ambayo itkuwa inajishughulisha na kuwawezesha vijana kwa kuwapatia uwezeshaji wa hali na maki katika kuwasaidia kujikwamua nahali ngumu ya maisha inayowakabili kada hiyo katika jamii. Mratibu wa Benki ya vijana wilayani Kibaha, BI. LULU MKOMAMBO amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa makusudi katika kumwezesha kijana kujikwamua na hali duni aliyonayo, na hasa ikizingatiwa vijana ndio kundi kubwa ambao wanakadiriwa kuwa asilimia 60 ya wakazi jumla ya wa Tanzania. Bi. LULU amesema maeneo mengine yameshaanza kufaidika na Beki hiyo kwa vijana waliobahatika kukopeshwa pikipiki kwa masharti ya kuwasilisha shilingi laki tano na kupatiwa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.8, ambapo kijana atatakiwa kulipa kiasi kilichobaki kwa kadiri ya makubaliano. Amefafanua kuwa kijana atawajibika kutoa fedha za fomu ambayo ni shilingi 20,000/=, a,bazo atalipa mara ba...

MWENYEKIT UVCCM AKANUSHA UVUMI DHIDI YAKE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Friday, December 21, 2012/18:20:03 Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mjini Kibaha, BW.IDD KANYALU amekanusha uvumi wa kuwa yeye amekamatwa kwa jinai na kupelekwa Tanga kitu ambacho amethibitisha kuwa sio kweli. Akiongea na mwandishi wa habari hizi, BW. KANYALU amesema siasa ni mchezo mchafu na huwezi kumjua mbaya wako, na ameomba kama mtu yoyote ana madai kama hayo na athibitishe, kwani uchaguzi umemalizika hivi karibuni na makundi bado yapo. Bw.KANYALU amesema masuala hayo kweli yamezagaa katika lengo zima la kupakana matope kutokana na wanachama wa chama hicho kung'ang'ania makundi yaliyokuwapo wakati wa kampeni wa chaguzi za ndani za chama hicho, na kutokana na makundi kuna bomoa hali ya umoja na mshikamano iliyokuwepo hapo awali kabla ya mfumo wa vyama vingi kuingia nchini. Amewaasa wana CCM kuwa kitu kimoja na kuimarisha upendo na mshikamano ndani ya chama hicho, na si vyema kwa wanachama wa chama hicho kuchafuana kwa m...

MBUNGE AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KIBAHA MJINI.

Image

DOUBLE STANDARD

DOUBLE STANDARD Ben Komba/Pwani-Tanzania/16 December, 2012/18:32:08 Baraza vijana mkoa wa Pwani limewakana wale ambao wanadai kutoka baraza hilo katika Mkoa wa Mwanza wanaoshinikiza Katibu wa Chama hicho, DR. WILBROAD SLAA ajiuzulu kutokana na yeye kuwa na kadi ya CCM. Mwenyekiti wa Baraza la vijana Mkoa wa Pwani, BW. ELLISON KINYAHA amesema kuwa mkoa wa Pwani hautambui watu hao wanaojiita viongozi wa BAVICHA mkoa wa Mwanza na siku zote wataambatana na Katibu wao DR. WILBROAD SLAA ambaye mpaka sasa ameonyesha nia ya kweli ya kumkomboa Mtanzania, na kuwachukulia watu wanaompinga kama mamluki ambao wamekosa kazi ya kufanya, na hata katika mkoa wa Pwani wapo wanaozunguka kumpiga vita Katibu wao. BW. KINYAHA amefafanua katika operesheni ya mwezi wa tatu, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ubunge katika uchaguzi uliopita aliondoka katika mazingira ya kutatanisha na fedha alizokabidhiwa kwa ajili ya mafuta ya magari yatayotumika kuendesha operesheni hiyo ya kukinadi chama. Aidha amese...

MBUNGE AHIMIZA UPENDO NA UMOJA CCM.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-Dec-12/17:03:00 Mbunge wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW. SYLVESTER KOKA amewataka wanaCCM MJINI Kibaha mjini kutoogopa kuwakosoa viongozi wake moja kwa moja badala ya kusemea pembeni na kutoa fursa kwa maadui kukidhoofisha chama chao. Ameyasema hayo akiwa katika ziara maalum ya kuimarisha uhai wa chama mjini Kibaha katika kata ya Mailimoja Tawi la TAMCO, BW. KOKA amesema tabia ya baadhi ya wana CCM kutotumia nafasi yao kama wanachama wa chama hicho kuongea na viongozi juu ya mambo mbalimbali ambayo wanayafahamu na badala yake kwenda kuongea mahali ambapo hapastahili ndio zinazokichimbia karibu chama hicho. BW. KOKA ametoa mfano wa kuwa haiwezekani Mzazi akaenda kumsifia mwanaye kama labda analala nje kwa jirani yake badala ya kujadili suala lile na mwanae, kwani kwa kumueleza vile jirani hakutasaidia kurekebisha hali ya mambo badala yake inaweza kusababisha mambo kuharibika zaidi. Mbunge huyo wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW. SYLVESTER KOK...

CCM WAHIMIZA VIKAO VYA NDANI YA CHAMA.

Ben Komba/16 December 2012/23:32:44 Chama cha mapinduzi mjini Kibaha kimeonywa kuwa kisimtafute mchawi kitakapofanya vibaya katika uchaguzi mkuu ujao, kutokana na viongozi wa ngazi za matawi na Kata kutozingatia vikao vya kikatiba. Mwenyekiti wa CCM, Kibaha mjini BW. MAULID BUNDALA amesema hayo akiwa katika ziara yake ya kukiimarisha chama katika kata ya Picha ya Ndege. BW. BUNDALA amefafanua kutokana na mweleko anaona sasa kuna kila dalili ya viongozi na wanachama wa CCM wenyewe kuwa chachu ya kushindwa kwa chama hicho katika chaguzi zijazo. Ameongeza toka mwanzo wa ziara yake amekatishwa tama na baadhi ya matawi kushindwa kuitisha vikao vya wanachama ili kuweza kutathimini utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama. BW. BUNDALA ameyasifu matawi ya Picha ya Ndege B na Lulanzi kwa kuonyesha uhai wa chama katika maeneo hayo, na amewaonya viongozi ambao wamekuwa na tabia ya kutoroka vikao kwa visingizio mbalimbali. END.

WALIOJITA BAVICHA WASUTWA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/16 December, 2012/18:32:08 Baraza vijana mkoa wa Pwani limewakana wale ambao wanadai kutoka baraza hilo katika Mkoa wa Mwanza wanaoshinikiza Katibu wa Chama hicho, DR. WILBROAD SLAA ajiuzulu kutokana na yeye kuwa na kadi ya CCM. Mwenyekiti wa Baraza la vijana Mkoa wa Pwani, BW. ELLISON KINYAHA amesema kuwa mkoa wa Pwani hautambui watu hao wanaojiita viongozi wa BAVICHA mkoa wa Mwanza na siku zote wataambatana na Katibu wao DR. WILBROAD SLAA ambaye mpaka sasa ameonyesha nia ya kweli ya kumkomboa Mtanzania, na kuwachukulia watu wanaompinga kama mamluki ambao wamekosa kazi ya kufanya, na hata katika mkoa wa Pwani wapo wanaozunguka kumpiga vita Katibu wao. BW. KINYAHA amefafanua katika operesheni ya mwezi wa tatu, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ubunge katika uchaguzi uliopita aliondoka katika mazingira ya kutatanisha na fedha alizokabidhiwa kwa ajili ya mafuta ya magari yatayotumika kuendesha operesheni hiyo ya kukinadi chama. Aidha amesema wazi ku...

M4C YAVAMIA KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/14-Dec-12/19:25:28 Chama cha demokrasia na maendeleo kimezindua rasmi kampeni yake ya vuguvgu la mabadiliko mjini Kibaha kwa kuwataka wananchi kuchukua hatua ili kuleta mabadiliko ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya nchi yetu. Akiongea katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya mpira Maili Moja, Mbunge wa Ubungo, BW. JOHN MNYIKA amesema wakati ni huu kwa wale wanaoteseka katika nchi hii kunga mkono kampeni ya vuguvugu la mabadiliko ili kuyaona mabadiliko ambayo mnataka kuyaona. BW. MNYIKA amebainisha kuwa ili kuwa wakala wa mageuzi inabidi kila mtu awajibike katika eneo lake kama ni Mwalimu awe wakala wa mabadiliko katrika eneo lake, na kama ni askari basi awe wakala wa mabadiliko katika eneo lake halikadhalika wamachinga na jamii nzima kwa ujumla. Mbunge huyo wa Ubungo ameongeza kuwa wananchi wamekuwa wakiona misukosuko mbalimbali ikiwakabili viongozi wa CHADEMA, kama mauaji ya Morogoro, mauaji ya Mwandishi DAUD MWANGOSI, yaliyomkuta DR....

ZING ZONG STORY

Ben Komba/Pwani-Tanzania/11-Dec-12/17:51:23 Mkazi wa Picha ya Ndege mjini Kibaha, BW. HEZRON MWANSASU amefikishwa mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mkoa wa Pwani akituhumiwa kwa kosa la kumuingilia kinyume cha maumbile mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 7 ambaye alikuwa anaishi naye. Akisomewa shtaka mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mkoa, BW. ESTOMI KISANGA na Mwendesha mashtaka, BW. JONAS SIRA inadaiwa tarehe 24 Novemba mwaka huu majira ya saa tano usiku huko maeneo ya Picha ya Ndege mjini Kibaha mkoa wa Pwani mshtakiwa alimuingilia kinyume cha maumbile mtoto huyo mwenye umri wa miaka 7 ambaye jina lake limehifadhiwa na kumsababishia maumivu makali. Hakimu mfawidhi wa Mkoa BW. ESTOMI KISANGA aliahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 21 Desemba mwaka huu na mshtakiwa yupo nje kwa dhamana. END.

CHANJO MPYA YA NIMONIA NA ROTAVIRUS WANACHI WAHAMASISHWA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/30-Nov-12/06:27:06 Wananchi wilayani Kibaha wametakiwa kuto ushirikiano wa kutosha kwa watoa huduma ya chanjo ROTAVIRUS na NIMONIA katika suala zima la uimarishaji wa afya, na katika muda wote wa utekelezaji wa zoezi hilo ambalo likifanikiwa litawezesha kufanya magonjwa ya uti wa mgongo na kuharisha kwa watoto wadogo kuwa historia hapo baadaye. Akizungumza katika kikao cha uhamasishaji na kamati ya afya ya msingi ya wilaya, Mwakilishi wa mkuu wa wilaya Bw. ANATOLY MHANGO amekemea tabia ya baadhi ya watu kupotosha malengo ya chanjo mbalimbali zinazotolewa kwa jamii katika kuiepusha na magonjwa ambayo yanaweza kukingika. BW. MHANGO amewaasa wananchi kutoa ushirikiano ili kuweza kiampeni hiyo ya chanjo ya RITOVIRUS na NIMONIA ifanikiwe, katika kuhakikisha suala zima la kuboresha huduma ya afya ya jamii. Naye Mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BIBI. REHEMA PILIMO amesema kuwa ROTAVIRUS ni vimelea vinavyosababisha kuharisha kwa watoto...

UPATIKANAJI WA MAJI KUBORESHWA-KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18:38/27-11-2012. Chanzo cha maji chenye uwezo wa kuzalisha mpaka zaidi ya mita za ujazo 36,ambazo ni sawa lita 36,000 za maji zinazalishwa na chanzo cha kisima kilichochimbwa maeneo ya Ngeta katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha, na kuvifaidisha vitongoji 6 vya halmashauri vya halmashauri hiyo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mhandisi wa maji katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BW. CHRISTOPHER MDUMA amesema hatua hiyo ni katika kuhakikisha halmashauri ya wilya ya Kibaha inakuwa na maji ya uhakika katika kipindi chote cha mwaka. BW. MDUMA ameongeza chanzo cha maji cha Ngeta kitawezesha kupunguza makali ya upatikanaji wa maji kwa baadhi ya vitongoji ambavyo awali iliwalazimu wakazi wake kutembea umbali mrefu kutafuta maji hasa nyakati za kiangazi, kutokana na visima vingi kukauka katika kipindi hicho. Amefafanua kuwa kabla ya kutekelezwa kwa mradi huo, wananchi walikuwa wakitegemea visima vya asili, kutokana na chanzo cha Ngeta kitafai...

Father Kidevu: MSANII/MUIGIZAJI/MCHEKESHAJI SHARO MILIONEA HAYUPO NASI

Father Kidevu: MSANII/MUIGIZAJI/MCHEKESHAJI SHARO MILIONEA HAYUPO NASI

MINISTER KAWAMBWA LIE ABOUT RELIGIONISM IN OUR SCHOOLS

Image
Bernard Komba   DONTLIE:Kawambwa it is time for you to step down,it seem that you are the source of religion inspired violence caused by muslims student you try to lie, and if not what about kibiti,usagara. you are there to promote religion or what. why you manipulate the truth, here in coast region we witness rise of islamists who indirectly supported by some people especially fellow muslims who are plenty in every high position in our region to cause unrest to rob christian land forceful and erect the mosque in kibaha. 9 hours ago  via  mobile  ·  Edited  ·  Like Bernard Komba   dont blame teachers and all students, blame muslims students supported by board member with arab origin and one muslim teacher who are known and government protect them for hidden reason, in proccess to muslimize Tanzania, it is conspiracy from high to ... See More 9 hours ago  via  mobile  ·  Like Berna...

ONLINE BENEFITS

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/11/23/8:53:32 AM Mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI. MWANTUMU MAHIZA ameelezea matarajio makubwa ya mafanikio katika suala zima la maendeleo kutokana na kujengwa mkonga wa mawasiliano wa Taifa na hivyo kurahisisha utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii. Akizungumza na waandishi wa habari ambao walikuwa wameambatana na na mtaalamu wa masuala ya Mtandao, BW. LUKELA MKAMI ambae alikuwepo hapa kwa ajili ya kuwanoa waandishi wa habari wa mkoa Pwani juu ya matumizi ya mtandao wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Ambapo Mkuu wa mkoa MAHIZA amesema yeye binafsi amefurahishwa na hatua ya serikali kujenga mkonga wa mawasiliano ambao unanuwiwa kupunguza gharama za matumizi ya mtandao na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya serikali. Amebainisha mpaka sasa serikali imeshaanza kutekeleza majukumu yake mbalimbali kwa kutumia mtandao ikiwa pamoja na kuanzisha ulipaji wa fedha kwa kutumia mfumo wa kielektroniki unaojulikana ...
Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/11/23/8:53:32 AM Mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI. MWANTUMU MAHIZA ameelezea matarajio makubwa ya mafanikio katika suala zima la maendeleo kutokana na kujengwa mkonga wa mawasiliano wa Taifa na hivyo kurahisisha utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii. Akizungumza na waandishi wa habari ambao walikuwa wameambatana na na mtaalamu wa masuala ya Mtandao, BW. LUKELA MKAMI ambae alikuwepo hapa kwa ajili ya kuwanoa waandishi wa habari wa mkoa Pwani juu ya matumizi ya mtandao wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Ambapo Mkuu wa mkoa MAHIZA amesema yeye binafsi amefurahishwa na hatua ya serikali kujenga mkonga wa mawasiliano ambao unanuwiwa kupunguza gharama za matumizi ya mtandao na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya serikali. Amebainisha mpaka sasa serikali imeshaanza kutekeleza majukumu yake mbalimbali kwa kutumia mtandao ikiwa pamoja na kuanzisha ulipaji wa fedha kwa kutumia mfumo wa kielektroniki unaojulikana ...

CCM INATISHA KIBAHA-KOKA

MBUNGE KIBAHA MJINI ASEMA CCM INATISHA-KOKA Ben Komba/Pwani -Tanzania/12/11/18/9:47:21 Mbunge wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW. SLYVESTER KOKA ametambia mafanikio ambayo Kibaha imeyapata katika kipindi cha miaka miwili akiwa kama mbunge wa Jimbo hilo. Akizungumza katika hafla ya kuwashukuru wananchi wa mtaa wa Kwa mfipa kwa kuichagua CCM karibuni katika nafasi zote za uongozi, BW. KOKA amesema katika kipindi cha miaka miwili cha ubunge wake amewezesha mji wa Kibaha kuwa na barabara ya lami kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa Kibaha kama makao makuu ya mkoa wa Pwani mwaka 1974. Mbunge huyo alipokuwa anawafumbua macho na masikio wananchi wa Kata ya Kwa mfipa kuhusiana na shughuli mbalimbali za maendeleo katika kipindi cha miaka miwili cha ubunge wake kwa kueleza nini kinaendelea, ikiwa pamoja na kuanzisha mfuko wa elimu wenye lengo la kuhakikisha vijana wanapata elimu ambayo itasaidia kuchochea maendeleo ya Jimbo lake. BW. KOKA amesema kuwa katika kuhakikisha mfuko ...

WATOA HUDUMA MAJUMBANI KIBAHA WALIA UJIRA KIDUCHU

watoa huduma kwa wagonjwa majumbani walia malipo hafifu kibaha Ben Komba/Pwani-Tanzania/15-Nov-12/05:30:05 PM Imebainishwa mijini Kibaha kuwa kubadilika kwa mashirika yanayoendesha mradi wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa majumbani mjini Kibaha, ndio chnazo cha kubadilika kwa taratibu mbalimbali za uendeshaji kutokana na kila shirika kuwa na sera yake. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kufuatia baadhi ya watoaji huduma kwa wagonjwa waliopo majumbani, kulalamikia ufinyu wa malipo ambayo wanapatiwa na shirika lisilo la kiserikali linalosimamia mradi huo kwa sasa mjini Kibaha la PATHFINDER kwa kushirikiana na RED CROSS na EGPF ambao wamerithi kutoka kwa shirika la KIFARU, Mratibu wa huduma za wagonjwa majumbani, DR. ALEX MLIGA amesema wadau hao wameanza kazi toka mwezi wa nne mwaka huu. Na kwa kuanzia waliendesha zoezi la utambuzi kubaini uwezo wa watoaji huduma majumbani waliopo, ili kubaini iwapo kama kuna wenye upungufu kutoendelea nao, na kigezo kikubwa kilichozingatiwa ni...

HALMASHAURI KUSAMBAZA MAJI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13-Nov-12/07:19:16 PM Halmashauri ya wilaya ya Kibaha katika mkoa wa Pwani imeanzisha mpango maalum wa usambazaji wa maji katika vijiji takriban 10, mradi amabao utagharimu fedha za Kitanzania zaidi ya milioni 300. Akiongea na mwandishi wa habari hizi mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BW. JUMA IBRAHIM amesema shughuli ambazo zinatarajiwa kutekelezwa katika hatua ya awali katika vijiji viwili vya NGETA na MSONGOLA, Ambapo katika kijiji cha Ngeta mradi unatarajia kujenga tanki la lita 100,000. Mbali ya ujenzi wa tenki hilo BW. IBRAHIMI amesema mabomba yenye urefu wa mita 737 ambalo litakuwa bomba kubwa litalogawanya maji katika vituo saba ambavyo vitakuwa na umbali wa mita 6040, sawa na ufungaji wa jenereta na pampu ya maji. BW. IBRAHIMU ameongeza katika kuhakikisha mradi huo unajiendesha idara ya maji halmashauri ya wilaya ya Kibaha itafunga mita katika kila kituo cha kusambaza maji, ikiwa na utoaji wwa mafunzo kwa kamati za maji za vi...

KAMPENI YA MAMA MISITU YAZINDULIWA PWANI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/11/11/12 Kampeni ya mama misitu imezinduliwa rasmi katika kijiji cha Kisanga tarafa ya Sungwi wilayani Kisarawe, ikiwa na lengo la kuahamasisha jamii kuwa na ufahamu kuhusiana na masuala ya utunzaji wa mazingira na umuhimu wake katika kupunguza hewa ukaa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo Mratibu wa BW. YAHYA MTONDA ambaye amesema lengo kuu la kampeni ya mama misitu, ni kupeleka suala la utawala bora katika suala la uhifadhi wa misitu kwa jamii ili kuweza kuwa shirikishi kwa jamii kushiriki moja kwa moja katika kuilinda na kuitunza misitu ya RUVU Kusini. BW. MTONDA ameongeza kuwa kwa kampeni hiyo ni kuleta mageuzi chanya katika suala uhifadhi wa misitu na kupunguza uvunaji haramu wa mazao ya misitu sawa na kuhakikisha wanajamii wanaoishi maeneo yaliyozunguka misitu wanafaidika kwayo. Amesema katika suala zima la kuwepo kwa utawala bora, halmashauri za wilaya na vyombo vinavyosimamia sheria kwa kuwapatia elimu kuhusiana na utawala bora katik...

VUTA NIKUVUTE YA UDINI BADO YAENDELEA BAGAMOYO SEKONDARI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/03-Nov-12/17:25:09 Mgogoro wa kidini unaoendelea katika shule ya sekondari Bagamoyo na huku viongozi wa mkoa wa Pwani wakipiga chenga kuzungumzia suala hilo na kulishughulikia kutokana na wengi wao kuwa wenye madaraka makubwa mkoani hapa kuwa waumini wa dini ya Kiislam hali ambayo inaendelea kuzua maswali miongoni mwa wananchi hususan wakristo kuhusiana ni wapi tunakwenda. Hayo yamezungumzwa na baadhi ya wazazi wa watoto wa kikristo wanaosoma kwa kuelezea kukatishwa tamaa na maneno ya Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani. SALEH MBAGA ambaye alikiri kwa kuwepo kwa tatizo hilo, na kuonysha kufurahishwa kwake na taarifa ya Mwalimu mkuu wa shule ya kuondoka na Familia yake kwa kusema wao ndio walivyotaka kwani wanafunzi wa kiislamu hawamtaki na ikizingatiwa kaimu kamanda naye ni muislam bila kuangalia wanafunzi wakristo wana hoja gani. Mzazi huyo amesikitishwa na hatua ya serikali kujaribu kuvundika jambo hilo kwa kuficha taarifa kwa sababu ambazo...

MJI WA KIBAHA WAPANGA MIKAKATI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/28-Oct-12/10:56:35 Halmashauri ya mji wa Kibaha katika robo ya kwanza ya Julai-Septemba inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 4 milioni 230 laki mbili elfu 15 na 94, ikiwa ni makusanyo kutoka vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ambayo ni asilimia 36 ya makisio ya mwaka 2012 mpaka 2013. Akisoma taarifa hiyo Makamumwenyekiti wa halmashauri hiyo BW. NANGULUKUTA SAID AHMAD amebainisha halmashauri katika robo ya kwanza ya Julai mpaka Septemba 2012 inatarajia kutumia shilingi milioni 323,967,413/= ambayo ni sawa na asilimia 16 ambayo ndiyo ya makisio ya mwaka wa fedha 2012/2013 ikiwa pamoja na salio anzia la Julai 01 2012. Na kati ya mambo ambayo yanatarajiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na suala zima la utunzaji na usafi wa mazingira ya mji wa Kibaha kwa kuzindua gari la taka kwa ajili ya kukusanya taka kutoka maeneo mbali, kipaumbele kingine kitakuwa ni ununuzi wa gari la idara ya ardhi kupitia mapato ya ndani. Akizungumza katika kikao cha Baraz...

VITA VYA KIDINI VYAPEWA NAFASI BAGAMOYO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/28-Oct-12/09:35:52 Wanafunzi wakristo wa shule ya Sekondari Bagamoyo zamani maarufu kama MAGAMBANI wamefunga virago vyao na kuamua kurudi makwao kufuatia serikali kushindwa kusimamisha uasi unaofanywa na wanafunzi wa Kiislam wanaosoma katika shule hiyo ambao wamekuwa mstari wa mbele kuwakashifu wenzao wakristo na kuwatishia kuwauwa huku wakiangaliwa tu. Mmoja wa wanafunzi ambaye amerejea jana kutoka shule hiyo kutokana na hali kuzidi kuwa tete kutokana na kutochukuliwa hatua madhubuti ya kutatua mgogoro huo na serikali ya wilaya ya Bagamoyo inayoongozwa na BW. AHMED KIPOZI ambaye amewahi kuwa mwandishi wa habari na Mhadhiri katika Chuo cha Kiislam Morogoro kushindwa kutatua mgogoro huo ambao umeota mizizi wilayani hapo. Wanafunzi hao waliamua kuondoka kufuatia baadhi Waislamu wa nje kushupalia mgogoro huo na kuwatisha wanafunzi wakristo hao ambao wengi wao wakiwa ni wenye umri wa miaka 18 mpaka 25, ambapo nao wameazimia iwapo serikali itakubali ulalamis...

KINAMAMA WAWEZESHWA NA INUKA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-Oct-12/4:56:04 PM Wafanyakazi ambao wameajiriwa katika sekta mbalimbali za utumishi wa umma wametakiwa kujishughulisha na masuala ya ujasiria mali wanapotoka kuwajibika katika kazi zao walizoajiriwa nazo ili kuweza kukabiliana na changamoto za kiuchumi ambazo wanakumbana nazo kwa sasa na mara baada ya kustaafu. Mkurugenzi mtendaji wa kanda ya kaskazini, BW. DAVID MSUYA wa shirika hilo linaloitwa INUKA, linalowawezesha kina mama wajasiriamali bila kulazimika kuwa na amana kama ilivyo kwa taasisi nyingine za fedha, amesema katika kanda yake kuna vikundi takriban 24 na lengo kuu ni kuwajengea uwezo akinamama kuweza kutambua haki zao za msingi na kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali ili kumfanya Mama nae awe chanzo cha mapato. BW. MSUYA amesema katika Mkoa wa Pwani wameanza kwa ktengeneza vikundi viwili ambavyo kimoja kipo katika Kata nya Magomeni mjini Bagamoyo na kingine kikiwa Ruvu darajani, amebainisha vikwazo kadhaa kujitokeza wakati wa utekelezaji wa zo...

UDINI WAFUKUTA BAGAMOYO SEKONDARI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-Oct-12/16:14:56 Hali ya sintofahamu imeyakumba mazingira ya Shule ya sekondari Bagamoyo kufuatia wanafunzi wa Kiislamu kutaka shule hiyo iendeshwe kwa misingi ya Kiislamu, na wakisusia taratibu za kawaida za shule kwa kisingizio cha kutekeleza nguzo za Kiislamu ya Uislam wao kwa kuamua kumlazimisha Mwalimu Mkuu aachie nafasi hiyo eti kuwa amekuwa akiwanyanyasa sana wao. Kutokana na hali hiyo wanafunzi wa Kikristo nao wakaamua kuvunja ukimya kwa kuamua kukabiliana na wanafunzi wenzao wa Kiislam ambao walikuwa wanataka kumshambulia Mwalimu Mkuu kwa kumsogelea na kumweka kati, na kuona hivyo wanafunzi wakristo nao wakasogelea eneo hilo wakiwa wamewazunguka Wanafunzi hao Waislamu wakiawaangalia kujua watamfanya nini Mwalimu Mkuum ili kujibu mapigo dhidi ya wenzao wa Kiislamu. Taarifa ya chanzo chetu ndani ya eneo la tukio kinasema hali hiyo imefuatiwa kwa kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi kama ilivyo ada, na ndipo ilipobainika kuwa wenzao ...

VIJANA WAPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUPITIA ilo NA ypc

Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-Oct-12/05:44:31 PM Mkuu wa wilaya Kibaha BIBI. HALIMA KIHEMBA amekemea tabia ya wanajamii kuwaita vijana kuwa ni bomu ambalo linasubiriwa kulipuka muda wowte bila kutafuta mbinu mwafaka za kuwaondoa katika ukosefu wa kazi kwa kuwapatia mafunzo na mtaji wa kuanzisha biashara na miradi ya kilimo na ufugaji. Mkuu huyo wa wilaya ya Kibaha, BIBI HALIMA KIHEMBA amesema juhudi ambazo zinaonyeshwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kama ambavyo YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE ambalo limewapatia vijana mafunzo kuhusiana masuala ya ujasiriamali ambapo kutasaidia kuwafanya vijana kubadilisha mtazamo kutoka kwa uliopo sasa wa kuwa vijana ni bomu linalongojea kulipuka mpaka kuwa wazalishaji wakuu ambao nguvu kazi yao itakuwa tegemeo kwa Taifa. Hayo ameyazungumza katika uzinduzi wa awamu ya pili ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wa Kibaha ambvayo yanmefadhiliwa kwa asilimia kubwa na shirika la kazi ulimwenguni -ILO-, Na amekataa kukubaliana na dhana ya kuwa vijan...

VIONGOZI WA DINI WAKUTANA NA JESHI LA POLISI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/10/22/04:29:49 PM Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani limeelezea kushangazwa kwake na hatua ya wahuni kuchoma makanisa na kuharibu mali za serikali kwa kisingizio cha muungano. Katika taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa viongozi wa dini katika suala zima la kutambua mchango wao katika kuleta amani na utulivu katika jamii, Kaimu Kamanda wa mkoa wa Pwani, SALEH MBAGA amesema vitendo vinavyofanyika hivi sasa hapa nchini vinatia doa amani na usalama wa nchi yetu. BW. MBAGA amewashukuru viongozi wa dini hususan ya Kiislamu kwa kuweza kuwashika waumini wao wasifanye maandamano ya vurugu kama ilivyotokea Mkoa wa Dar es Saalam na Zanzibar, na kwa kutambua hilo Jeshi la Polisi liumeona vyema kukaa pamoja na viongozi wa dini ili kupata njia ya pamoja za amani ili kuendeleza ushirikiano wetu uliodumu kwa muda mrefu. Amebainisha kuwa Jeshi la Polisi kwa upande wake wanaamini kuwa kuna misingi ambayo ikifuatwa vyema italiweka Taifa pazuri, kwa kuifikia jamii ...

UNITED WITH ISRAEL.

Israel Alert Newsletter 26 Tishrei 5773 October 12, 2012 Israeli Vaccine to Stop Cancer from Returning to Patients (Nes Ziona, ISRAEL) An Israeli company is developing a new cancer drug which aims to stop cancer from coming back. Every year millions of people are diagnosed with cancer worldwide. Although modern medicine has made huge progress in treating this disease, what often happens is that the cancer is treated and the patient goes into remission or is even "cured" - but then it becomes a waiting game to see if the cancer comes back. Imagine if there was a new treatment option that would stop cancer from returning! An Israeli medical team is attempting to do just that, to offer a new treatment with the potential for long-term maintenance - to stop the cancer from coming back. Click here to read more>> Israel Nuclear Facility Receives 'Spiritual Protection' (Dimona, ISRAEL) The Israeli Dimona nuclear reactor facility now has an extra laye...

BLESSED NATION RESPECT IT, and LEAVE BEHIND CAIN JELOUS AGAINST HIS BROTHER ABEL.

September 23, 2012 Israel Revolutionizes Liver Disease Treatment! Israeli scientists are developing a treatment for people suffering from liver disease. Nonalcoholic steatohepatitis (NASH) is a "silent" liver disease which affects two to five percent of Americans - approximately six to fifteen million people. Another ten to twenty percent of Americans, thirteen to twenty three million people, have fat in their livers but have not yet developed NASH. Tens of millions of people around the world also are at risk of suffering from NASH. Click here to read more>> Koch Urges Obama To Be Firm Over Israel Former New York City Mayor Ed Koch stood before over 1,000 people to deliver his annual Rosh Hashana sermon at the Park East Synagogue. Koch, who has talked openly about his close ties to President Obama, lambasted the president and current US policy towards Israel: "I'm distressed. President Obama is refusing to publicly make clear to Iran that 'I...

FIRE SOCIAL CLUB YAPATA VIONGOZI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/07/2012/16:32:18 FIRE SOCIAL CLUB ya mijini Kibaha imefanya kikao chake cha uchaguzi mkuu na kufanikiwa kupata viongozi watakaoiongoza kwa kipindi cha miaka mitatu, ambapo uongozi huo umenuia kufanya mambo mabalimbali katika kuhakikisha michezo inakuwa ajira ya kutegemewa na vijana. Katika uchaguzi huo Mwenyekiti amechagulia kuwa JUMA MBWANA, na nafasi ya Katibu ikichukuliwa na RICH KIBAJA, Mweka hazina akiwa KESSY PONSI na mtunza vifaa akichaguliwa kuwa ni MESHAKI KAIRA. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa FIRE SOCIAL CLUB, RICH KIBAJA amebainisha kuwa lengo ni kukuza michezo hususan timu ya soka ambayo tayari ipo, kwa kuibua vipaji vya vijana ambao wanahitaji usaidizi mdogo ili waweze kusonga mbele katika medani ya michezo. KIBAJA ameongeza kuwa michezo ina umuhimu mkubwa kwa binadamu toka michezo ni starehe, afya na burudani. END

KIBAHA INDEPENDENT SCHOOL.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/10/07/12:04:46 PM Shule ya msingi ya Kibaha independent iliyopo mjini Kibaha imeazimia kuwaandaa wanafunzi kuishi kulingana na maendeleo na mabadiliko ya sayansi ya teknolojia ya utandawazi ili kuweza kukua kitaaluma, kiakili, kijinsia na kimaono. Ameyazungumza hayo Mkuu wa shule ya Kibaha Independent, BW. HEZRON MUSALALE wakati akimkaribisha mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la saba, Lengo kuu la shule yao ni kuhakikisha vijana wanaopita hapo wanakuwa matunda ambayo yatachangia kwa njia moja au nyingine maendeleo ya Taifa. BW. MUSALALE amebainisha makakati wa shule kuvipa nuru ya kielimu vizazi vingi kwa kuvipatia elimu ya hali ya juu, na hasa shule ikiwa ina malengo mahsusi ya kuhakikisha wanafunzi wanaweza kusoma na kuandika kwa kutumia lugha mbalimbali hususan Kiswahili na Kiingereza, kuhakikisha wanafunzi wanajenga uwezo wa hali ya juu ya mahesabu na pamoja na kuwajenga wanafunzi katika kujiamini na kuwa na mawazo yakinifu. Akizungumza...

WAJASIRIAMALI VIJANA WAONYESHA BIDHAA KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/10/07/11:05:32 Waziri wa utamaduni, habari, vijana na michezo BIBI. FENELA MKANGARA amewahimiza vijana kujikusanya katika vikundi kwa lengo la kujiendeleza katika kazi za kijasiriamali kwa kuwawezesha kuaminika katika umoja wao na kuweza kukopesheka kwa kudhaminiana wenyewe kwa wenyewe. BIBI. MKANGARA amesema vijana kwa kujikusanya katika vikundi na kuanzisha miradi ya uzalishaji mali kutasaidia kwa kiasi kikubwa vijana wanaoamka na kukaa vijiweni bila kujishughulisha na kazi yoyote ya uzalishaji mali, na kuwataka vijana kutumia kilimo kwanza kujiajiri binafsi na hasa kutokana na maisha ya sasa kuhitaji vijana kuwa wabunifu ili waweze kujiepusha na umaskini. BIBI. MKANGARA amewahimiza kila kijana wa Kitanzania kuanzia miaka 18 aweze kuchangia chakula mezani kwao kwa kuwajibika kikamilifu katika shughuli za kijasiriamali ambazo zitawaingizia tija, na Wizara ya utamaduni, habari, vijana na michezo itajitahidi kwa hali na mali kutafuita masoko kwa ajili...

MAMA WA KAMBO ATESA MWANA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2012-09-30/09:21:22 Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Mlandizi, BI. MIRIAM MBWANA amemuhukumu muuguzi BI. JOSEPHINE CHARLES wa kituo cha afya Mlandizi kilichopo katika wilaya ya Kibaha, kifungo cha miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki mbili na fidia ya shilingi 150,000/= kwa ajili ya kumtesa mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 6. Akitoa hukumu hiyo HAKIMU MBWANA amesema kufuatia uwepo sheria ya haki ya mtoto ambayo inasisitiza katika kumlinda na kumpatia haki stahili mtoto na si vinginevyo, kutokana na hilo hakimu huyo ameamuru mtoto huyo ambaye jina limehifadhiwa akabidhiwe kwa Afisa ustawi wa jamii BW. SAID MBEGU mpaka hapo mama yake mzazi atakapopatikana. Hali hiyo inafuatia wakazi wa mtaa wa Kaloleni uliopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi kuungana kunusuru maisha ya mtoto wa kambo, Ambaye mumewe BW. CHARLES JULIUS DINDA amezaa na mama mwingine, na yeye kumpata BI. JOSEPHINE CHARLES ambaye amezaa naye mtoto mmoja ambaye ana...

DSTV WITH RELIGIOUS DISCRIMINATION

Michael Ajewole 2:18am Sep 16 RE: REMOVAL OF EWTN FROM THE DSTV NETWORK The news is no longer new that EWTN, the darling channel of most Catholics worldwide, particularly in Nigeria, has been yanked off the satellite DSTV network since about a week. From my investigations and contact with the African representative of EWTN, the reasons given are that the channel is non-performing meaning practically that not enough people in Nigeria are watching it. This of course cannot be true because: a. We of the communications apostolate have been inundated with protests messages since it was yanked off and same goes for the EWTN African representative and others internationally. b. No other religious channel has been so treated and we do not believe at all that we are the least of all channel captive audiences off all religious networks. Even of others go, the only Catholic 24 hour satellite channel known amidst the cacophony of religion channels in Africa must not be allowed to go. EWTN h...

TTCL PWANI YAIBIWA NYAYA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/19/12/18:56:24 Shirika la simu katika Mkoa wa Pwani -- TTCL-- limekumbwa na wimbi la kuibiwa nyaya za kusambazia miundombinu ya simu katika Maeneo ya mamlaka ya mji wa Kibaha na wilayani Kisarawe na hivyo kuathiri utoaji wa huduma hiyo ya mawasiliano kwa simu za waya. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mjini Kibaha, Meneja wa TTCL mkoa wa Pwani, BW. FRANCIS MWENDA amesema kuwa wizi huo uetokea maeneo ya TAMCO kati ya Agosti 11 mwaka huu majira ya saa 1.30 na saa 2.00 na kuathiri wateja takriban 30. BW. MWENDA ameongeza waya ulioibiwa ulikuwa na urefu wa mita 180, ambapo mtuhumiwa amekamatwa japo anajifanya hamnazo anapotakiwa kujitambulisha kwa kutaja majina tofauti kila wakati, na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa. Aidha BW. MWENDA amefafanua kwamba matukio hayo ya wizi yamekuwa yanashika kasi kiasi cha kusababisha wilaya ya Kisarawe kukosa mawasiliano kw karibu wiki mbili sasa kutokana na hujuma ambayo...

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI BARABARA-MSATA - BAGAMOYO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/09/18/2012/18:37:04 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. JAKAYA KIKWETE amewataka madereva kuwa makini wanapoendesha magari yao ili kuepusha vifo na majeruhi, ambapo katika kipindi cha mwaka 2011 watu 3100 walikufa katika ajali za barabara na kati yao wengine zaidi ya elfu 22 walijeruhiwa katika ajali hizo. DKT. KIKWETE ameongea hayo wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Msata- Makofia-Bagamoyo yenye urefu wa kilometa 64, ambapo amesisitiza kwa madereva kuwa makini wanapoendesha magari ili kutopotosha nia ya serikali kueneza mtandao wa barabara zenye kiwango cha lami nchi nzima. DKT. KIKWETE amefafanua kuwa barabara hiyo itafungua fursa ya maendeleo kwa wakazi wa Bagamoyo na vitongoji vyake hasa kwa kuzingatia kuwa itakuwa ni kichocheo cha maendeleo hususan kwa wakulima wa kilimo cha mananasi wa Kiwangwa ambao kutokana na ubovu wa barabara uliokuwepo m,ananasi yao yalikuwa yanaozea mashambani wakati wa kipindi cha mvua. Aidha amewaasa wa...

MJI WA KIBAHA KUFAIDIKA NA USHIRIKIANO

Ben Komba/Pwani- Tanzania/9/17/12/19:00:02 Ushirikiano uliopo kati ya halmashauri ya mji wa Kibaha na manispaa ya manispaa ya mkoa wa kisiwa cha GOTLAND, utainufaisha kwa kiasi kkubwa katika suala la demokrasia na, usambazaji wa maji safi na salama, utunzaji wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisisni kwake mjini Kibaha, Mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. ABUDADI MKOMAMBO amesema uhusiano huo kati ya miji hii miwili una takribani miaka 12 sasa. Ambapo BW. MKOBAMBO amebainisha katika kipindi cha miaka miwili ijayo yaani m,waka 2012 mpaka 2014, uhusiano wao umetoa kipaumbele kwa miradi kadhaa ambayo itafadhiliwa na ICLD (international center for loca demokrasi) ambayo ina lengo la kuimarisha demokrasia kwa watu wa kada ya kawaida, ikiwa pia ndio kipaumbele cha shirika la kimataifa la maendeleo la SWEDEN-SIDA- Akizungumzia suala la kuimarisha mfumo wa maji halmashauri ya mji wa Kibaha itaanzisha mirad...

WAANDISHI PWANI WASHUTUMU AMUAJI YA MWENZAO.

WAANDISHI WASHUTUMU POLISI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/04/09/2012 Waandishi mkoa wa Pwani wamelaani hatua ya Jeshi la Polisi kumuua kwa makusudi mwandishi mwenzao, MAREHEMU DAUD MWANGOSI wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi. ... Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Pwani, BW. JOHN GAGARIN amesema kama inavyoonekana katika Picha ambayo waandishi wa habari wanaamini inaongea maneno 1000, ndivyo tunavyofundishwa darasani, inayoonyesha askari akimlenga BW. DAUD MWANGOSI waziwazi. BW. GAGARIN ameshangazwa na hatua ya Jeshi la Polisi kuunda tume ya kuchunguza mauaji hayo, kwani ni upotevu wa fedha za umma bure, kinachotakiwa ni kuwajibika kwa viongozi wa Jeshi hilo, kwa kuanzia na yule aliyempiga risasi kwa makusudi. Wakizungumza katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, Mmoja wa waandishi ambaye nimeongea naye, BW. OMARY MNGINDO amesema hatua hiyo ni mbinu za makusudi za Jeshi la Polisi kutaka kuwatisha waandishi wasifanye kazi yao kwa weledi na kuwafanya wananchi was...

BAVICHA WATAKA IGP MWEMA AACHIE NGAZI.

BAVICHA WATAKA IGP MWEMA AACHIE NGAZI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/09/03/14:56:56 Baraza la vijana la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA-BAVICHA mkoa wa Pwani, limemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kujiuzulu nafasi ambayo anayo kutokana na Jeshi hilo kushindwa kulinda wananchi na mali zao na kujihusisha zaidi na masuala ya kuua wananchi wasio na hatia kwa msukumo wa kisiasa. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA, BW. ELLISON KINYAHA amesema kumekuwepo na ongezeko la mauaji ya wananchi kila panapofanyika mikutano ya chama chao kwa lengo la kuwatisha wananchi, na ameelezea tukio la hivi karibuni kabisa la kuuliwa kwa mwandishi wa habarai wa Televisheni ya CHANNEL 10, BW. DAUD MWANGOSI kuwa ni ushahidi wa kushindwa kwa Jeshi hilo. BW. KINYAHA amebainisha kitendo hicho ni kielelezo tosha cha jinsi gani Jeshi la Polisi halizingatii haki za binadamu, kwa ajili kuwafurahisha wanasiasa wa chama tawala, ambao wameonesha kustushwa ...

SENSA-KIBAHA

SENSA YAENDELEA VIZURI KIBAHA Ben Komba/Pwani-Tanzania/28-08-2012 MKUU wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani Halima Kihemba amesema kuwa zoezi la sense linaendelea vizuri pamoja na kuwepo kwa changamoto kadhaa. Akizingumza na waandioshi wa habari ofisini kwake, amebainisha kuwa wananchi wameitikia vizuri hilo na kwamba wengi wamekubali kujiandikisha tofauti na ilivyofikiliwa hapo awali. Amesema kwamba kulikuwa na familia 25 korofi ambazo baada ya kupata taarifa zake viongozi walizifikia na kuzipatia elimu juu ya umuhimu wa sense na watu na makazi. “Kati ya hao kaya 12 zilikubali kuhesabiwa na zilizobaki zinaendelea kupatiwa elimu ili kuzishawishi kushiriki zoezi hilo linaloendelea kwa siku saba,” alisema Kihemba. Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi wilayani Kibaha mkoani hapa limetupiwa lawama kwa kutowakamata wachochezi wanaolipinga zoezi la sensa ili hali wakiwafahamu wanaosambaza nyaraka za uchochezi. Taarifa kuhusu wachochezo hao zimeshafika kwenye ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Pol...

SENSA TUHESABIWE.....

Image

SENSA YAANZA PWANI NA ONYO KWA WAKOROFI.

Image
BenKomba/Pwani-Tanzania/Sunday, August 26, 2012/19:38:46 Zoezi la sensa ya watu na makazi limeanza rasmi Katika mkoa wa Pwani na kuwepo na vipingamizi vidogo vidogo vilivyojitokeza na na kushughulikiwa na viongozi katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa manufaa ya Taifa. Leo ii mwandishi wa habari hizi ameshuhudia Mkuu wa mkoa wa Pwani BIBI. MWANTUMU MAHIZA akihesabiwa kama ilivyo ada inapofikia siku hii muhimu kitaifa, Ambapo baada ya kuhesabiwa amesema kuwa anajisikia fahari kuhesabiwa kwani anatambua kwamba yeye kuwa ni mtanzania halisi na wala sio suala la kuchosha na haijateteresha imani yake ya dini. Na amewataka wananchi kujitokeza kuhesabiwa bila kujali kampeni zinazoendeshwa na watu wasio itakia mema Tanzania kwa kivuli cha udini, Ingawa mpaka sasa hakuna vikwazo vyovyote ambavyo vimejitokeza, toka ulinzi wa kutosha uliwekwa katika maeneo yote ambayo yalikuwa na utata. Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Pwani BIBI. MAHIZA amewataka makarani wa sensa kuwa...