HALMASHAURI KUSAMBAZA MAJI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13-Nov-12/07:19:16 PM Halmashauri ya wilaya ya Kibaha katika mkoa wa Pwani imeanzisha mpango maalum wa usambazaji wa maji katika vijiji takriban 10, mradi amabao utagharimu fedha za Kitanzania zaidi ya milioni 300. Akiongea na mwandishi wa habari hizi mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BW. JUMA IBRAHIM amesema shughuli ambazo zinatarajiwa kutekelezwa katika hatua ya awali katika vijiji viwili vya NGETA na MSONGOLA, Ambapo katika kijiji cha Ngeta mradi unatarajia kujenga tanki la lita 100,000. Mbali ya ujenzi wa tenki hilo BW. IBRAHIMI amesema mabomba yenye urefu wa mita 737 ambalo litakuwa bomba kubwa litalogawanya maji katika vituo saba ambavyo vitakuwa na umbali wa mita 6040, sawa na ufungaji wa jenereta na pampu ya maji. BW. IBRAHIMU ameongeza katika kuhakikisha mradi huo unajiendesha idara ya maji halmashauri ya wilaya ya Kibaha itafunga mita katika kila kituo cha kusambaza maji, ikiwa na utoaji wwa mafunzo kwa kamati za maji za vijiji juu ya usimamizi na uendeshaji wa mradi wa maji, ambapo mpaka sasa mreadi huo wa maji upo katika hatua za mwisho. Kwa upande utekelezaji mradi huo katika kijiji cha Msongola, mita 12318 za mabomba zinatarajiwa usambazwa na ujenzi wa vituo sita vya kusambazia maji ikiwa pamoja na ufungaji wa mita ili kuwezesha wananchi kulipia huduma hiyo. Mradi huo ambao unafadhiliwa na wadau wa maendeleo, Benki ya Dunia, halmashauri ya wilaya ya Kibaha na serikali kuu na utakapokamilika utasaidia kupunguza tatizo la maji katika vijiji vya MWANABWITO, MADIMLA, KIKONGO na KISABI. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA

WANANCHI KIDIMU WAPINGA HATUA YA MKURUGENZI WA MJI KIBAHA.