Posts

Showing posts from August, 2014

TIBA ZA ASILI ZIPEWE KIPAUMBELE

Ben Komba/Pwani-Tanzania Serikali nchini imetakiwa kutoa kipaumbele kwa kazi za kitabibu zinazofanywa na watafiti wa tiba asili ili kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali yanayojitokeza na kusumbua binadamu. Mtafiti wa madawa asilia mwenye maskani yake,katika eneo la Magwila Chalinze BW.ABDALLAH MBEMBENUE amesema kuwa katika utafiti wake ambao ameufanya amebaini kwamba kuna miti dawa ambayo inaweza kufanya maajabu katika kutibu magonjwa mbalimbali. Akizunguimza na mwandishi wa habari hizi ambaye alifika kwa mtafiti watiba za asili kufuatia habari za kuponywa upofu kijana BW.SHOMARI KICHWECHWE ambaye alipata upofu toka Juni mwaka huu na kumfanya kuishi maisha ya mashaka kutokana na mabadiliko hayo ya kimaumbile ambayo ameyapata. BW.MBEMBENUE ameongeza kuw tiba za asili zina nafasi kubwa ya kuokoa maisha ya maelfu ya Watanzania iwapo wizara ya afya ikiwa makini na kukaa karibu na watafiti wa tiba asilia, ambapo kwa upande wake kuna magonjwa kadhaa ambayo hayampi shida k

VIFO VYA MAMA NA WATOTO VYAPUNGUA KIBITI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Tuesday, August 26, 2014 Kituo cha afya Kibiti wilayani Rufiji mkoa wa Pwani kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya kinamama na watoto wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua kutoka vifo 63 kwa mwaka hadi kufikia vifo 3.   Daktari msaidizi wa kituo hicho,BW.DKT CHAGI LYIMO amesema hayo alipokutana na waandishi wa habari 18 waliotembelea kituo hicho kutoka Dar es Saalam,Pwani na Morogoro ambapo wanapatiwa   mafunzo juu masuala ya afya ya uzazi na jinsia yaliondaliwa na shirika lisilo la kiserikali la WORLD LUNG FOUNDATION. BW.LYIMO amesema toka januari mpaka sasa hakuna mamamjamzito ambaye amefariki kutokana na matatizo ya uzazi,mafanikio hayo yametokana na usaidizi wanaopata kutoka WORLD LUNG FOUNDATION ambao wamewasaidia kwa njia moja au nyingine katika kuhakikisha wanapunguza vifo vya mama na mtoto.   Bw.LYIMO amebainisha juhudi ambazo WORLD LUNG FOUNDATION wamefanya, ni pamoja na kujengewa wodi ya uzazi,chumba cha upasuaji na k

VIFO VYA KINAMAMA NA WATOTO VYAPUNGUA PWANI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Tuesday, August 26, 2014 Kituo cha afya Kibiti wilayani Rufiji mkoa wa Pwani kimefanikiwa kwakiasi kikubwa kupunguza vifo vya kinamama na watoto wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua. Daktari msaidizi wa kituo hicho,BW.DKT CHAGI LYIMO amesema hayo alipokutana na waandishi wa habari 18 waliotembelea kituo hicho kutoka Dar es Saalam,Pwani na Morogoro ambapo wanapatiwa   mafunzo juu masuala ya afya ya uzazi na jinsia yaliondaliwa na shirika lisilo la kiserikali la WORLD LUNG FOUNDATION. Amefariki kutokana na matatizo ya uzazi,mafanikio hayo yametokana na usaidizi wanaopata kutoka WORLD LUNG FOUNDATION ambao wamewasaidia kwa njia moja au nyingine katika kuhakikisha wanapunguza vifo vya mama na mtoto. Bw.LYIMO amebainisha juhudi ambazo WORLD LUNG FOUNDATION, ni pamoja na kujengewa wodi ya uzazi,chumba cha upasuaji nakupatiwa gari la kubeba wagonjwa. Naye Mkunga wa kituo hicho,BI.DARIA NDUNGURU amefafanua kuwa yeye kwa nafasi yake ameshuhu

WAPINGA KULIPISHWA KODI AMBAYO IMESHAFUTWA

Ben Komba/Pwani=Tanzania/11:56 Umoja wa Wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni na mahoteli UGEHOKI mjini Kibaha wameilalamikia halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kuendelea kutoza kodi ambayo imefutwa kisheria. Katibu wa UGEHOKI, BW.RICHARD NGELEJA amesema hayo katika mkutano wa wanachama wa umoja huo uliofanyika katika ukumbi wa COUNTRYSIDE,Ambapo amenukuu majadliano ya kikao cha nane cha bunge cha tarehe 22 juni 2012. BW.NGELEJA amebainisha kuwa katika kikao hicho cha bunge ambacho kilijadili kuhusu ushuru wa hotel levy ipunguzwe kutoka 20% hadi 18% au 16%,na serikali inakamilisha zoezi lakuhuisha sheria ya utalii ya mwaka 2008 iliyoanza kutumika mwezi Julai,2009. Naye Mwenyekiti wa UGEHOKI, BW.FABIAN MAJAGA amebainisha kuwa wao wana vielelezo vyote vinavyoonyesha kufutwa kwa ushuru huo wa nyumba za wageni na mahoteli ikiwa pamoja hansard ya Bunge ambayo inaeleza wazi kufutwa kwa ushuru huo. BW.MAJAGA ameongeza kuwa hatua mbali mbali wamechukua ikiwa

FIVE STAR MODERN TAARAB YATISHA KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/ Kundi la muziki wa taarab la Five Star limeiteka mamlaka ya Mji mdogo wa Mlandizi baada ya kukaa kimya kwa kipindi Fulani kufutia ajali iliyoua wanamuziki wao 13. Kiongozi wa kundi hilo, BW.ALLY JUMA amesema pembeni ya ukumbi wa CONTAINER BAR Mlandizi kuwa wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo ya Taarab kuwaunga mkono na kutosikiliza maneno ya watu wasiowatakia mema bendi hiyo. Ameshauri vikundi vya muziki wa taarabu kujitokeza na kuunda umoja ambao utaangalia maslahi yao na kulinda haki zao, kutokana watu wengi kuiba kazi za wasaanii na kuwanyima mapato kutokana na wizi huo. Nye Mkurugenzi wa ukumbi huo wa CONTAINER BAR Mlandizi,BW.FRANK MWALEMBWE ameelezea nia yake ya kuhakikisha kuwa kunakuwepo na burudani kila miwsho wa wiki katika ukumbi huo ili kutoa fursa kwa wasanii wa Tanzania kuonyesha uwezo wao. END.