Posts

Showing posts from December, 2012

CERVICAL CANCER

Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-Dec-12/00:45:48 Imesemekana mjini Kibaha kumekuwepo na tatizo kubwa la kansa ya shingo ya uzazi, ambapo katika kila mwaka watu 500,000 wanaogundulika kuwa na kansa ya shingo ya uzazi 275000 wanakufa kila mwaka. Msimamizi wa Kitengo cha kansa ya shingo ya uzazi kituo cha afya mkoani mjini Kibaha, BI. JULIETH SANGA amesema tatizo hilo kwa sasa ni kubwa kwa kiwango cha asilimia 50.9/100,000 na vifo vinavyosababishwa navyo ni wastani 37.5/100,000. BIBI.SANGA amebainisha kuwa kutokana na takwimu hizo ugonjwa huo umekuwa tishio kwa kinamama na mzigo kwa wanaougua na wanaouguza kwani Tanzania imekuwa iko juu kulinganisha na nchi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla wake. BIBI. SANGA amefafanua chanzo cha ugonjwa huo ni kuanza mapenzi katika umri mdogo na hasa wanapokutana na mwanaume mwenye virus vya PAPPILOMA wanaoishi katika mwili wa mwanaume bila kumletea madhara. Amesisitiza hatari ya maambukizi inazidi kwa mwanamke kuwa na wapenzi wengi, ma

KANSA YA SHINGO YA KIZAZI TISHIO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-Dec-12/00:45:48 Imesemekana mjini Kibaha kumekuwepo na tatizo kubwa la kansa ya shingo ya uzazi, ambapo katika kila mwaka watu 500,000 wanaogundulika kuwa na kansa ya shingo ya uzazi 275000 wanakufa kila mwaka. Msimamizi wa Kitengo cha kansa ya shingo ya uzazi kituo cha afya mkoani mjini Kibaha, BI. JULIETH SANGA amesema tatizo hilo kwa sasa ni kubwa kwa kiwango cha asilimia 50.9/100,000 na vifo vinavyosababishwa navyo ni wastani 37.5/100,000. BIBI.SANGA amebainisha kuwa kutokana na takwimu hizo ugonjwa huo umekuwa tishio kwa kinamama na mzigo kwa wanaougua na wanaouguza kwani Tanzania imekuwa iko juu kulinganisha na nchi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla wake. BIBI. SANGA amefafanua chanzo cha ugonjwa huo ni kuanza mapenzi katika umri mdogo na hasa wanapokutana na mwanaume mwenye virus vya PAPPILOMA wanaoishi katika mwili wa mwanaume bila kumletea madhara. Amesisitiza hatari ya maambukizi inazidi kwa mwanamke kuwa na wapenzi wengi, ma

WAZAZI WATAKA KURUDISHIWA MALI ZAO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/25-Dec-12/22:57:12 Wanachama wa wa Jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi mjini Kibaha wamemtaka mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kuirudisha shule ya wazazi ya Sekondaro Kaole iliyopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani kurudishwa kwa mikononi mwa Jumuiya hiyo. Akizungumza katika kikao cha Baraza la Jumuiya ya wazazi kata ya Kongowe mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya jumuiya hiyo kata ya Kongowe, DR. NASSORO KAZAMBO ameitaka serikali ya chama cha mapinduzi kurudisha shule hiyo kwa jumuiya ya wazazi ili kutoa fursa kwa jumiya hiyo kuingia ubia na mashirika mbalimbali ili kuziendesha shule hizo. DR. KAZAMBO amesema kitendo cha kupora mali za jumuiya ya wazazi na baadaye kubezwa kuwa ni jumuiya ambayo haitoshi hilo halikubaliki na hasa ikizingatiwa kuwa jumuiya hiyo ni tajiri na kinachosokana ni usimamizi wa mali hizo na kwa kuingia ubia na watu mbalimbali katika kuzisimamia na kuziendesha. Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mjin

GREETINGS

HAPPY XMAS & NEW YEAR

X MAS

Ben Komba/Pwani-Tanzania/24-Dec-12/18:14:46 Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Pwani limesema kuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mkoa na halmashauri zake katika kipindi hiki cha Krismas ambapo leo kutakuwa na misa za mkesha tayari kwa sikukuu hiyo ya kuzaliwa mwokozi YESU KRISTO kama inavyoaminika na mabilioni ya wakristu ulimwenguni Akiongea na mwandishi wa habari hizi msemaji wa Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani, INSPEKTA ATHUMAN MTASHA ambapo amesema siku kama hizi kunakuwepo na mikusanyiko ya watu wengi hasa maeneo ya makanisani na baa. INSPEKTA MTASHA amewataka wazazi kutotoka wote majumbani kuepuka kutoa fursa kwa wahalifu kufanya madhara, na ameaasa kama watu watatoka itakuwa vyema anayebaki nyumbani kuwa na simu iwapo tatizo lolote litakalojitokeza atoe taarifa linapotokea tatizo. Akizungumzia kuhusiana wenye magari amewataka madereva kupaki maeneo ambayo yapo salama na kuheshimu sheria za usalama barabarani katika kipindi hiki cha sikukuu kutokana na baadhi

BENKI YA VIJANA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-Dec-12/09:58:38 Vijana mjini Kibaha watafaidika kutokana na hatua ya kuanzishwa benkia ya vijana ambayo itkuwa inajishughulisha na kuwawezesha vijana kwa kuwapatia uwezeshaji wa hali na maki katika kuwasaidia kujikwamua nahali ngumu ya maisha inayowakabili kada hiyo katika jamii. Mratibu wa Benki ya vijana wilayani Kibaha, BI. LULU MKOMAMBO amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa makusudi katika kumwezesha kijana kujikwamua na hali duni aliyonayo, na hasa ikizingatiwa vijana ndio kundi kubwa ambao wanakadiriwa kuwa asilimia 60 ya wakazi jumla ya wa Tanzania. Bi. LULU amesema maeneo mengine yameshaanza kufaidika na Beki hiyo kwa vijana waliobahatika kukopeshwa pikipiki kwa masharti ya kuwasilisha shilingi laki tano na kupatiwa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.8, ambapo kijana atatakiwa kulipa kiasi kilichobaki kwa kadiri ya makubaliano. Amefafanua kuwa kijana atawajibika kutoa fedha za fomu ambayo ni shilingi 20,000/=, a,bazo atalipa mara ba

MWENYEKIT UVCCM AKANUSHA UVUMI DHIDI YAKE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Friday, December 21, 2012/18:20:03 Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mjini Kibaha, BW.IDD KANYALU amekanusha uvumi wa kuwa yeye amekamatwa kwa jinai na kupelekwa Tanga kitu ambacho amethibitisha kuwa sio kweli. Akiongea na mwandishi wa habari hizi, BW. KANYALU amesema siasa ni mchezo mchafu na huwezi kumjua mbaya wako, na ameomba kama mtu yoyote ana madai kama hayo na athibitishe, kwani uchaguzi umemalizika hivi karibuni na makundi bado yapo. Bw.KANYALU amesema masuala hayo kweli yamezagaa katika lengo zima la kupakana matope kutokana na wanachama wa chama hicho kung'ang'ania makundi yaliyokuwapo wakati wa kampeni wa chaguzi za ndani za chama hicho, na kutokana na makundi kuna bomoa hali ya umoja na mshikamano iliyokuwepo hapo awali kabla ya mfumo wa vyama vingi kuingia nchini. Amewaasa wana CCM kuwa kitu kimoja na kuimarisha upendo na mshikamano ndani ya chama hicho, na si vyema kwa wanachama wa chama hicho kuchafuana kwa m

MBUNGE AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KIBAHA MJINI.

Image

DOUBLE STANDARD

DOUBLE STANDARD Ben Komba/Pwani-Tanzania/16 December, 2012/18:32:08 Baraza vijana mkoa wa Pwani limewakana wale ambao wanadai kutoka baraza hilo katika Mkoa wa Mwanza wanaoshinikiza Katibu wa Chama hicho, DR. WILBROAD SLAA ajiuzulu kutokana na yeye kuwa na kadi ya CCM. Mwenyekiti wa Baraza la vijana Mkoa wa Pwani, BW. ELLISON KINYAHA amesema kuwa mkoa wa Pwani hautambui watu hao wanaojiita viongozi wa BAVICHA mkoa wa Mwanza na siku zote wataambatana na Katibu wao DR. WILBROAD SLAA ambaye mpaka sasa ameonyesha nia ya kweli ya kumkomboa Mtanzania, na kuwachukulia watu wanaompinga kama mamluki ambao wamekosa kazi ya kufanya, na hata katika mkoa wa Pwani wapo wanaozunguka kumpiga vita Katibu wao. BW. KINYAHA amefafanua katika operesheni ya mwezi wa tatu, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ubunge katika uchaguzi uliopita aliondoka katika mazingira ya kutatanisha na fedha alizokabidhiwa kwa ajili ya mafuta ya magari yatayotumika kuendesha operesheni hiyo ya kukinadi chama. Aidha amese

MBUNGE AHIMIZA UPENDO NA UMOJA CCM.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-Dec-12/17:03:00 Mbunge wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW. SYLVESTER KOKA amewataka wanaCCM MJINI Kibaha mjini kutoogopa kuwakosoa viongozi wake moja kwa moja badala ya kusemea pembeni na kutoa fursa kwa maadui kukidhoofisha chama chao. Ameyasema hayo akiwa katika ziara maalum ya kuimarisha uhai wa chama mjini Kibaha katika kata ya Mailimoja Tawi la TAMCO, BW. KOKA amesema tabia ya baadhi ya wana CCM kutotumia nafasi yao kama wanachama wa chama hicho kuongea na viongozi juu ya mambo mbalimbali ambayo wanayafahamu na badala yake kwenda kuongea mahali ambapo hapastahili ndio zinazokichimbia karibu chama hicho. BW. KOKA ametoa mfano wa kuwa haiwezekani Mzazi akaenda kumsifia mwanaye kama labda analala nje kwa jirani yake badala ya kujadili suala lile na mwanae, kwani kwa kumueleza vile jirani hakutasaidia kurekebisha hali ya mambo badala yake inaweza kusababisha mambo kuharibika zaidi. Mbunge huyo wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW. SYLVESTER KOK

CCM WAHIMIZA VIKAO VYA NDANI YA CHAMA.

Ben Komba/16 December 2012/23:32:44 Chama cha mapinduzi mjini Kibaha kimeonywa kuwa kisimtafute mchawi kitakapofanya vibaya katika uchaguzi mkuu ujao, kutokana na viongozi wa ngazi za matawi na Kata kutozingatia vikao vya kikatiba. Mwenyekiti wa CCM, Kibaha mjini BW. MAULID BUNDALA amesema hayo akiwa katika ziara yake ya kukiimarisha chama katika kata ya Picha ya Ndege. BW. BUNDALA amefafanua kutokana na mweleko anaona sasa kuna kila dalili ya viongozi na wanachama wa CCM wenyewe kuwa chachu ya kushindwa kwa chama hicho katika chaguzi zijazo. Ameongeza toka mwanzo wa ziara yake amekatishwa tama na baadhi ya matawi kushindwa kuitisha vikao vya wanachama ili kuweza kutathimini utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama. BW. BUNDALA ameyasifu matawi ya Picha ya Ndege B na Lulanzi kwa kuonyesha uhai wa chama katika maeneo hayo, na amewaonya viongozi ambao wamekuwa na tabia ya kutoroka vikao kwa visingizio mbalimbali. END.

WALIOJITA BAVICHA WASUTWA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/16 December, 2012/18:32:08 Baraza vijana mkoa wa Pwani limewakana wale ambao wanadai kutoka baraza hilo katika Mkoa wa Mwanza wanaoshinikiza Katibu wa Chama hicho, DR. WILBROAD SLAA ajiuzulu kutokana na yeye kuwa na kadi ya CCM. Mwenyekiti wa Baraza la vijana Mkoa wa Pwani, BW. ELLISON KINYAHA amesema kuwa mkoa wa Pwani hautambui watu hao wanaojiita viongozi wa BAVICHA mkoa wa Mwanza na siku zote wataambatana na Katibu wao DR. WILBROAD SLAA ambaye mpaka sasa ameonyesha nia ya kweli ya kumkomboa Mtanzania, na kuwachukulia watu wanaompinga kama mamluki ambao wamekosa kazi ya kufanya, na hata katika mkoa wa Pwani wapo wanaozunguka kumpiga vita Katibu wao. BW. KINYAHA amefafanua katika operesheni ya mwezi wa tatu, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ubunge katika uchaguzi uliopita aliondoka katika mazingira ya kutatanisha na fedha alizokabidhiwa kwa ajili ya mafuta ya magari yatayotumika kuendesha operesheni hiyo ya kukinadi chama. Aidha amesema wazi ku

M4C YAVAMIA KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/14-Dec-12/19:25:28 Chama cha demokrasia na maendeleo kimezindua rasmi kampeni yake ya vuguvgu la mabadiliko mjini Kibaha kwa kuwataka wananchi kuchukua hatua ili kuleta mabadiliko ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya nchi yetu. Akiongea katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya mpira Maili Moja, Mbunge wa Ubungo, BW. JOHN MNYIKA amesema wakati ni huu kwa wale wanaoteseka katika nchi hii kunga mkono kampeni ya vuguvugu la mabadiliko ili kuyaona mabadiliko ambayo mnataka kuyaona. BW. MNYIKA amebainisha kuwa ili kuwa wakala wa mageuzi inabidi kila mtu awajibike katika eneo lake kama ni Mwalimu awe wakala wa mabadiliko katrika eneo lake, na kama ni askari basi awe wakala wa mabadiliko katika eneo lake halikadhalika wamachinga na jamii nzima kwa ujumla. Mbunge huyo wa Ubungo ameongeza kuwa wananchi wamekuwa wakiona misukosuko mbalimbali ikiwakabili viongozi wa CHADEMA, kama mauaji ya Morogoro, mauaji ya Mwandishi DAUD MWANGOSI, yaliyomkuta DR.

ZING ZONG STORY

Ben Komba/Pwani-Tanzania/11-Dec-12/17:51:23 Mkazi wa Picha ya Ndege mjini Kibaha, BW. HEZRON MWANSASU amefikishwa mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mkoa wa Pwani akituhumiwa kwa kosa la kumuingilia kinyume cha maumbile mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 7 ambaye alikuwa anaishi naye. Akisomewa shtaka mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mkoa, BW. ESTOMI KISANGA na Mwendesha mashtaka, BW. JONAS SIRA inadaiwa tarehe 24 Novemba mwaka huu majira ya saa tano usiku huko maeneo ya Picha ya Ndege mjini Kibaha mkoa wa Pwani mshtakiwa alimuingilia kinyume cha maumbile mtoto huyo mwenye umri wa miaka 7 ambaye jina lake limehifadhiwa na kumsababishia maumivu makali. Hakimu mfawidhi wa Mkoa BW. ESTOMI KISANGA aliahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 21 Desemba mwaka huu na mshtakiwa yupo nje kwa dhamana. END.