DOUBLE STANDARD
DOUBLE STANDARD
Ben Komba/Pwani-Tanzania/16 December, 2012/18:32:08
Baraza vijana mkoa wa Pwani limewakana wale ambao wanadai kutoka baraza hilo katika Mkoa wa Mwanza wanaoshinikiza Katibu wa Chama hicho, DR. WILBROAD SLAA ajiuzulu kutokana na yeye kuwa na kadi ya CCM.
Mwenyekiti wa Baraza la vijana Mkoa wa Pwani, BW. ELLISON KINYAHA amesema kuwa mkoa wa Pwani hautambui watu hao wanaojiita viongozi wa BAVICHA mkoa wa Mwanza na siku zote wataambatana na Katibu wao DR. WILBROAD SLAA ambaye mpaka sasa ameonyesha nia ya kweli ya kumkomboa Mtanzania, na kuwachukulia watu wanaompinga kama mamluki ambao wamekosa kazi ya kufanya, na hata katika mkoa wa Pwani wapo wanaozunguka kumpiga vita Katibu wao.
BW. KINYAHA amefafanua katika operesheni ya mwezi wa tatu, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ubunge katika uchaguzi uliopita aliondoka katika mazingira ya kutatanisha na fedha alizokabidhiwa kwa ajili ya mafuta ya magari yatayotumika kuendesha operesheni hiyo ya kukinadi chama.
Aidha amesema wazi kuwa BW. HABIB MCHANGE ndiye ambaye amefanya hivyo katika harakati za kukidhoofisha chama mkoa wa Pwani, na ndio hao wanaoingia katika mitandao na kumchafua DR. SLAA kwa kuficha majina yao halisi, na kutokana na vitendo hivyo ameishauri kamati kuu ya Chama hicho inayokutana kwa sasa mjini Dar eEs Saalam kulifanyia kazi suala hilo kwa kuwaadhibu wote watakaobainika kutaka kukichafua chama hicho na viongozi wake.
END.
Comments
Post a Comment