Posts

Showing posts from May, 2017

HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA KUFANYA TATHMINI UHARIBIFU BARABARA

Image

WANANCHI WAJITOLEA KUKARABATI KIPANDE CHA BARABARA MLANDIZI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/28/05/2017 15:56:54 Wananchi katika mji wa Mlandizi wamejitolea kutengeneza miundombinu ya barabara iliyoharibika kufuatia mvua kubwa zilizonyesha kwa takriban miezi miwili  nchini. Wakazi hao wa Mlandsizi Mtongani waliungana kwa  umoja kukarabati kipande hicho cha barabara ambacho kilikuwa na kalavati lililozidiwa nguvu na maji yaliyokuwa yananatiririka na kuzidi kiasi cha kupita pembeni na kusababisha  kumeguka kwa barabara hiyo inayounganisha vitongoji vya Msagasa na Mtongani. Mmoja wa wakazi wa eneo BW.KONDO MGEGEDA amesema kipande hicho cha barabara kinachounganisha vijiji vya Mlandizi na kuelekea maeneo ya Disunyala na Mzenga kiliharibika katika kipindi cha mvua  na kusababisha usumbufu mkubwa kwa magari yaliyotaka kwenda maeneo hayo. Hivyo kwa kuliona hilo wakaamua kuita msaragambo kwa ajili ya kukarabati eneo hilo ili kuwezesha usafiri wa pikipiki kupita maeneo hayo katika kupunguza  makali ya tatizo hilo. BW. MGEGEDA ameonmgeza

RAIS MAGUFULI AMWAGIWA SIFA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/27/05/2017 09:44:00 Rais JOHN POMBE MAGUFULI amepongezwa kufuatia hatua mbalimbali anazochukua  kukabiliana na upotevu wa fedha za mchanga wa madini ambao uliokuwa unaigharimu nchi zaidi ya matrilioni  ya shilingi zilizokuwa zinapotea kwenye baadhi ya mikono ya watumishi wa serikali wasio waaminifu. Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE la mjini Kibaha, BW.ISRAEL ILUNDE ameyasema hayo wakati  akizungumza na mwandishi wa habari hizi pembeni mwa jukwaa la ufahamu wa kiraia linalofanyika kila  ya ijumaa ya mwisho wa mwezi. Ambapo amesema hatua ambazo amekuwa akizichukua kudhibiti uvujaji wa mapato mbalimbali hazina budi kuungwa mkono na umma wa Watanzania kwani zitawezesha nchi kuelekea katika maendeleo endelevu kwa ustawi wa n chi katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii. Bw. ILUNDE ameongeza kitendo chake cha kutofumbia macho vitendo hivyo ni ishhara tosha ya kuonyesha lengo lake la kutaka kuikw

FATHERHOUSE CORNER STUDIO

Image

SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LALAMIKIWA URASIMU MALIPO YA WAKANDARASI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/04/05/2017 09:53:24 Baadhi ya wazabuni wanaofanya kazi na Shirika la Elimu Kibaha wamelalamikia kitengo cha ukaguzi kwa kuwakata fedha ambazo wamepatana kulipwa kwa zabuni wanapewa kwa visingizio ambavyo havina mantiki. Uchunguzi ambao umefanywa na mwandishi wa habari hizi kwa takribani wiki mbili kufuatia malalamiko ya mmoja wa wazabuni ambaye alipatiwa kazi ya kufanya matengenezo katika chumba cha kuzalishia dripu za kwa ajili ya wagonjwa, BW.KABUGI MNDEME na baadaye kulipwa nusu ya fedha iliyopo katika makubaliano. BW.MNDEME amesema kuwa yeye aliingia makubaliano ya kuweka milango na madirisha  ya aluminium katika chumba hicho cha kuzalisha dripu za maji ya kuongezewa wagonjwa kupitia LPO No. 20161163 ambapo kwa upande wake ametimiza wajibu na kukamilisha  matengenezo hayo ambayo gharama yake halisi ilikuwa shilingi 5,892,500.00. BW.MNDEME ameongeza kuwa cha kushangaza mara kazi ilipokamilika ndipo urasimu wa malipo ulipoanza, kukaanza kuzuka