WANANCHI WAJITOLEA KUKARABATI KIPANDE CHA BARABARA MLANDIZI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/28/05/2017 15:56:54
Wananchi katika mji wa Mlandizi wamejitolea kutengeneza
miundombinu ya barabara iliyoharibika kufuatia mvua kubwa zilizonyesha kwa
takriban miezi miwili nchini.
Wakazi hao wa Mlandsizi Mtongani waliungana kwa umoja kukarabati kipande hicho cha barabara
ambacho kilikuwa na kalavati lililozidiwa nguvu na maji yaliyokuwa
yananatiririka na kuzidi kiasi cha kupita pembeni na kusababisha kumeguka kwa barabara hiyo inayounganisha
vitongoji vya Msagasa na Mtongani.
Mmoja wa wakazi wa eneo BW.KONDO MGEGEDA amesema kipande
hicho cha barabara kinachounganisha vijiji vya Mlandizi na kuelekea maeneo ya
Disunyala na Mzenga kiliharibika katika kipindi cha mvua na kusababisha usumbufu mkubwa kwa magari
yaliyotaka kwenda maeneo hayo.
Hivyo kwa kuliona hilo wakaamua kuita msaragambo kwa ajili ya
kukarabati eneo hilo ili kuwezesha usafiri wa pikipiki kupita maeneo hayo
katika kupunguza makali ya tatizo hilo.
BW. MGEGEDA ameonmgeza kuwa Diwani wa eneo hilo, BIBI.HABIBA
MFALAMAGOHA alifika eneo hilo na kuahidi kulishughulikia tatizo hilo ili
kuwezesha barabara hiyo kupitika.
INSERT:WANANCHI WALIOJITOLEA
END
Comments
Post a Comment