WAPINGA KULIPISHWA KODI AMBAYO IMESHAFUTWA
Ben Komba/Pwani=Tanzania/11:56
Umoja wa Wafanyabiashara wa nyumba
za kulala wageni na mahoteli UGEHOKI mjini Kibaha wameilalamikia halmashauri ya
mji wa Kibaha kwa kuendelea kutoza kodi ambayo imefutwa kisheria.
Katibu wa UGEHOKI, BW.RICHARD
NGELEJA amesema hayo katika mkutano wa wanachama wa umoja huo uliofanyika
katika ukumbi wa COUNTRYSIDE,Ambapo amenukuu majadliano ya kikao cha nane cha
bunge cha tarehe 22 juni 2012.
BW.NGELEJA amebainisha kuwa katika
kikao hicho cha bunge ambacho kilijadili kuhusu ushuru wa hotel levy ipunguzwe
kutoka 20% hadi 18% au 16%,na serikali inakamilisha zoezi lakuhuisha sheria ya
utalii ya mwaka 2008 iliyoanza kutumika mwezi Julai,2009.
Naye Mwenyekiti wa UGEHOKI,
BW.FABIAN MAJAGA amebainisha kuwa wao wana vielelezo vyote vinavyoonyesha
kufutwa kwa ushuru huo wa nyumba za wageni na mahoteli ikiwa pamoja hansard ya
Bunge ambayo inaeleza wazi kufutwa kwa ushuru huo.
BW.MAJAGA ameongeza kuwa hatua mbali
mbali wamechukua ikiwa pamoja na kwenda kumuona Mkurugenzi wa halmashauri ya
mji wa Kibaha, BW.JENIFA OMOLO na Ofisa biashara bila mafanikio yoyote.
Mkurugenzi wa
halmashauri ya mji wa Kibaha BI.JENIFA OMOLO alipopigiwa simu na mwandishi wa
habari hizi ili kupata ufafanuzi zaidi juu madai ya wafanyabiashara hao,amesema
anachojua yeye ni kuwa kulikuwa na kesi mahakamani na wafanyabiashara hao
kushindwa na hivyo hana lolote la kusema kuhusina na suala hilo.
END.
Comments
Post a Comment