VIFO VYA MAMA NA WATOTO VYAPUNGUA KIBITI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Tuesday, August 26, 2014

Kituo cha afya Kibiti wilayani Rufiji mkoa wa Pwani kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya kinamama na watoto wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua kutoka vifo 63 kwa mwaka hadi kufikia vifo 3.
 
Daktari msaidizi wa kituo hicho,BW.DKT CHAGI LYIMO amesema hayo alipokutana na waandishi wa habari 18 waliotembelea kituo hicho kutoka Dar es Saalam,Pwani na Morogoro ambapo wanapatiwa  mafunzo juu masuala ya afya ya uzazi na jinsia yaliondaliwa na shirika lisilo la kiserikali la WORLD LUNG FOUNDATION.

BW.LYIMO amesema toka januari mpaka sasa hakuna mamamjamzito ambaye amefariki kutokana na matatizo ya uzazi,mafanikio hayo yametokana na usaidizi wanaopata kutoka WORLD LUNG FOUNDATION ambao wamewasaidia kwa njia moja au nyingine katika kuhakikisha wanapunguza vifo vya mama na mtoto.
 
Bw.LYIMO amebainisha juhudi ambazo WORLD LUNG FOUNDATION wamefanya, ni pamoja na kujengewa wodi ya uzazi,chumba cha upasuaji na kupatiwa gari la kubeba wagonjwa.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA