Posts

Showing posts from June, 2014

MKUU WA MKOA WA PWANI AZINDUA VIATAMBULISHO VYA URAIA.

Image
  Ben Komba/Pwani-Tanzania/30/6/2014 Mkuu wa mkoa wa Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA amepongezea hatua ya serikali ya kutoa vitambulisho vya uraia ili kuweza kutambua wageni na raia halali wa nchi hii ya Tanzania.   Akizungumza katika kipindi cha uzinduzi wa usajili wa watu mkoa wa Pwani, BI.MAHIZA amesema jukumu hilo linaloratibiwa na NIDA ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi na ni maelekezo ya serikali ya awamu ya nne.   Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani, BI.MAHIZA amewasisitiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha jukumu hilo linatekelezeka kama serikali ilivyoaagiza, kwa kuipa NIDA ushirikiano wa hali na mali ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa vitambulisho vya uraia.   Ameagiza iwapo kutakuwa na tatizo lolote amewataka watendaji kumpa taarifa katika kipindi mwafaka, ili kuepuka kukwamisha zoezi hilo muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya Taifa letu.   Awali akizungumza kukmaribisha Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mkurugenzi wa mamlaka ya

TALAWANDA YAZITOA HOFU TAASISI ZA MOKOPO

Na Omary Mngindo, Bagamoyo Juni 29 SERIKALI Kata ya Talawanda wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imezitoa hofu taasisi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kwamba itawasimamia ipasavyo wakazi ndani ya Kat hiyo watakaoomba mikopo ili kuhakikisha wanairejesha kwa wakati. Diwani wa Kata hiyo Bw. Said Zikatimu ameyasema hayo juzi akifungua mafunzo ya siku moja kwa wajasiriamali wapatao 293 kupitia vikundi 58 ndani ya Kata yaliyoendeshwa na taasisi ya TAGIDOyenye makazi yake wilayani humo inayojihusisha na utoaji wa elimu hiyo ikishirikiana na tasisi za kifedha lengo kuviinua vikundi mbalimbali. "Niwahakikishie kwamba serikali ya Kata itashirikiana na bega kwa bega na viongozi wake ngazi mbalimbali ili kuhakikisha vikundi vyote vitakavyokopa tunavisimamia ipasavyo na hatimaye mikopo inarejeshwa kwa wakati hivyo niwaondoe hofu juu hilo," alisema Zikatimu. Aliongeza kuwa katika vikundi hivyo vyote vimesajiliwa na vina hati kutoka kwa msajili mwenye dhamana na kwa sasa vinaendelea na m

TAGIDO YAWANOA WAKAZI TALAWANDA

Na Omary Said, Bagamoyo Juni 30 TAASISI ya TAGIDO inayojihusisha na utoaji wa elimu ya ujasiriamali wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani juzi imeendesha mafunzo ya siku moja kwa vikundi 58 vyenye wanachama 293 ndani ya Kata ya Talawanda wilayani hapa. Akizungumza kwenye mafunzo hayo katika kijiji cha Magulumatali ofisa wa TAGIDO Hamza Mfuame alisema kuwa wamekuwa wakiendesha mafunzo ambayo yamekuwa na faida kwa vikundi na wanachama ambapo tayari vikundi vimenufaika na mikopo kupitia taasisi mbalimbali za kifedha. "Asasi yetu ambayo ina makao yake Bagamoyo imejikita zaidi katika utoaji wa mafunzo kwa vikundi vya ujasiriamali ambapo vikundi mbalimbali na wanachama wake wamenufaika na elimu hii na hatimaye kukopa fedha na kujikwamua kwenye shughuli za kimaendeleo," alisema Mfaume. Nae Mwakilishi wa NMB Mark Andulu alisema kwamba uongozi wa Makao Makuu wa benki umeelekeza nguvu zake maeneo ya vijijini kwa lengo la kuwafikia wakazi wake ambao wanahitaji huduma hiyo na kuwa kuna akaunt

UZINDUZI WA VITAMBULISHO VYA URAIA WAFANYIKA PWANI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/30/6/2014 Mkuu wa mkoa wa Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA amepongezea hatua ya serikali ya kutoa vitambulisho vya uraia ili kuweza kutambua wageni na raia halali wa nchi hii ya Tanzania. Akizungumza katika kipindi cha uzinduzi wa usajili wa watu mkoa wa Pwani, BI.MAHIZA amesema jukumu hilo linaloratibiwa na NIDA ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi na ni maelekezo ya serikali ya awamu ya nne. Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani, BI.MAHIZA amewasisitiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha jukumu hilo linatekelezeka kama serikali ilivyoaagiza, kwa kuipa NIDA ushirikiano wa hali na mali ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa vitambulisho vya uraia. Ameagiza iwapo kutakuwa na tatizo lolote amewataka watendaji kumpa taarifa katika kipindi mwafaka, ili kuepuka kukwamisha zoezi hilo muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya Taifa letu. Awali akizungumza kukmaribisha Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambuli

WADAU WATAKIWEA KUJITOKEZA KUSAIDIA MICHEZO-VIDEO

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania   Naibu Waziri TAMISEMI BW.KASSIM MAJALIWA ametoa wito kwa mashirika na taasisi binafsi kushirikiana na serikali katika kuboresha mashindano ya UMITASHUMTA, kwani huko ndiko kunakotoka vipaji wanavyoviona leo hii.   Naibu Waziri MAJALIWA amesema hayo wakati wa ufunguzi wa michezo ya 22 ya UMITASHUMTA inayofanyika katika Mkoa wa Pwani, ambapo amewataka watu binafsina mashirika kushirikiana serikali katika kuboresha michezo nchini.   Aidha amezitaka halmashauri kuzuia uvamizi wa viwanja vya shule kunakofanywa na wananchi wenyewe, kutokana na hapo nyuma serikali kusitisha shughuli za michezo na baadhi ya wtu kuchukua fursa hiyo kupora vilivyokuwa viwanja vya michezo.   Awali akizungumza katika ufunguzi huo, Mkurugenzi msaidizi elimu ya msingi nchini, BW.ABDUL MAULID alimuomba Waziri kuchukua hatua kudhibiti uporaji wa viwanja vya michezo kwa kuwahimiza wakurugenzi wa halmashauri kuvilinda viwanja vya michezo.   END

ANAHITAJI MSAADA AKATIBIWE MARADHI YANAYOMSIBU

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-6-2014 Mkazi wa Kitongoji cha Kisogo katika kata ya Vigwaza, Tarafa ya Msoga wilayani Bagamoyo, BI SELATIAN NATA ameombva msaada kwa watu mbalimbali ili aweze kwenda kutibiwa mguu ambao umevimba. BI SELATIAN amesema yeye alizaliwa mzima wa afya bilka kuwa na kasoro yoyote mpaka alipofika umri wa miaka 16, ndipo alipotokwa na kipele kidogo ambacho kilikuwa kinamuasha na alipokuwa anakuna mguu ulianza kuvimba. BI,SELATIAN awali alikuwa ameolewa lakini hali ilipozidi kuwa mbaya ilibidi arudishwe nyumbani kwao ambapo anaishi mpaka sasa akiwa na mtoto mdogo wa miezi nane, ameongeza kuwa mguu huo umekuwa unamsababishia maumivu makali yanayoambatana na homa kali, Naye Baba wa BI, SELATIAN, BW,MUMBI NATA amebainisha kuwa mtoto wake alizaliwa mzima na hakuwa na kasoro yoyote mpaka alipofikisha miaka 16 ndipo alipopatwa na matatizo hayo, mpaka sasa wameshafanya juhudi mbalimbali kumsaidia. BW.NATA amewaomba wasamaria wema kujitokeza ku

VIWANJA VYA MICHEZO VILINDWE WAAGIZWA MA-DED

Ben Komba/Pwani-Tanzania   Naibu Waziri TAMISEMI BW.KASSIM MAJALIWA ametoa wito kwa mashirika na taasisi binafsi kushirikiana na serikali katika kuboresha mashindano ya UMITASHUMTA, kwani huko ndiko kunakotoka vipaji wanavyoviona leo hii.   Naibu Waziri MAJALIWA amesema hayo wakati wa ufunguzi wa michezo ya 22 ya UMITASHUMTA inayofanyika katika Mkoa wa Pwani, ambapo amewataka watu binafsi na mashirika kushirikiana serikali katika kuboresha michezo nchini.   Aidha amezitaka halmashauri kuzuia uvamizi wa viwanja vya shule kunakofanywa na wananchi wenyewe, kutokana na hapo nyuma serikali kusitisha shughuli za michezo na baadhi ya watu kuchukua fursa hiyo kupora vilivyokuwa viwanja vya michezo.   Awali akizungumza katika ufunguzi huo, Mkurugenzi msaidizi elimu ya msingi nchini, BW.ABDUL MAULID alimuomba Waziri kuchukua hatua kudhibiti uporaji wa viwanja vya michezo kwa kuwahimiza wakurugenzi wa halmashauri kuvilinda viwanja vya michezo.   END --

AOMBA MSAADA AKATIBIWE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-6-2014 Mkazi wa Kitongoji cha Kisogo katika kata ya Vigwaza, Tarafa ya Msoga wilayani Bagamoyo, BI SELATIAN NATA ameombva msaada kwa watu mbalimbali ili aweze kwenda kutibiwa mguu ambao umevimba. BI SELATIAN amesema yeye alizaliwa mzima wa afya bilka kuwa na kasoro yoyote mpaka alipofika umri wa miaka 16, ndipo alipotokwa na kipele kidogo ambacho kilikuwa kinamuasha na alipokuwa anakuna mguu ulianza kuvimba. BI,SELATIAN awali alikuwa ameolewa lakini hali ilipozidi kuwa mbaya ilibidi arudishwe nyumbani kwao ambapo anaishi mpaka sasa akiwa na mtoto mdogo wa miezi nane, ameongeza kuwa mguu huo umekuwa unamsababishia maumivu makali yanayoambatana na homa kali, Naye Baba wa BI, SELATIAN, BW,MUMBI NATA amebainisha kuwa mtoto wake alizaliwa mzima na hakuwa na kasoro yoyote mpaka alipofikisha miaka 16 ndipo alipopatwa na matatizo hayo, mpaka sasa wameshafanya juhudi mbalimbali kumsaidia. BW.NATA amewaomba wasamaria wema kujitokeza kums

SILAHA YAKAMATWA PWANI.

Image
Add ca Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Ulrich Matei akionyesha silahaaina ya Bastora Browning iliyokamatwa Wilaya ya Mkuranga mkoani humo baada ya Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi kumpora mfanyabiashara aitwaye   Musa Kambangwa   mkazi Kijiji cha Mwaanambaya iliyokuwa na risasi 23 na magazine mbili pamoja na chaja ya kutunzia risasi ambapo pia katika tukio hilo ilikamatwa sare ya Jeshi la Wananchi Tanzania( JWTZ) Jozi moja,simu tatu za mnoni ,deki moja ya Dvd na Inveta moja PICHA KWA HISANI YA JESHI LA POLISI

WLAC YAWAPATIA WASAIDIZI WA KISHERIA MAFUNZO

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/ Kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake-WLAC-   kimetoa mafunzo kwa wasaidiz wa kisheria wilayani Kibaha ili kuweza kuwajengea uwezo na kuwawezesha kusaidia jamii katika maeneo yao wanaokabiliwa na migogoro mbalimbali. Afisa mradi msaidizi wilaya ya Kibaha, kutoka WLAC ambao wanasaidiwa kwa ufadhili wa LEGAL SERVICES FACILITIES, BI.SABRINA MTEGA amebainisha kuwa mradi huo umelenga kutoa mafunzo ya siku 25   kwa wasaaidizi wa kisheria wilayani Kibaha. BI.MTEGA ameongeza kuwa anatarajia mara baada ya kukamilika kwa awamu ya tatu nay a mafunzo hayo, wasaidizi wa kisheria watakuwa wamefundishwa mbinu mbali mbali za kupambana na changamoto za kisheria ikiwa pamoja na kutoa rufaa klwa masuala ambyo yanahitaji utaalamu zaidi wa kisheria, BI,MTEGA amewataka wasaidizi wa kisheria wanaopatiwa mafunzo wafanye kazi kwa mshikamno na kuweka ubinafsi pembeni ili malengo ya mradi yaweze kufikiwa. Naye mwezeshaji kutoka WLAC,BW.ROBERT CHUWA

WANANCHI WAIGOMEA TANROADS

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/Sunday, June 01, 2014 Wakazi wa Kata ya Pangani na Kata ya Maili moja halmashauri ya mji wa Kibaha wamewazuia wakala wa barabara Tanzania TANROADS kuweka mawe katika maeneo yao kabla hawajalipwa fidia stahili kutokana maeneo yao kummegwa kutokana na upanuzi wa barabara ya TAMCO-MAPINGA.   Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Diwani wa Kata ya MAILIMOJA BW.ANDREW LUGANO akiaambatana na mwenyekiti wa serikali ya machinjioni,amesema inashangaza kuona TANROADS wanaweka mawe kana kwamba wameshakamilisha taratibu za kulipa fidia.   BW.LUGANO amebainisha kuwa tahtimini katika eneo hilo imeshafanyika na kinachosubiriwa na kwa TANROADS kulipa fidia kwa wananchi hao, toka kwa sasa wanashindwa kuyaendeleza kuhofia kuvunjwa na TANROADS na hivyo kuwafanya kuishi katika hali ya wasiwasi na kushindwa kujua hatima yao.   BW.LUGANO ameshangazwa na hatua hiyo ya TANROADS kuanza kuweka mawe kabla ya kulipa fidia kwa wananchi, kitu ambach

WANANCHI WATAKA MATUTA RUVU DARAJANI

Image
  Ben Komba/Pwanio-Tanzania/05 thursday 2014   Wananchi wa Kata ya VIGWAZA kijiji cha Ruvu wilayani Bagamoyo wameitaka serikali kuweka matuta katika barabara ya kuu ya Morogoro katika eneo lao kufuatia mwendo kasi wa madereva ambao unaosababisha kugongwa kwa wananchi kila siku katika eneo hilo.   Mwandishi wa habari hizi akiongea na mmoja wa wananchi wa eneo hilo BW.SADALA CHACHA ambaye amesema kuwa katika kipindi cha wiki moja tu, takriban watatu wamegongwa na magari na kuwafanya wananchi kutishia kufunga barabara.   BW.SADALAH amebainisha kuwa hivi karibuni waligongwa watu watatu ambao ni wanafunzi, mwanamke na mwendesha Boda boda na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa wananchi wa eneo hilo.   Naye Mama mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina amebainisha kuwa wananchi wanaogopa hata kuvuka barabara kutokana na magari kupita kwa kasi eneo hilo na kushudia watu wakigongwa kila siku, ameongeza kuwa mbaya zaidi katika eneo la kuvukia kwenda shule ya Msingi Ru