WADAU WATAKIWEA KUJITOKEZA KUSAIDIA MICHEZO-VIDEO
Ben Komba/Pwani-Tanzania
Naibu Waziri TAMISEMI
BW.KASSIM MAJALIWA ametoa wito kwa mashirika na taasisi binafsi kushirikiana na
serikali katika kuboresha mashindano ya UMITASHUMTA, kwani huko ndiko
kunakotoka vipaji wanavyoviona leo hii.
Naibu Waziri MAJALIWA amesema
hayo wakati wa ufunguzi wa michezo ya 22 ya UMITASHUMTA inayofanyika katika
Mkoa wa Pwani, ambapo amewataka watu binafsina mashirika kushirikiana serikali
katika kuboresha michezo nchini.
Aidha amezitaka halmashauri
kuzuia uvamizi wa viwanja vya shule kunakofanywa na wananchi wenyewe, kutokana
na hapo nyuma serikali kusitisha shughuli za michezo na baadhi ya wtu kuchukua
fursa hiyo kupora vilivyokuwa viwanja vya michezo.
Awali akizungumza katika
ufunguzi huo, Mkurugenzi msaidizi elimu ya msingi nchini, BW.ABDUL MAULID
alimuomba Waziri kuchukua hatua kudhibiti uporaji wa viwanja vya michezo kwa
kuwahimiza wakurugenzi wa halmashauri kuvilinda viwanja vya michezo.
END
Comments
Post a Comment