VIWANJA VYA MICHEZO VILINDWE WAAGIZWA MA-DED

Ben Komba/Pwani-Tanzania
 
Naibu Waziri TAMISEMI BW.KASSIM MAJALIWA ametoa wito kwa mashirika na taasisi binafsi kushirikiana na serikali katika kuboresha mashindano ya UMITASHUMTA, kwani huko ndiko kunakotoka vipaji wanavyoviona leo hii.
 
Naibu Waziri MAJALIWA amesema hayo wakati wa ufunguzi wa michezo ya 22 ya UMITASHUMTA inayofanyika katika Mkoa wa Pwani, ambapo amewataka watu binafsi na mashirika kushirikiana serikali katika kuboresha michezo nchini.
 
Aidha amezitaka halmashauri kuzuia uvamizi wa viwanja vya shule kunakofanywa na wananchi wenyewe, kutokana na hapo nyuma serikali kusitisha shughuli za michezo na baadhi ya watu kuchukua fursa hiyo kupora vilivyokuwa viwanja vya michezo.
 
Awali akizungumza katika ufunguzi huo, Mkurugenzi msaidizi elimu ya msingi nchini, BW.ABDUL MAULID alimuomba Waziri kuchukua hatua kudhibiti uporaji wa viwanja vya michezo kwa kuwahimiza wakurugenzi wa halmashauri kuvilinda viwanja vya michezo.
 
END
--

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA