AOMBA MSAADA AKATIBIWE
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/18-6-2014
Mkazi wa Kitongoji
cha Kisogo katika kata ya Vigwaza, Tarafa ya Msoga wilayani Bagamoyo, BI
SELATIAN NATA ameombva msaada kwa watu mbalimbali ili aweze kwenda kutibiwa
mguu ambao umevimba.
BI SELATIAN amesema
yeye alizaliwa mzima wa afya bilka kuwa na kasoro yoyote mpaka alipofika umri
wa miaka 16, ndipo alipotokwa na kipele kidogo ambacho kilikuwa kinamuasha na
alipokuwa anakuna mguu ulianza kuvimba.
BI,SELATIAN awali
alikuwa ameolewa lakini hali ilipozidi kuwa mbaya ilibidi arudishwe nyumbani
kwao ambapo anaishi mpaka sasa akiwa na mtoto mdogo wa miezi nane,
ameongeza kuwa mguu
huo umekuwa unamsababishia maumivu makali yanayoambatana na homa kali,
Naye Baba wa BI,
SELATIAN, BW,MUMBI NATA amebainisha kuwa mtoto wake alizaliwa mzima na hakuwa
na kasoro yoyote mpaka alipofikisha miaka 16 ndipo alipopatwa na matatizo hayo,
mpaka sasa wameshafanya juhudi mbalimbali kumsaidia.
BW.NATA amewaomba
wasamaria wema kujitokeza kumsaidia binnti yake ili aweze kupata matibabu na
hasa ikizingatiwa umri mdogo wa mniaka 24 aliyonayo sasa.
END
Comments
Post a Comment