WANANCHI WATAKA MATUTA RUVU DARAJANI

 
Ben Komba/Pwanio-Tanzania/05 thursday 2014
 
Wananchi wa Kata ya VIGWAZA kijiji cha Ruvu wilayani Bagamoyo wameitaka serikali kuweka matuta katika barabara ya kuu ya Morogoro katika eneo lao kufuatia mwendo kasi wa madereva ambao unaosababisha kugongwa kwa wananchi kila siku katika eneo hilo.
 
Mwandishi wa habari hizi akiongea na mmoja wa wananchi wa eneo hilo BW.SADALA CHACHA ambaye amesema kuwa katika kipindi cha wiki moja tu, takriban watatu wamegongwa na magari na kuwafanya wananchi kutishia kufunga barabara.
 
BW.SADALAH amebainisha kuwa hivi karibuni waligongwa watu watatu ambao ni wanafunzi, mwanamke na mwendesha Boda boda na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa wananchi wa eneo hilo.
 
Naye Mama mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina amebainisha kuwa wananchi wanaogopa hata kuvuka barabara kutokana na magari kupita kwa kasi eneo hilo na kushudia watu wakigongwa kila siku, ameongeza kuwa mbaya zaidi katika eneo la kuvukia kwenda shule ya Msingi Ruvu darajani hakuna matuta,
 
amewataka askari wa usalama barabarani kuwabana madereva hususan wa mabasi makubwa kutokana na wo kuwa vinara wa kukikmbiza mabasi hayo na kuchagia vifo vya watanzania na kuwasababishia wengine ulemavu.
 
Naye Diwani wa Kata ya Vigwaza BW. MBEGU DILUNGA kwa upande wake nilipomtafuta kwa njia ya simu kutaka kujua yeye kama mwakilishi wa wananchi anachukuliaje kilio hicho cha wananchi, alionyesha kusita na alipoombwa kutumia akili ya kawaida kama mkazi wa hapo amesema kwa kifupi kuwa suala hilo limeshafikishwa kwa mkuu wa mkoa.
END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA