Posts

Showing posts from April, 2013

MWIZI MTANDAONI ATUPWA JELA MIAKA 10.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/04/25/2013/5:34:57 PM Mkazi wa mtaa wa Mwendapole, BW. CHARLES BEATUS maarufu kwa jina la Ngoge amehukumiwa kwenda jela miaka 10 kwa kosa la wizi katika mtandao pamoja na wizi wa kuaminiwa. Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa Kibaha BI.HERRIETH MWAILOLO mtuhumiwa ametiwa hatiani baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi uliotolewa na kufanya mtuhumiwa huyo kuingizwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela. Inadaiwa kuwa tarehe 05 May 2011, BW. GWELINO WILFRED mkazi wa Kongowe wilaya ya Kibaha aligundua kuibiwa kutoka akaunti yake kiasi cha shilingi milioni moja laki tatu na themanini-3,380000/= kutoka katika akaunti yake katika Tawi la NMB Mjini Kibaha yenye namba 2121606490 ambapo fedha zake zilihamishwa kupitia mtandao wa NMB-MOBILE kupitia namba yasimu 0767-122144 na kuhamishiwa kwenye akaunti yenye namba 2031614880 inayotumiwa na mtuhumiwa huyo. Kesi hiyo iliyokuwa inasimamiwa na wakili wa serikali BW. SALIM MSEMO mtuhumiwa BW. CHARLES B

WANANCHI WAGOMEA BARAZA LA MADIWANI KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/04/25/18:04:09 Katika hali inayoaashiria kukosekana kwa ushirikishwaji kwa wananchi kuhusiana na ratiba ya vikao vya Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha kumesababisha kukosa ushiriki wa wananchi kutokana na kutokuwepo na taarifa za mapema za vikoa hivyo na wakati mwingine baadhi ya watendaji kukalia taarifa ambazo zinapaswa kufikishwa kwa wananchi. Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia viti ambavyo vilipaswa kukaliwa na wananchi vikiwa wazi na ukumbi huo kujazwa na madiwani na wakuu wa idara pekee na hivyo kufanya kikao hicho kupoteza mvuto wake wa kawaida ambao ulikuwa na lengo la kupanua demokrasia katika ngazi ya serikali za mitaa. Kutokana na hali hiyo ilimbidi wa Chama Cha Mapinduzi halmashauri ya wilaya ya Kibaha BW. HAMIS KANESA kuchukua fursa hiyo kuwataka watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanaboresha utoaji taarifa kuhusiana na ufanyikaji wa vikao hivyo kama ratiba inavyoainisha. Mbali ya kujitokeza hali hiyo Madiw

POLICE PWANI WAKUTANA NA WANAHABARI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-Apr-13/07:02:32 PM Kamanda wa Jeshi la Polisi katika mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi ULRICH MATEI amesema suala la ajali ndio kitisho kikubwa ambacho Jeshi la Polisi linakabiliana katika mkoa huo, ingawa mpaka sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha ajali. Ameyazungumza katika kikao cha kila mwezi na waandishi wa habari wanaofanya kazi katika mkoa wa Pwani katika kujaribu kubadilishana uzoefu katika mambo mbalimbali na hasa kutokana na kada ya uandishi ndiyo imekuwa ikifanya kazi bega kwa bega na Jeshi hilo, kwa kuzitangaza taarifa zinazotolewa na Jeshi hilo na kuchukulia suala la ajali kama ni changamoto namba moja ya Jeshi hilo. Kamanda MATEI amebainisha kuwa kwa kutambua umuhimu wa tasnia ya habari nchini na namna inavyotoa m,chango mkubwa katika kuielimisha jamii na kuibua maswala mbalimbali yanayotokea katika nchi yetu na jeshi nla Polisi mkoa wa Pwani kwa kuliona hilo ikaona ipo haja ya kukaa na waandishi kama wadau muhimu ili

SERIKALI YA AWAMU YA NNE YAJIPIGIA DEBE NA KUSAHAU UDINI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18 April, 2013/19:41:28 Mkuu wa wilaya ya Kibaha,BI HALIMA KIHEMBA amesema kwa kipindi cha miaka 7 ya utawala wa awamu ya nne kuna mambo mengi mazuri ambayo yamefanywa na serikali katika sualazima la kuhakikisha inawaletea maendeleo wananchi ambao ndio wapiga kura kwa kuimarisha huduma mbalimbali za kijamii. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha, Mkuu wa wilaya BIBI.KIHEMBA akizungumzia suala zima la usimamiaji na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi ambacho ndio chama tawala, amegusia maeneo ambayo yameweza kufikiwa katika kipindi cha miaka saba ya awamu ya nne. BIBI. KIHEMBA akizungumzia mafanikio yaliyopatikana akianziana sekta ya kilimo kama mojha ya shughuli kuu ya kiuchumi katika wilaya amesema kuna mafanikio makubwa hususan katika Kata za Kwala, Magindu na Ruvu kwa kuweza kusimamia kikamilifu suala ufugaji wa kisasa wa kuku na ng'ombe wa maziwa na huku wakijishugfhulisha na kilimo cha Korosho,ufuta,

KIONGOZI WA CCM AKANUSHAKUJIHUSISHA NA USHOGA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/04/15/13/19:32:10 Katibu wa uchumi, malezi na mazingira wa chama cha mapinduzi Kata ya Mailimoja BW. LAZARO KULIGWA amekanusha kuhusika kwake na ufanyaji wa mapenzi ya jinsia moja kama inavyosambazwa na mahasimu wake wa kisiasa ndani ya chama hicho kwa lengfo la kumharibia mafanikio ambayo ameyapata katika medani ya siasa. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisi ya CCM wilaya ya KIBAHA, BW. KULIGWA amesema kuwa yeye binafsi kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akisikia watu wakimsema chinichini na alikuwa anangoja mwenye kujitokeza amuulize kuhusiana na hilo lakini hakutokea mpaka alipokutana na mwandishi wa hizi. BW.KULIGWA amebainisha kuwa kwa mara ya kwanza ilikuwa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu uliopita ambapo mmojka wa wagombea alikusanya vijana na kujenga maneno hayo kwa lengo la kumharibia kisiasa ingawa mpaka sasa anasubiri mtuwa kujitokeza kuthibitisha madai hayo ambayo yana lengo la kumchafua. Akizungumzia kuibuka kwa maneno hayo ya kumhu

CHADEMA KUPASUKA KIBAHA M4C

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Apr-13/17:50:33 Chama cha demokrasia na maendeleo katika mkoa wa Pwani wamelalamikia Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku mpaka kufikia hatua ya Polisi kuwaandikia hotuba na kulazimisha kutumika katika mikutano yao kama ilivyojidhihirisha katika mikutano yao waliyofanya wilayani Rufiji, Kisarawe na Bagamoyo. Akiongea na waandishi wahabari katika kikao cha maalum chenye lengo la uzinduzi wa kikanda wa M4C, Yaani vuguvugu la mabadiliko ambalo linahusisha mikoa ya kichama ya Ilala, Temeke na Kinondoni am,bao utafanyika katika wilaya ya Kibaha tarehe 14 April. Mwenyekitiwa chama hicho katika mkoa wa Pwani, BW. SAID UKWEZI amesema wamekuwas wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kutoka kwa Jeshi la Polisi ikiwa pamoja na viongozi wao kubambikiwa kesi ambazo hawakuhusika nazo kwa lengo lakuwapaka matope viongozi wa chama hicho. Bw. UKWEZI amebainisha kuwa ilifikia hatua Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Bagamoyo alitekwa wakiwa

MOTO WATEKETEZA MADUKA KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Apr-13/17:09:19 Moto mkubwa umezuka katika eneo la mtaa wa Soga katika halmashauri ya mji na kutekeza duka la vifaa vya baiskeli na pikipiki, duka la vifaa vya kielektroniki na sehemu ya kukatia nywele na kusababisha hasara ya fedha na mali ya fedha na mali. Wananchi kwa kushirikiana gari la kuzima moto la halmashauri ya mji wa Kibaha walifanya kazi bega kwa bega kuhakikisha moto huo hauleti madhara zaidi kwa nyumba zilizopo jirani ya eneo la tukio ambalo lilisababisha mmiliki wa duka la vifaa vya baiskeli na pikipiki aliyejulikana kwa jina la DEO kutokomea kusikojulikana. Lakini taarifa nyingine zinasema baadhi ya watu baadaya kumuona alivyokuwa amechanganyikiwa waliamua kumtuliza na kumpeleka kwa kaka yake kwa ajili ya kuliwazwa kufuatia janga hilo ambalo limemwacha akiwa hana nyuma wala mbele kibiashara ingawa bado kuna matumaini kimaisha. Naye shuhuda wa tukio hilo Bw. IBRAHIM CHAKA amesema wao walianza kuona moshi ukifuka katika duka la vif

MEYA WA BAGAMOYO, ABDUL SHARRIF AKEMEA UZEMBE WA WATUMISHI

Tuesday, 9 April, 2013, 14:03 Tuesday, 9 April, 2013, 14:03 Ben Komba/Pwani-Tanzania/Tuesday, 9 April, 2013, 14:03 viongozi nchini wametakiwa kutimiza majukumu kwa kadiri ya wajibu na miongozo iliyopo katika suala zima la kuwatumikia wananchi.Hayo yamezungumzwa na meya wa mji wa Bagamoyo, Bw. Abdul Sharrif amezungumza hayo katika kikao na waandishi wa habari hivi karibuni mjini Kibaha,na amesema tatizo lililopo ni kwamba kila mtu anapopata uongozi wanafikiria maslahi binafsi.Bw. Sharrif amesema kuwa ccm ina lengo la kweli la kumkomboa mwananchi wa kawaida kwa kuangalia hata ilani yake kwani inatekelezeka na hata viongozi wake ni makini na kinachotokea ni changamoto za kisiasa na nyingine ni matatizo ya baadhi ya wachache. Amebainisha baadhi ya viongozi wake hawakitendei haki ccm,kwa kusahau majukumu ya kuwaletea maendeleo wananchi, amesisitiza chini ya uongozi wa DR. KIKWETE nmambo mengi yamefanywa kwa chama na serikali. BW. SHARRIF amesema wananchotaka wananchi sio kununuliw

MENGI YAIBUKA ZOEZI LAKUTAFUTA WAJUMBE WA BARAZA LA KATIBA KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/03 April, 2013/17:10:47 Udhaifu mkubwa na mashaka umejitokeza katika zoezi zima la kutafuta wajumbe wa baraza la katiba katika wilaya ya Kibaha hasa baada ya kampeni hizo kuytawaliwa na udini, ukabila, siasa na makundi yanayowindana kuelekea uchaguzi wa 2015 kutoka chama cha mapinduzi. Moja wa washriki wa mchakato huo katika Kata ya Kwa Mfipa BW. DAVID MRAMBA amesema kwa sasa hali si mzeni kabisa kwani kuna chuki za waziwazi kunakosababishwa na kufumbiwa macho vitendo ambavyo vinaweza kuzuilika kabisa kwa akili za kawaida kabisa kisa cha kumkashifu mwenzio ni kosa basi watu washitakiwe kwa vifungu kama hivyo. BW. MRAMBA ameongeza Kwa kuachiliwa kwa vitrendo kama hivyo kumesababisha kuongezeka kwa mpasuko mkubwa kwa wananchi kuelekea mwaka 2015, na kama hazitachukuliwa mapema hali inawezxa kuwa mbaya zaidi na toka vitendo hivi vipo ndani ya uwezo wa Rais wa kuvizuia kwa kutumia sheria zilizopo. Mbali ya kujitokeza mpasuko unaosababishwa na masuala ya d

JUMUIYA YA KIISLAMU YACHANGIA DAMU.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/02-Apr-13/19:00:09 Shura ya waislamu mjini Kibaha kitengo cha ustawi wa jamii wamechangia damu kupitia mpango wa damu salama katika kuhakikisha kunakuwepo na damu wakati wote katika kuunga mkono juhudi za serikali kuimarisha huduma za kijamiii katika zoezi hilo jumla ya uniti 32 za damu zilipatikana na hivyo kuweza kwenda kuwasaidia wahitaji. Amiri mkuu wa shura ya Kiislamu ya mjini Kibaha, BW. SALUM MKUMBA amesema jambo ambalo wamelifanya ni sehemu ya majukumu ya kitengo cha ustawi wa jamii na wanalichukulia suala la kutoa damu kama sunnah na kulichukulia kama ni jambo la kiimani. BW. MKUMBA amesema wamefanya hivyo kuzingatia ajali zinazotokea mara kwa mara katika Barabara kuu ya kwenda bara na hivyo kufanya mahitaji ya damu kuwa makubwa na hasa ikizingatiwa kuwa ajali hazipo kwa watu maalum tu bali mtu yoyote anaweza kupata ajali. Amewaasa watu binafsi kujitokeza kutoa damu ili kuweza kusaidia wagonjwa wanaohitaji damu, na mpango huo wamwepanga k