MENGI YAIBUKA ZOEZI LAKUTAFUTA WAJUMBE WA BARAZA LA KATIBA KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/03 April, 2013/17:10:47 Udhaifu mkubwa na mashaka umejitokeza katika zoezi zima la kutafuta wajumbe wa baraza la katiba katika wilaya ya Kibaha hasa baada ya kampeni hizo kuytawaliwa na udini, ukabila, siasa na makundi yanayowindana kuelekea uchaguzi wa 2015 kutoka chama cha mapinduzi. Moja wa washriki wa mchakato huo katika Kata ya Kwa Mfipa BW. DAVID MRAMBA amesema kwa sasa hali si mzeni kabisa kwani kuna chuki za waziwazi kunakosababishwa na kufumbiwa macho vitendo ambavyo vinaweza kuzuilika kabisa kwa akili za kawaida kabisa kisa cha kumkashifu mwenzio ni kosa basi watu washitakiwe kwa vifungu kama hivyo. BW. MRAMBA ameongeza Kwa kuachiliwa kwa vitrendo kama hivyo kumesababisha kuongezeka kwa mpasuko mkubwa kwa wananchi kuelekea mwaka 2015, na kama hazitachukuliwa mapema hali inawezxa kuwa mbaya zaidi na toka vitendo hivi vipo ndani ya uwezo wa Rais wa kuvizuia kwa kutumia sheria zilizopo. Mbali ya kujitokeza mpasuko unaosababishwa na masuala ya dini, ukabila nao haukuwa nyuma katika mchakato huo ambapo ilifikia hatua watu wakaanza kuchaguana kwa kutumia wewe kabila gani na huku siasa haikuwa nyuma kwa chama cha Demokrasia na maendeleo kupatra nafasi kadhaa katika baraza hilo la katiba. Napo katika mtaa wa Mkoani Block B ambapo napo kunasifika kwa kampeni zenye kufuata misingi ya kidini hali ya uchaguzi ilikuwa shaghala baghala baada ya wasimamizi wa uchaguzi huo kutokuwa makini katika suala zima la ugawaji wa karatasi za kupigia kura nba ukusanyaji wa kura kulikosababishwa na uzembe wa makusudi na kusababishauchaguzi huo kurudiwa mara nne, hali iliyosababisha baadhi ya wapiga kura kushindwa kutumia haki yao ya msingi. Pamoja na kuwepo kwa uzembe kwa upande wa wasimamizi wa zoezi la kuchagua wajumbe wa baraza la katiba, vijana wa eneo hilo nao walikutwa na mwandishi wa habari hizi wakijisifu jinsi gani walivyotumia uzembe wa wasimamizi kupiga kura mara tatu tatu, na wakati mwingine mtu kubaki na kura yake mkononi bila kukusanywa hali ambayo inasemekana ilifanywa kwa makusudi katika baadhi ya watu wenye hila mbaya kuchezea zoezi hilo. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA