JUMUIYA YA KIISLAMU YACHANGIA DAMU.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/02-Apr-13/19:00:09
Shura ya waislamu mjini Kibaha kitengo cha ustawi wa jamii wamechangia damu kupitia mpango wa damu salama katika kuhakikisha kunakuwepo na damu wakati wote katika kuunga mkono juhudi za serikali kuimarisha huduma za kijamiii katika zoezi hilo jumla ya uniti 32 za damu zilipatikana na hivyo kuweza kwenda kuwasaidia wahitaji.
Amiri mkuu wa shura ya Kiislamu ya mjini Kibaha, BW. SALUM MKUMBA amesema jambo ambalo wamelifanya ni sehemu ya majukumu ya kitengo cha ustawi wa jamii na wanalichukulia suala la kutoa damu kama sunnah na kulichukulia kama ni jambo la kiimani.
BW. MKUMBA amesema wamefanya hivyo kuzingatia ajali zinazotokea mara kwa mara katika Barabara kuu ya kwenda bara na hivyo kufanya mahitaji ya damu kuwa makubwa na hasa ikizingatiwa kuwa ajali hazipo kwa watu maalum tu bali mtu yoyote anaweza kupata ajali.
Amewaasa watu binafsi kujitokeza kutoa damu ili kuweza kusaidia wagonjwa wanaohitaji damu, na mpango huo wamwepanga kuwa endelevu kutokana na kitengo chao kucheza karibu na mambo ya hospitali na wagonjwa na wanatarajia kuaandaa mkutano mkubwa wa vitengo vya huduma za jamii na watataka kutumia fursa hiyo kuchangia damu ambapo wajumbe 18 wanatarajia kuhudhuria mkutano huo.
Aidha nimebahatika kuongea na mmoja wa wachangiaji hao kutoka shura ya waislamu mjini Kibaha, BI. HALIMA ATHUMANI SAGARE amesema kuwa wameshawishika kufika hospitalini hapo kutokana na yeye kuwa katika kitengo kinachotoa huduma kwa jamii na hivyo kupata nafasi ya kujua matatizo makubwa yaa damu yanayozikabili hospitali zetu, hivyo amewataka watanzania wawe na moyo wa kuchangia damu ili kunusuru maisha ya binadamu wenzetu au wenyewe.
END.
Comments
Post a Comment