SERIKALI YA AWAMU YA NNE YAJIPIGIA DEBE NA KUSAHAU UDINI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/18 April, 2013/19:41:28
Mkuu wa wilaya ya Kibaha,BI HALIMA KIHEMBA amesema kwa kipindi cha miaka 7 ya utawala wa awamu ya nne kuna mambo mengi mazuri ambayo yamefanywa na serikali katika sualazima la kuhakikisha inawaletea maendeleo wananchi ambao ndio wapiga kura kwa kuimarisha huduma mbalimbali za kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha, Mkuu wa wilaya BIBI.KIHEMBA akizungumzia suala zima la usimamiaji na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi ambacho ndio chama tawala, amegusia maeneo ambayo yameweza kufikiwa katika kipindi cha miaka saba ya awamu ya nne.
BIBI. KIHEMBA akizungumzia mafanikio yaliyopatikana akianziana sekta ya kilimo kama mojha ya shughuli kuu ya kiuchumi katika wilaya amesema kuna mafanikio makubwa hususan katika Kata za Kwala, Magindu na Ruvu kwa kuweza kusimamia kikamilifu suala ufugaji wa kisasa wa kuku na ng'ombe wa maziwa na huku wakijishugfhulisha na kilimo cha Korosho,ufuta, mbogamboga na mazao mengine kama mihogo na viazi vitamu.
BIBI.KIHEMBA amebainisha kilimo ni shughuli kuu ya kiuchumi katika wilaya ambapo zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wanategemea shughuli za kilimo na ufugaji,na kuhusu uzalishajiwa mazo ya chakula umeongezeka kutoka tani 32,502 kwa mwaka 2005 hadi tani 55,404 kwa mwaka jana sawa na asilimia70.4.
Ingawa katika kila mafanikio kuna changamoto zake, Mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI.HALIMA KIHEMBA amefafdanua changamoto kubwa inayokabili sekta yakilimo ni uchelewashaji wa fedha za ujenzi wa miradi na kusababisha ujenzi kuchelewa na gharama za mradi kuongezeka, ikichangiwa na mwamko mdogo wa wakulima kuhusu matumizi ya zana bora za kilimo na pembejeo,ikiwa na wakulima kutohudhuria shamba darasa wanapokuja wataalamu wa kilimo katika maeneo yao.
END.
Comments
Post a Comment