CHADEMA KUPASUKA KIBAHA M4C

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Apr-13/17:50:33 Chama cha demokrasia na maendeleo katika mkoa wa Pwani wamelalamikia Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku mpaka kufikia hatua ya Polisi kuwaandikia hotuba na kulazimisha kutumika katika mikutano yao kama ilivyojidhihirisha katika mikutano yao waliyofanya wilayani Rufiji, Kisarawe na Bagamoyo. Akiongea na waandishi wahabari katika kikao cha maalum chenye lengo la uzinduzi wa kikanda wa M4C, Yaani vuguvugu la mabadiliko ambalo linahusisha mikoa ya kichama ya Ilala, Temeke na Kinondoni am,bao utafanyika katika wilaya ya Kibaha tarehe 14 April. Mwenyekitiwa chama hicho katika mkoa wa Pwani, BW. SAID UKWEZI amesema wamekuwas wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kutoka kwa Jeshi la Polisi ikiwa pamoja na viongozi wao kubambikiwa kesi ambazo hawakuhusika nazo kwa lengo lakuwapaka matope viongozi wa chama hicho. Bw. UKWEZI amebainisha kuwa ilifikia hatua Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Bagamoyo alitekwa wakiwa katika mchakato wa uchaguzi wa marudio ambapo baada ya kutekwa kwa mwenyekiti wao walifanikiwa kubaini majina ya watu waliomteka, namba ya gari na kuzikabidhi kwa JeshinlaPolisi lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa. Katika siku hizi za karibuni chama hicho viongozi wake wamekuwa wakikamatwa kwa makosa mbalimbali ambayo wenyewe wanadai hawakujihusisha nao kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi akitoa m,fano kesi inayomkabili mkurugenzi wa usalama wa Chama chka BW. WILFRED RWAKATARE ambaye mpaka anashikiliwa na Jeshi hilo katika harakati za serikali ya CCM kukibomoa chama hicho kabla ya uchaguzi wa 2015. Kuhusiana na mkutano wa uzinduzi ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa cham hicho ngazi ya Taifa, BW.FREEMAN MBOWE na katibu mkuuDR. WILBROAD SLAA na viongozi wengine wa kitaifa na wabunge mbalimbali wa cham hicho ambapo kutatanguliwa na mapokezi ya viongozi kutoka makao makuu ya chama mpakani mwa mkoa wa Pwani na Kanda maalum ya Dar es saalam. END. .

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA