POLICE PWANI WAKUTANA NA WANAHABARI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-Apr-13/07:02:32 PM Kamanda wa Jeshi la Polisi katika mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi ULRICH MATEI amesema suala la ajali ndio kitisho kikubwa ambacho Jeshi la Polisi linakabiliana katika mkoa huo, ingawa mpaka sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha ajali. Ameyazungumza katika kikao cha kila mwezi na waandishi wa habari wanaofanya kazi katika mkoa wa Pwani katika kujaribu kubadilishana uzoefu katika mambo mbalimbali na hasa kutokana na kada ya uandishi ndiyo imekuwa ikifanya kazi bega kwa bega na Jeshi hilo, kwa kuzitangaza taarifa zinazotolewa na Jeshi hilo na kuchukulia suala la ajali kama ni changamoto namba moja ya Jeshi hilo. Kamanda MATEI amebainisha kuwa kwa kutambua umuhimu wa tasnia ya habari nchini na namna inavyotoa m,chango mkubwa katika kuielimisha jamii na kuibua maswala mbalimbali yanayotokea katika nchi yetu na jeshi nla Polisi mkoa wa Pwani kwa kuliona hilo ikaona ipo haja ya kukaa na waandishi kama wadau muhimu ili kuweza kufahamiana na kuelekezana masuala mbalimbali ya utendaji kazi. Katika taarifa yake kwa waandishi Kamanda MATEI amezungumzia katika kipindi cha Robo ya kwanza ya mwaka 2013 mkoa wa Pweani umekabiliwa na matukio kadhaa ya uvunjifu wa amani ikiwemo kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwadhuru watuhumiwa wanaowakamata badala ya kuwafikisha kituo cha Polisi ili sheria ichukuwe mkondo wake. Mmoja wa waandishi wakongwe Mkoa wa Pwani, BW. AYOUB MTAWAZO alichukua nafasi kumkunmbuka aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya ndani katika kipindi cha awamu ya pili, BW.AUGUSTINE LYATONGA MREMA kwa kuanzisha mpango wa ujenzi wa Polisi Post katika maeneo mbalimbali katiika suala zima la kukabiliana na uhalifu nchini. Aidha BW. MTAWAZO ameshauri kuanzishwa tena kwa ulinzi wa sungusungu katika mitaa yetu katika kuhakikisha huduma ya kuiomarisha ulinzi na usalama inafika ngazi ya jamii kikamilifu sawa mpango wa Poklisi jamii/Polisi shirikishi. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA