Posts

Showing posts from March, 2013

WABUNGE WAHITIMU MAFUNZO 832 KJ.

WABUNGE WAHITIMU MAFUNZO 832 KJ. Ben Komba/Pwani-Tanzania/29-Mar-13/09:46:30 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, DKT. JAKAYA KIKWETE amekumbuka ujasiri ambao aliupata kutokana na yeye kupitia Jeshi la kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria,akiwa katika kombania C ambapo alikutana na watu mbalimbali na kupata uzoefu mkubwa wa kimaisha. DKT. KIKWETE amebainisha kutokna na kupitia kwa mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria na kubahatika kupangiwa katika kikosi cha 832 cha Jeshi la kujenga Taifa Ruvu, na amewapongeza wabunge ambao wamehitimu mafunzo yao ya wiki tatu kwa kuonyesha uzalendo. Katika ziara hiyo Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu, DKT. JAKAYA KIKWETE ametembelea maeneo mbalimbali ya miradi ya kikosi na kuona nyumba namabweni ya vijana wa JKT na kufunga mafunzo maalum ya JKT kwa wabunge ambao wamehudhuria mafunzo hayo ambayo yalianza March 4. Wabunge ambao wamehudhuria mafunzo hayo ni, BW.DAVID SILINDE, BW. MURTAZA MANGU

MGOGOROWA ARDHI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-Mar-13/08:51:18 AM Wakazi na wakulima wa vitongoji vya Kisabi na Kiwalani katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha wameazimia kuifikisha halmashauri hiyo mahakamani kuhusiana na hatua ya idara ya ardhi kupima maeneo yao na kuweka mawe kuonyesha kuwa viwanja hivyo vimepimwa bila kuwashirikisha. Nikiongea na Katibu wa Jumuiya ya wakulima na wakazi wanaokaa katika vitongoji hivyo BW. ABILAHI SAAD amebainisha kuwa wao kwa pamoja wamekutana na kuazimia kulifikisha suala hili mahakamani kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi wa kisheria. BW. SAAD amefafanua kuwa kuna fununu kwamba eneo hilo linataka kutolewa kwa wafanyabiashara ambao wanqapata nguvu kutoka halmashauri kana kwamba wao ni weageni katika nchi na huku kuweepo kwa mji wa Mlandizi ni kuwepo kwa watu wanaoishi eneo hilo, hivyo amelaani tabia ya watendaji wanaotokla maeneo mengine kupuuza haki za wazawa wa maeneo wanayofanyia kazi. Amewataka watendaji kabla ya kufanya maamuzi makubwa kama ya kumnyang'a

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/20-Mar-13/15:33:23 Wananchi mjini Kibaha wametakiwa kushukluru kwa yale mambo ambayo wanayaona madogo yanayofanywa na serikali katika kuimarisha miundombinu ya maji katika suala zima la kuboresha maisha ya jamii badala ya kubeza kila mafanikio yanayofanywa na serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania. Akizungumza katika maadhimisho ya ya maji Kibaha mjini, Mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI.HALIMA KIHEMBA amesema taarifa alizosomewa zinaonyesha mafanikio na unapopata kidogo inabidi kushukuru kwa hilo maana mtu asiye na shukurani hata akipewa kikubwa hawezi kushukuru. BIBI.KIHEMBA amebainisha ipo tabia ya watanzania wengi kulaumu serikali katika kila jambo, Ilihali serikali imefanya makubwa kwani kuanzia mchakato wa kutafuta mkandarasi mradi unatekelezwa lakini wanamtaa wa Visiga, Jonugha na Saeni wao hawalioni hilo na amewataka wakazi wa mitaa hiyo kuwa na shukrani na subira kwa kuona serikali inajali na inafanya kazi hailali. Naye msoma risala, BW. BEATUS

ABC BANK WATOA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/14-Mar-13/19:42:09 Benki ya ABC imetoa mikopo ya pikipiki kwa kwa wajasiriamali kupitia mpango wake kuwezesha sekta isiyo rasmi kimtaji ili ziweze kujenga uchumi imara katika ngazi ya mtu mmoja mmoja katika suala zima la kupunguza pengo la watru wasi na shughuli maalum za kufanya. Mwenyekiti wa taifa wa muungano wa sekta isiyo rasmi, BW. DAUDA SALMINI kwa kushirikiana na AFRICA BANKING CORPORATION-ABC-, ambapo amebainisha kuwa hiyo ni mwanzo tu wa kuhakikisha sekta isiyo rasmi inaangaliwa kwa jicho tofauti katika suala zima la kuhakikisha kila mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi anawezeshwa ili kuweza kubuni mbinu mwafaka za kujipatia kipato na kuweza kulipa kodi stahili za serikali. BW. SALMIN amebainisha kuwa mkopo huo katika hatua ya mwanzo kabisa umetolewa katika halmashauri ya mji wa Kibaha katika mtaa wa Picha ya ndege ambapo wajasiriamali sita waliokidhi vigezo wameweza kukabidhiwa pikipiki ikiwa sehemu ya uwezeshaji wa sekta isiyo rasmi, ambap

MKAZI AWA KERO KWA WENZAKE.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/16 March, 2013/11:18:45 Wakazi wa eneo la Kibamba Mdimua katika manispaa ya Kinondoni wameilalamikia manispaa hiyo kwa kutomshinikiza mkazi mwenzao anayemiliki eneo kubwa la heka takriban 10 bila kulifanyia usafi na kusababisha kuzaliana kwa wanyama wakali na baridi. Mmoja wa wakazi ambao nimeongea nao, BW. ADAM SALUM amesema mmiliki wa shamba pori hilo amesema amekuwa akisababisha kero kwa wananchi kutokana kutolihudumia eneo hilo ambalo kisheria linahesabika liko mjini na mjini hakuna shamba inakuwaje manispaa ya Kinondoni haichukui hatua stahili. BW. SALUM amesisitiza kuwa mbali ya kutolihudumia eneo hilo, mmiliki huyo amekuwa akipanda mianzi katika kubadilish mwelekeo wa mto na hivyo kuwasababishia madhara wakazi wanaokaa ng'ambo nyingine ya mto, kwa kingo za upande huo kuliwa haraka na maji yanapokuwa yamejaa mtoni. Naye Bi mkubwa ASHA SALEH KIDEKWA amesema yeye akiwa ni watu wa mwanzo kuhamia meneo hayo mwanzoni mwa miaka ya themanini,, amee

BARABARA ZACHONGWA MJINI KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Mar-13/20:04:51 Halmashauri ya mji wa Kibaha imeendelea na mpango wake wa kuhakikisha barabara katika halmashauri ya mji wa Kibaha zinachoingwa na kuziweka katika hali nzuri ya kupitika katika kipindi cha chote cha mwaka, hali hiyo imekuja kufuatia halmashauri hiyo kuwa na Greda ambalo kwa njia moja au nyingine linarahisisha baadhi ya shughuli za ujenzi katika katika halmashauri. Mhandisi wa ujenzi halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. EZEKIEL KUNYARANYARA amesema lengo ni kuchonga barabara zote ambazo zipo kisheria katika kuhakikisha usumbufu unapungua kwa watumiaji na kusaidia katika kuweza kupanga mji katika mpangilio unaoeleweka kwa kuimarisha miundo mbinu ya barabara. Mhandisi KUNYARANYARA amesema barabara zote hizo kwa kuanzi zitakuwa katika kiwango cha udongo, wakati halmashauri ikijiandaa na mikakati mingine ya baadaye ikizingatia upatikanaji wa fedha ambazo itasaidia kuimarisha miundombinu ya barabara katika mji wa Kibaha kama alivyokutwa na kame

POLISI JAMII NA ELIMU MAALUM

Ben Komba/Pwani-Tanzania/11-Mar-13/20:05:34 Jeshi la Polisi nchini linafanya utafiti maalu yenye lengo la kujua mafanikio yaliyopatikana katika sera yake ya Polisi Jamii ambayo imelenga kuishirikisha jamii kikamilifu katika suala zima la ulinzi na usalama wa watu na mali zao. Katika utafiti huo ambao ulihusisha makundi ya watu tofauti katika jamii kwa kuwapatia madodoso yenye maswali ambayo washiriki walitakiwa kujaza kwa kadiri ya maono yao kuhusiana na utendaji wa Jeshi la Polisi katika suala zima la Polisi jamii katika kuhakikisha kunakuwepo na kuaminiana kati ya wanajamii na Polisi. Nikiongea na Mratibu msaidizi wautafiti huo katika mkoa wa Pwani, INSPEKTA ATHUMAN MTASHA amesema utafiti huo katika Mkoa wa Pwani utahusisha wilaya za Kibaha na Mkuranga na makundi mbali yameshafikiwa yakiwemo waandishi wa habari, walimu, watendaji na wafanyakazi wa kada mbalimbali. Naye mmoja wa watafiti wasaidizi amesema wao wanatekeleza agizo kutoka Jeshi la Polisi Tanzania na wao wametoka

WANAWAKE VIJANA HURU NA MAENDELEO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Mar-13/18:48:18 Mpango wa wanawake vijana uhuru na maendeleo unaoendeshwa kwa pamoja kati ya ACTION AID na shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE -YPC- lenye maskani yake mjini Kibaha limefanikiwa kuwafikia walengwa takriban 400 katika suala zima la kuwapatia wanawake hao vijana elimu juu ya kujitambua na ujasiriamali. Mratibu wa mpango kutoka YPC, BIBI. GROLIA MABERE amesema mpango huo unanuia kuwafikia wanawake vijana 2000 nchi nzima, kwa wilaya ya Kibaha mradi huo umegusa katika halmashauri zote mbili ya mjini na kijijini, kwa kuwakusanya wanawake kutoka katika kata mbalimbali na kuwasaidia kuunda vikundi na kufanya uchaguzi wa viongozi wao. BIBI. MABERE amebainisha kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kuwaamsha wanawake vijana na kujitambua na kuweza kushiriki katika mambo mbalimbali ya kitaifa na mtaa ikiwa pamoja na kushiriki chaguzi mbalimbali zinazojitokeza katika maeneo yao. Mratibu huyo wa mpango wa wanawake vijana kutoka YPC

SIKU YA WANAWAKE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Mar-13/10:29:44 Mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI. MWANTUM MAHIZA amewakumbusha wanawake kuhusiana na wajibu walio nao kama walezi kuutekeleza kikamilifu katika kuliletea Taifa ustawi wa kimaadili kwa familia zao na kuimarisha Amani ya taifa. BIBI. MAHIZA amesema wanawake watambue kuwa wao ni walezi wa watoto wao na watoto wa wanawake wenzao na vilevile wanawajibu wa kulea watu walio karibu nao na amewataka kutosita katika kushauri kwa ajili ya mustakabali mzuri wa taifa ambao utalenga katika kuimarisha amani ya familia na kuchochea maendeleo ya kijamii. BIBI. MAHIZA amewataka wanawake kukumbuka msemo unaosema NYUMA YA MWANAUME MWENYE MAFANIKIO KUNA MWANAMKE MWEREVU ambaye kwa njia moja au nyingine anamuwezesha mwanamume wake katika mambo mbalimbali ambayo yanasaidia kumjenga kiakili na kiafya na kumuwezesha mume kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Akizungumza katika Hafla aliyoiaandaa kwa ajili ya siku ya wanawake Duniani, Mke wa Mbunge wa Kibaha, BIBI. SE

BAJETI KIBAHA DC

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/03/06/19:34:02 Halmashauri ya wilaya ya Kibaha katika mpango wake wa maendeleo wa mwaka 2013/2014 imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 15,280,299,670/= ikiwa mbali na michango ya wananchi na hili ikiwa ni ongezeko la asuilimia 7.2 ukilinganisha na bajeti mwaka 2012/2013. Akisoma hotuba katika mkutano maalum wa Baraza la madiwani, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa MANSOUR KISEBENGO amesema kuhusiana na miradi ya maendeleo itatekelezwa kila sekta kwa kadiri ya mahitaji yao. MHESHIMIWA KISABENGO amebainisha miradi ya maendeleo itatekelezwa katika sekta ya elimu kwa kukarabati nyumba za walimu, ujenzi wa vyoo na ukarabati wa vyumba vya madarasa, ikiwa pamoja na kununua vifaa vya maabara za kemia na bailogia. Kwa upande wa sekta ya afya Halmashauri ya wilaya ya Kibaha katika mwaka wa fedha 2012/2013 imenuia kukamilisha ujenzi wa nyumba ya kuhifadhia maiti katika kituo cha afya Mlandizi, ujenzi wa nyumba za madaktari, upanuzi

MBUNGE WA KIBAHA MJINI AJADILI MAJI NA WAPIGA KURA WAKE.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-Mar-13/09:07:37 Kero ya maji imeendelea kuwa gumzo kwa wakazi wa mji wa Kibaha kufuatia kuvurugika kwa ratiba ya awali ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali kwa kile kinachodhaniwa ni mbinu ya makusudi inayofanywa na baadhi ya watumishi wenye magari ya kuuza maji kupata faida kwa kuyauza maji hayo kwa bei ya juu. Mmoja wa wakazi wa Maili moja BW. ALLY GONZA ameyasema hayo wakati akitoa malalamiko yake juu tatizo la upatikanaji wa maji kwa mbunge wa Jimbo uchaguzi la Kibaha mjini, MHESHIMIWA SYLVESTER KOKA wakati alipokuta na wafanyabiashara ili kuweza kuongea nao kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. BW. GONZA amebainisha suala la kutopatikana maji katika muda wa ratiba kuna wasababishia usumbufu mkubwa wananchi wa mji wa Kibaha na wamelaumu hatua ya DAWASCO kuwahamisha wateja wa Kibaha kutoka bomba la kubwa na kuwaunganisha katika bomba ambalo halina uwezo wa kutoa huduma hiyo barabara kwa wakazi mji wa Kibaha. Akijibu

WANANCHI KIDIMU WAPINGA HATUA YA MKURUGENZI WA MJI KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-Mar-13/16:18:21 Wakazi wa Kata ya Pangani Kitongoji cha Kidimu na Lumumba wameilalamikia halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kutaka kuwapora eneo la makazi yao kwa kupima viwanja katika mashamba yao bila kulipa fidia kama sheria kifungu namba 24 ya Katiba ya Muungano kinavyoainisha. Wakazi hao ambao tayari wamejenga nyumba za kudumu ikiwa pamoja na kukaa katika maeneo husika kwa muda mrefu ambapo kufuata na kifungu cha sheria namba 24 cha Katiba ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania ambayo lazima kuwepo na makubaliano kwa pande zote tatu zitakazoshiriki mchakato huo wa maeneo hayo kupimwa kwa maridhiano ambayo hayatakandamiza upande mwingine. Mmoja wa wakazi wa eneo hilo BW. JUMA MFUHU ameeleza kushangazwa kwake na jinsi halamshauri ya mji wa Kibaha inavyoendesha shughuli zake na hasa ukizingatia zoezi la upimaji mji sio jambo geni ikiwa halmashauri imeamua kweli kufuata sheria badala ya kutaka kutumia nguvu kuhamisha wakazi hao bila kuwalipa fidia. Na am

Imam kortini kwa uchochezi

Imam kortini kwa uchochezi