MBUNGE WA KIBAHA MJINI AJADILI MAJI NA WAPIGA KURA WAKE.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-Mar-13/09:07:37 Kero ya maji imeendelea kuwa gumzo kwa wakazi wa mji wa Kibaha kufuatia kuvurugika kwa ratiba ya awali ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali kwa kile kinachodhaniwa ni mbinu ya makusudi inayofanywa na baadhi ya watumishi wenye magari ya kuuza maji kupata faida kwa kuyauza maji hayo kwa bei ya juu. Mmoja wa wakazi wa Maili moja BW. ALLY GONZA ameyasema hayo wakati akitoa malalamiko yake juu tatizo la upatikanaji wa maji kwa mbunge wa Jimbo uchaguzi la Kibaha mjini, MHESHIMIWA SYLVESTER KOKA wakati alipokuta na wafanyabiashara ili kuweza kuongea nao kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. BW. GONZA amebainisha suala la kutopatikana maji katika muda wa ratiba kuna wasababishia usumbufu mkubwa wananchi wa mji wa Kibaha na wamelaumu hatua ya DAWASCO kuwahamisha wateja wa Kibaha kutoka bomba la kubwa na kuwaunganisha katika bomba ambalo halina uwezo wa kutoa huduma hiyo barabara kwa wakazi mji wa Kibaha. Akijibu swali hilo Mbunge wa Kibaha, Mheshimiwa SYLVESTER KOKA amesema mpaka sasa hatua mbalimbali zimeshachukuliwa ikiwa pamoja na kuanza mchakato wa Mji wa Kibaha kuwa na mamlaka yake yenyewe ya maji sawa na kuweka bomba kubwa la maji kwa ajili ya wakazi wa maeneo ya Kibaha na Kimara ambapo bomba hilo litaishia. Akijibu swali kwa nini basi mkoa wa Pwani usiuze maji hayo ili kuweza klujipatia fedha ikiwa maji ni bidhaa kama bidhaa nyingine katika kuwezesha mkoa huo kutumia maji hayo kama kitega uchumi, MH. KOKA amebainisha kuwa kwa sasa msimamo ni kukamilisha kwanza kwa bomba hili lenye inchi za kipenyo 46. END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA