MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/20-Mar-13/15:33:23 Wananchi mjini Kibaha wametakiwa kushukluru kwa yale mambo ambayo wanayaona madogo yanayofanywa na serikali katika kuimarisha miundombinu ya maji katika suala zima la kuboresha maisha ya jamii badala ya kubeza kila mafanikio yanayofanywa na serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania. Akizungumza katika maadhimisho ya ya maji Kibaha mjini, Mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI.HALIMA KIHEMBA amesema taarifa alizosomewa zinaonyesha mafanikio na unapopata kidogo inabidi kushukuru kwa hilo maana mtu asiye na shukurani hata akipewa kikubwa hawezi kushukuru. BIBI.KIHEMBA amebainisha ipo tabia ya watanzania wengi kulaumu serikali katika kila jambo, Ilihali serikali imefanya makubwa kwani kuanzia mchakato wa kutafuta mkandarasi mradi unatekelezwa lakini wanamtaa wa Visiga, Jonugha na Saeni wao hawalioni hilo na amewataka wakazi wa mitaa hiyo kuwa na shukrani na subira kwa kuona serikali inajali na inafanya kazi hailali. Naye msoma risala, BW. BEATUS LISOSO amesema maadhimisho ya wiki ya maji yanafanyika kila mwaka kuanzia ngazi ya mtaa, Kata, wilaya, Mkoa na Taifa na katika kipindi cha miaka 24 sasa nchi yetu imekuwa ikisheherekea maadhimisho ya wiki ya maji, Mwaka huu Kimkoa maadhimisho hayo yanafanyika Kibaha na kitaifa yanafanyika katika mkoa wa Lindi. BW.LISOSO maebainisha kauli mbi ya maadhimisho ya wiki ya maji mwaka huu ni MWAKA WA USHIRIKIANO WA MAJI Kitaifa, Mradi huo unaozinduliwa ni matunda ya ushirikishaji wa wananchi ambapo jamii imechangia Milioni 1 na laki 7, ambapo wakazi waliibua mradi wa maji ambao ulipewa kipaumbele na hatimaye fedha kupatikana kutoka Benki ya Duni takriban shilingi milioni 194. Baadhi ya wananchi wa mitaa hiyo waligoma kujitokeza kwa kudai kuwa wao walikuwa hawataki maji ya kisima bali ya DAWASCO kitu ambacho kilipuuzwa pamoja na kuwepo kwa fedha za kutosha kutekeleza mradi huo na kutokana na hilo wananchi wa maeneo hayo hawakujitokeza katika maadhimisho hayo. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA