WANANCHI KIDIMU WAPINGA HATUA YA MKURUGENZI WA MJI KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-Mar-13/16:18:21 Wakazi wa Kata ya Pangani Kitongoji cha Kidimu na Lumumba wameilalamikia halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kutaka kuwapora eneo la makazi yao kwa kupima viwanja katika mashamba yao bila kulipa fidia kama sheria kifungu namba 24 ya Katiba ya Muungano kinavyoainisha. Wakazi hao ambao tayari wamejenga nyumba za kudumu ikiwa pamoja na kukaa katika maeneo husika kwa muda mrefu ambapo kufuata na kifungu cha sheria namba 24 cha Katiba ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania ambayo lazima kuwepo na makubaliano kwa pande zote tatu zitakazoshiriki mchakato huo wa maeneo hayo kupimwa kwa maridhiano ambayo hayatakandamiza upande mwingine. Mmoja wa wakazi wa eneo hilo BW. JUMA MFUHU ameeleza kushangazwa kwake na jinsi halamshauri ya mji wa Kibaha inavyoendesha shughuli zake na hasa ukizingatia zoezi la upimaji mji sio jambo geni ikiwa halmashauri imeamua kweli kufuata sheria badala ya kutaka kutumia nguvu kuhamisha wakazi hao bila kuwalipa fidia. Na amesisistiza jambo ambalo ni jema ni kwa wao kukaa na kukubaliana nao kama utaratibu wa kisheria unavyohitajika na huku ikijulikana wazi halmashauri haina ardhi wala fedha za kufidia wale ambao wataathirika na sheria hiyo inahusu kama viwanja hivyo vinataka kutumika kwa ajili ya shughuli za taasisi, kampuni aua kiwanda au shughuli yoyote inayoingiza kipato kama ilivyo kwa Kidimu ambapo inasemekana Mamlaka ya kodi Tanzanaia inalitaka eneo hilo. Nilikutana na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BI. JENIFA OMOLO ambaye yeye amesema eneo hilo ambalo wao wanataka kupima viwanja lilikuwa ni eneo la halmashauri ya mji lililokabidhiwa kwao na Mitamba na wao kuamua kugawa viwanja katika suala zima la hamashauri kujiongezea kipato kutokana na upimaji huo wa viwanja ambavyo wao huviuza kwa bei ya juu na halmashauri ikiwalipa wananchi fedha kidogo. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA