ABC BANK WATOA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/14-Mar-13/19:42:09
Benki ya ABC imetoa mikopo ya pikipiki kwa kwa wajasiriamali kupitia mpango wake kuwezesha sekta isiyo rasmi kimtaji ili ziweze kujenga uchumi imara katika ngazi ya mtu mmoja mmoja katika suala zima la kupunguza pengo la watru wasi na shughuli maalum za kufanya.
Mwenyekiti wa taifa wa muungano wa sekta isiyo rasmi, BW. DAUDA SALMINI kwa kushirikiana na AFRICA BANKING CORPORATION-ABC-, ambapo amebainisha kuwa hiyo ni mwanzo tu wa kuhakikisha sekta isiyo rasmi inaangaliwa kwa jicho tofauti katika suala zima la kuhakikisha kila mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi anawezeshwa ili kuweza kubuni mbinu mwafaka za kujipatia kipato na kuweza kulipa kodi stahili za serikali.
BW. SALMIN amebainisha kuwa mkopo huo katika hatua ya mwanzo kabisa umetolewa katika halmashauri ya mji wa Kibaha katika mtaa wa Picha ya ndege ambapo wajasiriamali sita waliokidhi vigezo wameweza kukabidhiwa pikipiki ikiwa sehemu ya uwezeshaji wa sekta isiyo rasmi, ambapo waliofanikiwa iliowapasa kutanguliza shilingi laki tano kabla ya kukopeshwa.
Aidha kupitia mpango huo muungano wa sekta isiyo rasmi nchini imeandaa mipango madhubuti kwa kushirikiana mfanyabiashara mmoja wa nchini ili aweze kukopesha bidhaa zake kwa wafanyabiashara wadogo wadogo katika jitihada zake za kuwasaidia kada hiyo ya wafanyabiashara.
Akikabidhi pikipiki hizo kwa wajasiriamali waliokidhi vigezo vya kukopesheka, Mwenyekiti wa CC Kibaha mjini, BW. MAULID BUNDALA amewataka wajasiriamali kutanguliza hulka ya ubahili watakapotaka kufanikiwa katika biashara zao, kwani uwezo wa kutunza fedha ni msingi mkubwa kwa mafanikio ya kibiashara.
BW. BUNDALA amesisitiza katika kuhakikisha kuwa kila fedha inatumika kwa lengo lililokusudiwa badala ya kutumia vyombo hivyo kwa starehe ambazo mara nyingi mwisho wake hukosa tija, kwa kujikuta wanashindwa kurejesha mkopo na kuwanyima fursa wenzao wanaohitaji kama wao.
END.
Comments
Post a Comment