MKAZI AWA KERO KWA WENZAKE.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/16 March, 2013/11:18:45
Wakazi wa eneo la Kibamba Mdimua katika manispaa ya Kinondoni wameilalamikia manispaa hiyo kwa kutomshinikiza mkazi mwenzao anayemiliki eneo kubwa la heka takriban 10 bila kulifanyia usafi na kusababisha kuzaliana kwa wanyama wakali na baridi.
Mmoja wa wakazi ambao nimeongea nao, BW. ADAM SALUM amesema mmiliki wa shamba pori hilo amesema amekuwa akisababisha kero kwa wananchi kutokana kutolihudumia eneo hilo ambalo kisheria linahesabika liko mjini na mjini hakuna shamba inakuwaje manispaa ya Kinondoni haichukui hatua stahili.
BW. SALUM amesisitiza kuwa mbali ya kutolihudumia eneo hilo, mmiliki huyo amekuwa akipanda mianzi katika kubadilish mwelekeo wa mto na hivyo kuwasababishia madhara wakazi wanaokaa ng'ambo nyingine ya mto, kwa kingo za upande huo kuliwa haraka na maji yanapokuwa yamejaa mtoni.
Naye Bi mkubwa ASHA SALEH KIDEKWA amesema yeye akiwa ni watu wa mwanzo kuhamia meneo hayo mwanzoni mwa miaka ya themanini,, ameelezea kumjua kwake mmiliki wa eneo hilo, BW. OSCAR MNYALU aambaye katika eneo hilo amepanda miti ya matunda kama mipera, michungwa na miembe.
BI.KIDEKWA amesikitishwa kwake na hatua ya jirani yake huyo kutolifanyia usafi eneo lake jambo linalowafanya weaishi roho juu kutokana na uwepo wa nyoka wakubwa na ngedere ambao wamekuwa kero tosha kwa wakazi wa maeneo ya huko, hususan kwa wale ambao wameweka madirisha ya vioo.
Balozi wa eneo hilo, BW. MKUBWA MKUBWA HAMIS amethibitisha uhalali wa mmiliki wa eneo hilo linalolalasmikiwa kwa kuzalisha wanyama wakali na baridi na kwa nafasi yake amekuwa akipokea malalamiko mbalimbali kutokana kwa wakazi wa eneo hilo wakilalamikia vurugu wanazofanyiwa na wanyama wa aina ya ngedere ambao chanzo chake uwepo wa shamba pori katika eneo lake.
BW. HAMIS amebainisha hatua kadhaa ameshachukua katika kujaribu kutanzua kizungumkuti hicho ikiwa pamoja na kuwashirikisha Diwani na mwenyekiti wa serikali ya mtaa bila mafanikio.
END.
Comments
Post a Comment