BAJETI KIBAHA DC

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/03/06/19:34:02 Halmashauri ya wilaya ya Kibaha katika mpango wake wa maendeleo wa mwaka 2013/2014 imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 15,280,299,670/= ikiwa mbali na michango ya wananchi na hili ikiwa ni ongezeko la asuilimia 7.2 ukilinganisha na bajeti mwaka 2012/2013. Akisoma hotuba katika mkutano maalum wa Baraza la madiwani, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa MANSOUR KISEBENGO amesema kuhusiana na miradi ya maendeleo itatekelezwa kila sekta kwa kadiri ya mahitaji yao. MHESHIMIWA KISABENGO amebainisha miradi ya maendeleo itatekelezwa katika sekta ya elimu kwa kukarabati nyumba za walimu, ujenzi wa vyoo na ukarabati wa vyumba vya madarasa, ikiwa pamoja na kununua vifaa vya maabara za kemia na bailogia. Kwa upande wa sekta ya afya Halmashauri ya wilaya ya Kibaha katika mwaka wa fedha 2012/2013 imenuia kukamilisha ujenzi wa nyumba ya kuhifadhia maiti katika kituo cha afya Mlandizi, ujenzi wa nyumba za madaktari, upanuzi wa wa wadi ya wazazi na kuvuna maji. Naye Diwani wa Ruvu Mheshimiwa MWEKAMO yeye ameipongeza halmashauri ya wilaya ya kuleta bajeti ambayo kama ikitekelezwa ipasavyo itasaidia katika ukamilishaji wa miradi ya maendeleo. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA