Posts

Showing posts from May, 2012

HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA NA RIPOTI YA UKAGUZI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2012-05-24/17:33:26 Halmashauri ya wilaya ya Kibaha ya Kibaha kupitia kikao maalum cha Baraza la madiwani, imesoma taarifa ya ukaguzi wa mahesabu ya kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011 ambayo imebainisha maendeleo ya miradi mbalimbali yenye lengo la kusaidia jamii katika huduma muhimu kama za maji, ujenzi wa miundombinu na utawala. Akisoma taarifa hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha anayeondoka, BI. AZIMINA MBILINYI, ambaye anakwenda kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero amesema katika kipindi chake kuna kiasi cha shilingi milioni 32,890,673/=, ambapo zimenuwiwa kuelekezwa kwenye mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi Mlandizi, Na tayari maelekezo yameshatolewa kutengenezwa kwa mpango kazi ambao ambao utatoa mchanganuo wa matumizi ya fedha ambazo zinakadiriwa kufikia shilingi Milioni 30 zitatumbukizwa katika utekelezaji wa mradi huo,m ikiwa na pamoja na shilingi milkiuoni 2,890,00/= kwa ajili ya usimamizi wa mradi huo, na ma

CWT PWANI YAJIPANGA KIUCHUMI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/17-May-12/05:29:34 PM Zaidi ya shilingi milioni 455 zitatumika katika ujenzi wa jengo la chama cha walimu mkoa wa Pwani, ikiwa ni moja ya majengo yanayokusudiwa kujengwa kila mkoa katika kuhakikisha chama hicho kinajiimarisha kiuchumi kwa kujenga vitega uchumi ambavyo vitaongeza kipato na usalama wa maisha ya Mwalimu mara baada ya kustaafu utumishi. Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Pwani, MWL. NEHEMIAH JOSEPH amemweleza mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mjini Kibaha kuwa chama chao kinategemea kukamilika kwa ujenzi wa jengo lao la ghorofa mbili ambalo linajengwa na kampuni ya SUMA JKT katika mwezi Septemba, ambapo litakapokamilika jengo hilo litakuwa na ofisi za chama cha walimu mkoa na wilaya, Benki ya walimu, ukumbi wa mikutano na ofisi nyingine zitapangishwa kwa wahitaji. MWL. JOSEPH ameongeza mradi huo wa kujenga ofisi utaendelea mpaka ngazi ya wilaya ambapo mpaka sasa katika mkoa wa Pwani wilaya ambazo zina ofisi zao wenyewe ni wilaya ya R
Ben Komba/Pwani-Tanzania/05-May-12/06:53:40 PM Mtu anayesadikiwa ni moja kati ya majambazi waliovamia nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha wananchi wilayani Kibaha, BW. UWESU FADHILI amekutwa amekufa baada ya kujeruhiwa tumboni na kitu chenye ncha kali. Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia mwili huo ukiwa umeharibika kwa kiasi cha asilimia 70, huku wadudu wakiushambulia, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walimtambua marehemu kama mmoja wa vijana wanaokaa katika nyumba ya Mwenyekiti wa kitongoji cha DENGWA ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani BW. SHAABAN MISALE aka KANGEME. Na kushikiliwa kwake kunahusiana na tukio la kwanza ambapo askari waliokuwa doria walifanikiwa kukabiliana na majambazi hayo na kufanikiwa kumuuwa Jambazi SALUM HAMIS aka MAPOZI, ambaye baada ya kufuatiliwa taarifa zake ikagundulika anakaa nyumbani kwa mwenyekiti huyo anayeshikiliwa. Mwenyekiti wa kijiji cha Vikuge, BW. VITUS MCHAMI amebainisha taarifa kuhusiana na uwezeka