Posts

Showing posts from October, 2014

NG'OMBE NI SHIDA BAGAMOYO-VIDEO

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/31 octoba 2014 Tatizo la unyanyasaji unaofanywa na wafugaji dhidi ya wakulima limefikia hatua mbaya baada ya wakulima kushindwa kufanya shughuli zao ambazo zilikuwa zinawapatia kipato. RFA ikiongea na BIBI.MARIAM ALLY Mkazi wa VIGWAZA amesema kuwa anasikitishwa na hatua ya mfugaji KINDETI kufungulia ng’ombe majira ya usiku na kuanza kura mazao yao, hali ambayo inawadhoofisha kiuchumi kwani anategemea kazi hiyo kujikimu na hali ngumu ya maisha. BIBI. MARIAM ALLY ameongeza kuwa mara zote wanapoenda kutoa taarifa katika uongozi wa kijiji, kunakuwa hakuna hatua yoyote   inayochukuliwa kupambana na hali hiyo na hivyo kuwafanya wakulima kuwa na wakati mgumu kutafakari wataishi vipi baada ya mazao yao kuliwa na mifugo. Naye BI.HALIMA TILINDE amesema inapotokea kwenda kuripoti kwenye uongozi wanaambiwa kuwa wananchotakiwa kufanya ni kukamata mnyama husika na kumfikisha kituo cha Polisi, jambo ambalo limekuwa gumu kwa upande wao, kutokana na kutoku

WALIMU WATUMIA FEDHA ZAO ZA MFUKONI

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/Octoba 30 2014 Imegundulika wilayani Bagamoyo kuwa Walimu wamekuwa wanakabiliwa na mzigo mkubwa wa kuhakikisha shule inaendeshwa kama inavyostahili, kutokana na wao kulazimika kutoa fedha zao za mfukoni kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya shule. Akizungumza na RFA Mkuu wa shule ya Msingi Chalinze mzee, BW.HAMIS KIMEZA amesema wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika uendeshaji wa shule hiyo ambayo imeanzishwa mwaka 1991, na hivyo kuwalazimu walimu kujikuta wakiingia mfukoni kuchangia mambo ambayo yalitakiwa yafanywe na serikali. BW.KIMEZA ameongeza kuwa awali shule hiyo ilikuwa haipo katika hali nzuri mpaka Mkuu wa mkoa wa Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA ambaye alipendekeza ijengwe shule ya mabati kwa dharura, jambo ambalo halikufanywa na kuamua kujenga za tofali baada ya kupata msaada kutoka taasisi ya ROOM TO READ. Amefafanua kuwa ROOM TO READ wameenda mbali mpaka kufikia hatua ya kutoa madawati kwa shule ambazo imeingia nazo mk

MFUGAJI MKOROFI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/31 octoba 2014 Tatizo la unyanyasaji unaofanywa na wafugaji dhidi ya wakulima limefikia hatua mbaya baada ya wakulima kushindwa kufanya shughuli zao ambazo zilikuwa zinawapatia kipato. RFA ikiongea na BIBI.MARIAM ALLY Mkazi wa VIGWAZA amesema kuwa anasikitishwa na hatua ya mfugaji KINDETI kufungulia ng’ombe majira ya usiku na kuanza kura mazao yao, hali ambayo inawadhoofisha kiuchumi kwani anategemea kazi hiyo kujikimu na hali ngumu ya maisha. BIBI. MARIAM ALLY ameongeza kuwa mara zote wanapoenda kutoa taarifa katika uongozi wa kijiji, kunakuwa hakuna hatua yoyote   inayochukuliwa kupambana na hali hiyo na hivyo kuwafanya wakulima kuwa na wakati mgumu kutafakari wataishi vipi baada ya mazao yao kuliwa na mifugo. Naye BI.HALIMA TILINDE amesema inapotokea kwenda kuripoti kwenye uongozi wanaambiwa kuwa wananchotakiwa kufanya ni kukamata mnyama husika na kumfikisha kituo cha Polisi, jambo ambalo limekuwa gumu kwa upande wao, kutokana na kutokuwa

WALIMU WATUMIA FEDHA ZA MFUKONI, KUFANYA MAMBO YA SERIKALI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Octoba 30 2014 Imegundulika wilayani Bagamoyo kuwa Walimu wamekuwa wanakabiliwa na mzigo mkubwa wa kuhakikisha shule inaendeshwa kama inavyostahili, kutokana na wao kulazimika kutoa fedha zao za mfukoni kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya shule. Akizungumza na RFA Mkuu wa shule ya Msingi Chalinze mzee, BW.HAMIS KIMEZA amesema wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika uendeshaji wa shule hiyo ambayo imeanzishwa mwaka 1991, na hivyo kuwalazimu walimu kujikuta wakiingia mfukoni kuchangia mambo ambayo yalitakiwa yafanywe na serikali. BW.KIMEZA ameongeza kuwa awali shule hiyo ilikuwa haipo katika hali nzuri mpaka Mkuu wa mkoa wa Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA ambaye alipendekeza ijengwe shule ya mabati kwa dharura, jambo ambalo halikufanywa na kuamua kujenga za tofali baada ya kupata msaada kutoka taasisi ya ROOM TO READ. Amefafanua kuwa ROOM TO READ wameenda mbali mpaka kufikia hatua ya kutoa madawati kwa shule ambazo imeingia nazo mkat

MTANZANIA ABUNI PROGRAMU YA KOMPYUTA

Ben Komba/Pwani-Tanzania Watanzania   nao wameamua kutokaa nyuma katika suala zima la kutngeneza program mvbalimbali za kompyuta katika kuimarisha utendaji kazi katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma na kudhibiti mwanya wa uvujaji wa fedha za serikali. Kijana NOEL KAAYA mhitimu wa Chuo kikuu cha DSM amefanikiwa kutengeneza program ambayo kwa kiasi kikubwa inasaidia kuzuia kuvuja kwa fedha za umma kulikokuwa kunafanywa na baadhi watumishi wasio waaminifu. BW. KAAYA amefafanua kuwa program hiyo inayojulikana kama   FORPAY imeanza kutumika katika Hospital mbalimbali nchini ikiwa na hospital maalum ya rufaa ya Tumbi, na kufanikiwa kuongeza makusanyo kutoka laki tatu za awali mpaka milioni tatu kwa sasa. Kwa sasa anaaendelea kutoa elimu ya matumizi ya program hiyo kwa watumishi wa hospital ya Tumbi ili waweze kuitumia kwa mafanikio ambayo yatailetea tija hospital katika suala zima la kupunguza wizi wa fedha za umma. END