WAWEKEZAJI WA CHINA PWANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania
Wawekezaji kutoka
nchini China Jimbo la Jilin wamezuru Mkoa wa Pwani,wilaya ya Bagamoyo kwa ajili
ya lengo la kuwekeza katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uwekezaji
katika maeneo ya uvuvi na ujenzi na Bandari ya Kisasa eneo la Mbegani Bagamoyo.
Ujumbe huo
ulioongozwa na Naibu Gavana wa Jimbo la Jilin,BW . ZHONGCHENG SUI amesema
wamefurahishwa na kufika kwao nchini Tanzania kwani nchi mbili zimekuwa na
uhusiano wa kidiplomasia kwa muda mrefu.
BW.SUI
amebainisha kuwa Tanzania na China zimekuwa zinasaidiana katika mambo
mbalimbali ya kiuchumi,kisiasa,kijamii na kitamaduni toka miaka mingi nyuma na
kwa kuliona hilo,ujumbe huo unaendeleza yale ambayo yalianzishwa na waasisi wa
Taifa hilo la kikomunist la China.
Naibu Gavana
ZHONGCHENG SUI amewataka wawekezaji kutoka Mkoa wa Pwani,kutosita kwenda
kuwekeza katika Jimbo la Jilin ambalo lina wakazi milioni 28 na fursa ya
uwekezaji katika maeneo ya miundo mbinu ya usafirishaji na maeneo mengineyo, na
amechukua hatua kuupongeza mkoa wa Pwani kwa kudumisha utawala bora.
Mkuu wa mkoa
wa Pwani, BIBI.MWANTUMU MAHIZA aamesema
ujio wa wageni hao kunafuattiwa ziara waliyofanya viongozi wa mkoa katika Jimbo
la Jilin,nchini China ambapo walipata fursa mbalimbali za kuweza kuona jinsi
gani wenzao wanavyoweza kuendesha mambo yao kwa mafanikio.
BIBI.MAHIZA
ameongeza ni vizuri mkoa wa Pwani ukawapokea wawekezaji hao kwa lengo la kupata
uzoefu na kutambua mbinu ambazo zinaweza kuwasaidia Watanzania kukuza uchumi na
kutoa ajira katika kuharakisha maendeleo ya taifa.END
Comments
Post a Comment