CHADEMA WAENDELEZA MASHAMBULIZI PWANI
BenKomba/Pwani-Tanzania
Wananchi wametakiwa
kusimama imara kuhakikisha wanatetea haki zao zinaao-porwa na watawala, kwani
ndiyo njia pekee ya kuhimiza maendeleo ya Taifa katika Nyanja mbalimbali.
Mlezi wa
Jimbo la Pwani, Mbunge wa viti maalum kutoka Mara, BI.ESTHER MATIKO katika
mkutano wa hadhara katika Kata ya Mailimoja Ambapo amewakumbusha wana Kibaha
kuwa matatizo ya Kibaha yanajulikana vizuri na wana Kibaha wenyewe.
BI.MATIKO
amewahimiza wananchi wa Kibaha kwenda sambamba na chama cha mapinduzi katika
kuhakikisha Chaguzi zijazo wanaongeza idadi ya madiwani na wabunge watakaoweza
kuwassaidia katika kutafuta haki zinazostahili wana Kibaha,kwa kupata
uwakilishi stahili wenye kujaa uzalendo.
Naye mmoja
wa wanaotarajiwa kugombea ubunge kupitia tiketi ya CHADEMA katika uchaguzi
ujao,DKT.MICHAEL MTALI kwa upande wake amepinga mapendekezo ya rasimu ya Katiba
na kuifafanisha na kuwa ni maelekezo ya CCM kwa faida yake yenyewe.
KDT.MTALI
amesema katiba hiyo ambayo imependekezwa na CCM imeshindwa kujibu maswali mengi
ya wananchi ambayo yapo muongo hadi muongo, na ndio kichocheo kikubwa cha
maisha mabovu kutokana na uongozi mbovu wa CCM, hali inayotishia kuvurugika kwa
amani nchini.
END.
Comments
Post a Comment