WAZAZI WAHIMIZWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WALIMU
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/
Wazazi wa
wanafunzi wanaosoma shule ya msingi Mkoa Mjini Kibaha wametakiwa kushirikiana
na walimu kaatika kutengeneza mazingira bora ya upatikakanaji wa elimu kwa
watoto wao.
Akizungumkza
katika mahafali ya viajana wa darasa la saba Mbunge wa Jimbo la uchaguzi Kibaha
mjini, BW.SYLVESTER KOKA amesema kuwa ni wajibu wa wazazi kuchangia maendeleo
ya shule za watoto wao ili ziweze kutoa tija stahili.
Mbunge KOKA
ameongeza kuwa urithi wa mzazi kwa mtoto ni elimu ili kuweza kumfanya mtoto
aweze kuwa na msingi imara wa kuweza kumfanya tegemeo kwa Taifa la leo na Taifa
la kesho.
Katika
risala yao kwa mgeni rasmi wanafunzi wanaoondoka wamebainisha changamoto
mbalimbali ambazo wamekabiliana nazo katika kipindi chote walichokuwepo na hivyo
kutumia fursa hiyo kuomba changamoto hizo zipunguzwe au zimalizwe kabisa.
Changamoto
hizo ni pamoja na kukosekana kwa Walimu wa kutosha, Vitabu cvya kujifunzia
vimekuwa ni shida kwa shule yao, kukosekana kwa maji safi na salama kutokana na
kukatwa na DAWASCO.
Changamoto
nyingine ni pamoja na kukosekana kwa viwanja vya michezo hali inayowafanya
kushindwa kushiriki kikamilifu katika michezo, na kuomba serikali kusawazisha
viwanja hivyo na hasa ikizingatiwa michezo ni afya.
END.
Comments
Post a Comment