MAJAMBAZI YATIWA MBARONI BAGAMOYO
Ben Komba/Pwani-Tanzania
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamekamatwa eneo
la Chalinze wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani, kufuatia kufanya tukio la uporaji
katika mnadi wa mifugo wa Mdaula.
Mmoja wa wafanyabiashara ambaye nimeongea naye, BW.MOSES
KIMUNYU amesema kuwa siku hiyo majira ya saa 2:30 asubuhi akiwa katika shughuli
zake za biashara mnadani hapo, alivamiwa na mtu ambaye alikuwa amevaa soksi
usoni.
BW.KIMUNYU ameongeza kuwa mara baada ya kuvamiwa alijaribu
kukimbia lakini kwa bahati mbaya akaanguka, ndipo jambazi hilo ambaye
alijulikana kwa jina moja la CHARLES ambaye ni Mmang’ati alitoa bunduki ambayo
ilikuwa imefungwa na magazeti baadhi ya maeneo.
Akiwa chini Jambazi lishurutisha kupewa fedha kutoka kwa
BW.KIMUNYU na vinginevyo angemuua, ndipo BW.KIMUNYU akaona heri atoe fedha ili
aokoe uhai wake na akatoa Milioni moja na elfu sitini akamrushia Jambazi
hilo,lakini hakuridhika akashurutisha atoe zai ndipo akamalizia na shilingi
laki moja na sitini ambazo alichukua.
Kwa bahati nzuri wafanyabiashara wenzake wakastukia tukio
lile na kuanza kukabiliana na Jambazi ambalo lilijulikana wakati anakimbia
alipovua soksi usoni na wafanyabiashara hao kumtambua lakini walishindwa
kumkamata baada ya pikipiki kujitokeza nay eye kudandia.
Naye SEFU LEKAMWE ambaye alishuhudia anasema akiwa amesimama
Mnadani aliwaona MOSES KIMUNYU na mwenzie wakipita lakini mara alishangazwa
kuona mwenzie MOSES akirudi akipiga ukenje kuomba msaada na ndipo walipoamua
kuwakabili majambazi hayo.
BW.LEKAMWE ameitaka halmashauri za wilaya wanakoppita na
minadakuimarisha ulinzi kukabiliana na wimbi la ujambazi wanalokumbana nalo
wakitekeleza shughuli ya halali za kujipatia kipato.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Kamishna msaidizi mwandamizi
URLICH MATEI amethibitisha kwa tukio hilo.
END.
Comments
Post a Comment