AKEMEA WANAOTOA AHADI HEWA KTK MASUALA YA MAENDELEO-VI9DEO.
Ben Komba/Pwani
WAZAZI na walezi mtaa wa Mwambisi Kata ya Kongowe Kibaha mjini Mkoa wa
Pwani wametakiwa kutotegemea wafadhili katika kuleta maendeleo kwenye
elimu kwa watoto wao badala yake wajitoe katika hilo.
Yahya Mtonda ofisa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki
ndiye ametoa rai hiyo kwenye mahafali ya shule ya msingi ya Mwambisi
iliyoko wilayani hapa ambapo amesema umefika wakati kwa wakazi hao
kutambua umuhimu wa elimu na kujitolea kwa hali na mali katika
kufanikisha safari ya elimu kwa watoto wao.
BW.MTONDA amesema kuwa imekuwa ni deturi kwa baadhi ya watu kuahidi bila kufanya utekelezaji wa ahadi ambayo ameahaidi, hivyo sasa wakati umefika kwa wanaotoa ahadi kutekeleza ahadi zao ili kusaidia ustawi wa mazingira ya utoaji na upatikaji wa elimu kwa kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo..
akisoma risala ya shule hiyo mmoja wa walimu amebainisha uwepo wa changamoto mbalimbali, ikiwa pamoja na ukosefu wa vyoo, na hivyo kuwalazimu walimu kutembea umbali mrefu wanapotaka kujisaidia, na kuwataka wageni na wazazi wajitolee kuchangia kukamilisha ujenzi wa choo ambacho kilianza kujengwa na kanisa la TAG.
Risala hiyo imefafanua baadhi ya mafanikio ambayo yameshafikiwa mpaka sasa ni kuongezeka kwa vyumba vya madarasa kutoka vine hadi kufikia tisa, kujenga nyumba za ofisi 2 na ofisi 2 kwa ajili ya walimu sawa na kupata samani ambavyo vyote vimepatikana kutokana na fedha za ruzuku.
Katika mahafali hayo Mtonda alioongoza harambee ambayo imesaidia
kupatikana kwa fedha taslimu kiasi cha sh. Laki 412,000 ambapo
zinataraji kutumika kwa ajili ya kupunuza sehemu ya changamoto iliyopo
shuleni hapo.
Katika kiasi hicho cha fedha Mwenyekiti wa UVCCM Kibaha, mjini, Idd Kanyallu amechangia sh. Laki 3
taslimu huku akiahidi kununua ndoo za rangi zitazotumika kwa ajili ya
kupaka rangi madarasa yote shuleni hapo.
END.
Comments
Post a Comment