MHALIFU TISHIO AKAMATWA MJINI KIBAHA




Ben Komba/Pwani-Tanzania
Mmoja wa wahalifu wanaotingisha mji wa Kibaha na vitongoji vyake, BW.MICHAEL WILLIAM maarufu kama MICHAEL DADAA ametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,Mrakibu msaidizi mwandamizi, ULRICH MATEI amesema kuwa, mhalifu huyo ambaye alikuwa Habari ya mji wa Kibaha na vitongoji vyake amepatikana baada ya wizi mifugo.

Kamanda MATEI ameongeZa kuwa mhalifu huyo anajulikana sasa kwa vitendo vya ubakaji wa kina mama, ambapo kutokana na uwepo wake kuliwasababishaia hofu kubwa wakazi wa mji wa Kibaha.

Kamanda MATEI amefafanua kuwa opersheni ya kupambana na wahalifu inaendelea mjini Kibaha, katika suala zima la kudhibiti wimbi la ujambazi lililoibuka mjini hapa.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA