WALIMU WATUMIA FEDHA ZA MFUKONI, KUFANYA MAMBO YA SERIKALI




Ben Komba/Pwani-Tanzania/Octoba 30 2014
Imegundulika wilayani Bagamoyo kuwa Walimu wamekuwa wanakabiliwa na mzigo mkubwa wa kuhakikisha shule inaendeshwa kama inavyostahili, kutokana na wao kulazimika kutoa fedha zao za mfukoni kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya shule.

Akizungumza na RFA Mkuu wa shule ya Msingi Chalinze mzee, BW.HAMIS KIMEZA amesema wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika uendeshaji wa shule hiyo ambayo imeanzishwa mwaka 1991, na hivyo kuwalazimu walimu kujikuta wakiingia mfukoni kuchangia mambo ambayo yalitakiwa yafanywe na serikali.

BW.KIMEZA ameongeza kuwa awali shule hiyo ilikuwa haipo katika hali nzuri mpaka Mkuu wa mkoa wa Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA ambaye alipendekeza ijengwe shule ya mabati kwa dharura, jambo ambalo halikufanywa na kuamua kujenga za tofali baada ya kupata msaada kutoka taasisi ya ROOM TO READ.

Amefafanua kuwa ROOM TO READ wameenda mbali mpaka kufikia hatua ya kutoa madawati kwa shule ambazo imeingia nazo mkataba wa kusaidia na hivyo amewataka Watanzanaia nao kuchangia kwa njia moja au nyingine katika kuchangia elimu.

Naye Diwani wa Kata ya Bwilingu, BW.NASSER KARAMA amesema kuwa katika shule hiyo kuna tatizo la maktaba katika Shule hiyo na kwa sasa kipaumbele kikubwa cha Kata ni ujenzi wa maabara ili kuboresha utoaji wa elimu wa masomo ya sayansi ipasavyo.

BW.KARAMA ameongeza kwamba katika ujenzi wa maabara kila mwananchi anatakiwa kushiriki katika uchangiaji ili kuwezesha mpango huo kuwezesha, ambapo mahitaji halisi ni maabara ya Kemia, maabara ya Bailojia na maabara ya Fizikia.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA