MTANZANIA ABUNI9 PROGRAMU YA KOMPYUTA
Ben Komba/Pwani-Tanzania
Watanzania nao wameamua kutokaa nyuma katika suala zima
la kutngeneza program mvbalimbali za kompyuta katika kuimarisha utendaji kazi
katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma na kudhibiti mwanya wa uvujaji wa
fedha za serikali.
Kijana NOEL
KAAYA mhitimu wa Chuo kikuu cha DSM amefanikiwa kutengeneza program ambayo kwa
kiasi kikubwa inasaidia kuzuia kuvuja kwa fedha za umma kulikokuwa kunafanywa
na baadhi watumishi wasio waaminifu.
BW. KAAYA
amefafanua kuwa program hiyo inayojulikana kama
FORPAY imeanza kutumika katika Hospital mbalimbali nchini ikiwa na
hospital maalum ya rufaa ya Tumbi, na kufanikiwa kuongeza makusanyo kutoka laki
tatu za awali mpaka milioni tatu kwa sasa.
Kwa sasa
anaaendelea kutoa elimu ya matumizi ya program hiyo kwa watumishi wa hospital
ya Tumbi ili waweze kuitumia kwa mafanikio ambayo yatailetea tija hospital
katika suala zima la kupunguza wizi wa fedha za umma.
END
Comments
Post a Comment