WALIMU WATUMIA FEDHA ZAO ZA MFUKONI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/Octoba 30 2014
Imegundulika
wilayani Bagamoyo kuwa Walimu wamekuwa wanakabiliwa na mzigo mkubwa wa
kuhakikisha shule inaendeshwa kama inavyostahili, kutokana na wao kulazimika
kutoa fedha zao za mfukoni kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya shule.
Akizungumza
na RFA Mkuu wa shule ya Msingi Chalinze mzee, BW.HAMIS KIMEZA amesema wamekuwa
wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika uendeshaji wa shule hiyo ambayo
imeanzishwa mwaka 1991, na hivyo kuwalazimu walimu kujikuta wakiingia mfukoni
kuchangia mambo ambayo yalitakiwa yafanywe na serikali.
BW.KIMEZA
ameongeza kuwa awali shule hiyo ilikuwa haipo katika hali nzuri mpaka Mkuu wa
mkoa wa Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA ambaye alipendekeza ijengwe shule ya mabati
kwa dharura, jambo ambalo halikufanywa na kuamua kujenga za tofali baada ya
kupata msaada kutoka taasisi ya ROOM TO READ.
Amefafanua
kuwa ROOM TO READ wameenda mbali mpaka kufikia hatua ya kutoa madawati kwa
shule ambazo imeingia nazo mkataba wa kusaidia na hivyo amewataka Watanzanaia
nao kuchangia kwa njia moja au nyingine katika kuchangia elimu.
Naye Diwani
wa Kata ya Bwilingu, BW.NASSER KARAMA amesema kuwa katika shule hiyo kuna
tatizo la maktaba katika Shule hiyo na kwa sasa kipaumbele kikubwa cha Kata ni
ujenzi wa maabara ili kuboresha utoaji wa elimu wa masomo ya sayansi ipasavyo.
BW.KARAMA
ameongeza kwamba katika ujenzi wa maabara kila mwananchi anatakiwa kushiriki
katika uchangiaji ili kuwezesha mpango huo kuwezesha, ambapo mahitaji halisi ni
maabara ya Kemia, maabara ya Bailojia na maabara ya Fizikia.
END
Comments
Post a Comment