MTANZANIA ABUNI PROGRAMU YA KOMPYUTA



Ben Komba/Pwani-Tanzania
Watanzania  nao wameamua kutokaa nyuma katika suala zima la kutngeneza program mvbalimbali za kompyuta katika kuimarisha utendaji kazi katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma na kudhibiti mwanya wa uvujaji wa fedha za serikali.

Kijana NOEL KAAYA mhitimu wa Chuo kikuu cha DSM amefanikiwa kutengeneza program ambayo kwa kiasi kikubwa inasaidia kuzuia kuvuja kwa fedha za umma kulikokuwa kunafanywa na baadhi watumishi wasio waaminifu.

BW. KAAYA amefafanua kuwa program hiyo inayojulikana kama  FORPAY imeanza kutumika katika Hospital mbalimbali nchini ikiwa na hospital maalum ya rufaa ya Tumbi, na kufanikiwa kuongeza makusanyo kutoka laki tatu za awali mpaka milioni tatu kwa sasa.

Kwa sasa anaaendelea kutoa elimu ya matumizi ya program hiyo kwa watumishi wa hospital ya Tumbi ili waweze kuitumia kwa mafanikio ambayo yatailetea tija hospital katika suala zima la kupunguza wizi wa fedha za umma.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA