UJENZI KITUO CHA MUDA CHA MABASI MLANDIZI WAKAMILIKA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/10/3/2014 1:53:07 PM
Wakala wa
barabara mkoa wa Pwani umetumia kiasi cha shilingi 174 kutengeneza miundombinu
ya muda ya kituo cha mabasi Mlandizi, ikiwa sehemu ya kuhakikisha barabara
zinatunzwa kwa wakati wote.
Meneja wa
wakala wa barabara mkoa wa Pwani, BW.TUMAINI SARAKIKYA ameyasema hayo wakati
alipoongea na waandishi wa ofisini kwake mjini Kibaha, ambapo amesema sababu
kubwa ya kukarabati eneo hilo ni kutuwama kwa maji wakati wa mvua na hivyo maji
hayo kuharibu barabara.
BW.SARAKIKYA
ameongeza kuwa kwa kuliona hilo ofisi yake ikaanza mchakato wa kujenga mfereji
ambao hautaruhusu maji kutuwama inapofika msimu msimu wa mvua, ikiwa pamoja na
kuweka lami eneo la kituo cha muda cha mabasi Mlandizi ili kupunguza vumbi kwa
watumiaji wa kituo hicho ambacho kwa sasa kimekamilika.
Aidha meneja
huyo wa wakala wa barabara mkoa wa Pwani, BW.SARAKIKYA ameongelea kuhusiana na
mzani wa Vigwaza ambao kwa sasa unaelekea kwenye kukamilika na hatua ambayo
mpaka sasa imeshafikiwa ni kufungwa mtambo maalum wa kupima gari likiwa
linatembea, kitaalamu WEIGH IN MOTION.
Ujenzi huo
wa mizani eneo la Vigwaza unatarajia kukamilika mwisho mwa mwezi huu, na
gharama jula za ujenzi wa mzani huo ambao utakuwa wa kwanza wa kisasa na aina
yake nchi ni kiasi cha SHILINGI Bilioni 10.
END.
Comments
Post a Comment