ZA MWIZI AROBAINI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/10/6/2014 1:09:46 AM
Tabia ya
vijana kupenda mafanikio kwa njia ya mkato imemgharimu maisha kijana mmoja
ambaye jina lake halijatambulika mara moja baada alishukiwa na hasira ya
wananchi wenye hasira kali na kupoteza maisha.
Mwandishi wa
habari hizi ameshuhudia mwili wa kijana huo ukiwa umelala ndani ya eneo la
shirika la elimu Kibaha ukiwa na majeraha mbalimbali sehemu ya kichwani ikiwa
pamoja na kukatwa na kichwa.
Baadhi ya
wananchi waliokataa kutaja majina yao wamesema imekuwa kawaida kwa eneo hilo
kuibiwa pikipiki na tukio hilo ni la nne, na pikipiki nyingine walifanikiwa
kuondoka nazo lakini mara hii bahati haikuwa yao.
Mmoja wa
wananchi ambaye anaitwa BW.MURAD MOHAMED amesema mambo ya wizi wa pikipiki na
magari umekuwa unatokea maramara katika hospitali ya Tumbi na mara zote wezi
hao walifanikiwa, lakini asubuhi ya leo wananchi waling’amua janja ya wezi hao
na kuwakamata.
Mmoja wa
wezi hao aliokolewa na wasamaria mwema na kufikishwa kituo cha Polisi kwa
ajilio ya hatua zaidi.
END
Comments
Post a Comment