KIBAFA YAPATA UDHAMINI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania
Chama cha
soka wilayani Kibaha-KIBAFA- kimempata mdhamini wa kuendesha ligi ya daraja la
nne wilayani hapa.
Mwakilishi
wa vilabu wilaya ya Kibaha, MRISHO KHALFAN amebainisha kuwa wamempata mdhamini
ambaye atachukua jukumu lote la uendeshaji wa ligi ya soka daraja la nne
wilayani Kibaha.
KHALFAN
amesema kuwa Mdhamini huyo anayekwenda kwa jina la DOKTA MICHAEL MTALI ambaye
kwa upande wake amekuwa akijishughulisha bna masuala mbalimbali ya michezo ikiwa
pamoja na kumiliki timu ya soka ya wanawake.
Aidha mwakilishi
wa vilabu wilayani Kibaha, MRISHO KHALFAN ameongeza kuwa mpaka sasa timu 12
zimeshachukua fomu kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza
Oktoba 30.
END.
Comments
Post a Comment