JAMAL MALINZI APINGWA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania
Mdau maarufu
wa mchezo wa soka mjini Kibaha, MRISHO SWAGALA ameungana na vilabu kupinga hatua
ya Katibu wa TFF, JAMAL MALINZI kuamuru kwa kila klabu inayoshiriki Ligi kuu
kukatwa asilimia 5 ya wanachopata katika mapato yao.
SWAGALA
amebainisha kuwa maandalizi ya klabu ni suala zito na linalogharimu fedha
nyingi katika kuhakikisha Timu inakaa kambini na wachezaji makocha wanapata
stahili zao ipasavyo.
Hivyo yeye
kama mdau wa soka amemshauri JAMAL MALINZI kuangalia vyanzo vingine vya mapato
kama walivyofanya wenzie waliomtangulia, badala ya kung’ang’ania mapato kiduchu
ya klabu kuyapunguza.
END.
Comments
Post a Comment