Posts

Showing posts from September, 2015

MGOMBEA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI BAGAMOYO.

Image
Ben Komba,Pwani-Tanzania/9/28/2015 10:59 AM Mgombea wa udiwani katika Kata ya Vigwaza wilaya ya Bagamoyo,Jimbo la uchaguzi Chalinze amewataka wananchi wamuunge mkono katika uchaguzi mkuu ujao kwa kumpigia kura ya ndio ili aweze kuwasaidia katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili. Mgombea huyo, BW.SADALAH CHACHA amewahakikishia wapiga kura kuwa watakapomchagua hawatajutia kura yao na hivyo amewasihi wamkopeshe kura zao ili aweze kuwalipa maendeleo. BW.CHACHA amefafanua kuwa kwa muda mrefu wananchi wa Ruvu darajani wamekuwa kama yatima na kila mwenye nguvu kuonyesha uwezo wake katika kijiji hicho na kutolea mfano wa uvamizi wa ardhi unaofanywa na wageni ili hali wenyeji wakiwa hawana ardhi ya makazi na kilimo. Amepingana na dhana ambayo serikali ya CCM inatumia ya kugawa maeneo kwa watu wanaovaa joho la uwekezaji ikiwa wanajua sio wawekezaji na wanapofika vijijini wanawalaghai wananchi kwa ahadi hewa ambazo mara nyingi hazitekel;ezwi ikiwa kama nitawajengea shu

VIDEO ALALAMIKIA POLICE KIMARA KUMUACHIA MHALIFU WA KUTUMIA SILAHA YA MOTO.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/27/2015 2:28:03 PM Vitendo vya Jeshi la Polisi kukiuka maadili ya kazi zao kwa makusudi yamezidi kushika kasi na huku wananchi wakipoteza imani kabisa na Jeshi hilo jambo ambalo linachochea vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi. Hivi karibuni nimekutana na mwananchi ambaye kazi yake ni dereva wa magari ya mizigo, BW.JUMBE RASHID JUMBE ambaye amenielezea mkasa ambao umemkuta baada ya kupaki gari eneo la Kimara Korogwe. BW.JUMBE amesema siku ya tukio yeye akiwa anaelekea katika gari yake, ndipo wakatokea vijana wawili na BODA BODA na kuanza kumshambulia huku mwenzao akifungua starter ya gari lake, katika tukio hilo alifanikiwa kuwazidi nguvu majambazi yale ambayo yalikuwa na bastola na kuacha pikipiki yao. Bw.JUMBE baada ya kuona majambazi yale yamekimbia na kumwachia pikipiki ikiwa nay eye anasafiri aliamua kuipeleka kituo cha Polisi Kimara na kukikabidhi pikipiki hiyo sambamba na kuandika maelezo nay eye kuendelea na safari nj

PONGWA MUSIC VIDEO

Image
Kijana anayechipukia katika fani ya Mziki mjini Kibaha al maarufu kama Pongwa.

MUSIC VIDEO-A-MAMAZ

Image
MWIMBO:MSTAAFU WASANII:A-MAMAZ-SHAYO MICHAEL,IDENJARUMBI NA JASON Jr. MAUDHUI:Ni kuwakumbusha serikali pamoja na wastaafu kujipanga kuhakikisha serikali inamlipa mstaafu maslahi yake stahili na Mstaafua anatumia kipato chake hicho kwa manufaa fuatilia hii clips

VIDEO MGOMBEA AAHIDI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/17/2015 12:20:11 PM Mgombea wa udiwani Kata mpya ya Kawawa katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha kupitia tiketi ya UKAWA ameawaahidi wananchi kulivalia njuga suala la ukosefu wa maji katika Kata hiyo pamoja na serikali kutoa fedha za utekelezaji wa mradi huo. Mgombea huyo BW.OTTO KINYONYI amebainisha kuwa ameshawishika kuingia katika kinyang’anyiro hicho ili aweze kupambana na changamoto hiyo ambayo tayari serikali ilishatoa shilingi milioni 168 kwa ajili ya kusambaza maji katika kata hiyo Bw.KINYONYI amebainisha kuwa mradi huo wa maji umetekelezwa chini ya kiwango ilihali kwa miaka mitatu sasa toka kukamilika kwa mradi huo ni takriban miaka mitatu na tatizo la maji linaongezeka kuwa sugu kutokana na idadi ya wahamiaji kuongezeka kila siku. BW.KINYONYI amefafanua kuwa mradi huo ulikuwa unavihusu vijiji vya, Kimara, Matuga, Msongola na makazi mapya,lakini fedha hizo zilitoka lakini mkandarasi aliweka bomba dogo ambalo limeshindwa kukidhi m

MGOMBBEA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO

Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/17/2015 12:20:11 PM Mgombea wa udiwani Kata mpya ya Kawawa katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha kupitia tiketi ya UKAWA ameawaahidi wananchi kulivalia njuga suala la ukosefu wa maji katika Kata hiyo pamoja na serikali kutoa fedha za utekelezaji wa mradi huo. Mgombea huyo BW.OTTO KINYONYI amebainisha kuwa ameshawishika kuingia katika kinyang’anyiro hicho ili aweze kupambana na changamoto hiyo ambayo tayari serikali ilishatoa shilingi milioni 168 kwa ajili ya kusambaza maji katika kata hiyo Bw.KINYONYI amebainisha kuwa mradi huo wa maji umetekelezwa chini ya kiwango ilihali kwa miaka mitatu sasa toka kukamilika kwa mradi huo ni takriban miaka mitatu na tatizo la maji linaongezeka kuwa sugu kutokana na idadi ya wahamiaji kuongezeka kila siku. BW.KINYONYI amefafanua kuwa mradi huo ulikuwa unavihusu vijiji vya, Kimara, Matuga, Msongola na makazi mapya,lakini fedha hizo zilitoka lakini mkandarasi aliweka bomba dogo ambalo limeshindwa kukidhi mahit

VIDEO KANSA YAPATA TIBA.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/9/2015 2:18:57 PM Tabia Ya Watanzania Kupuuza tiba mabadala imekuwa sababu kubwa ya kushuka kwa umri wa kuishi kunakosababishwa na watu wengi kukumbatia mila na desturi za kigeni na kupuuza utamaduni wetu ikiwa pamoja na ulaji usio na mpangilio. Hayo yamebainishwa na DKT.BAHATI MAYALA ambaye ni maarufu kwa kutibi kwa kutumia tiba mbadala ambayo haiusiani na masuala ya nguvu za kiza, bali kwa kutumia mimea na miti inayotuzunguka. DKT.MAYALA ambaye kwa sasa amewahudumia wagonjwa mbalimbali ambao wanasumbuliwa na Kansa ya matiti ambao mwandishi wa Habari hizi amebahatika kuwaona na kuongea nao, na kumeleza jisi hali yao ilivyoimarika mara baada ya kukutana na DKT.MAYALA ambaye amesomea kazi hiyo. DKT.MAYALA ambaye amewahi kufanya kazi katika Hospital ya Mkoa wa Ruvuma kwa takriban miaka kumi,amesema yeye ameanza kujua miti dawa akiwa na miaka minane na kwa kupata nafasi kwenda kusomea udaktari kulimpanua akili na kuanza kufanya utafiti wa m

TIBA YA KANSA YAPATIKANA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/9/2015 2:18:57 PM Tabia Ya Watanzania Kupuuza tiba mabadala imekuwa sababu kubwa ya kushuka kwa umri wa kuishi kunakosababishwa na watu wengi kukumbatia mila na desturi za kigeni na kupuuza utamaduni wetu ikiwa pamoja na ulaji usio na mpangilio. Hayo yamebainishwa na DKT.BAHATI MAYALA ambaye ni maarufu kwa kutibi kwa kutumia tiba mbadala ambayo haiusiani na masuala ya nguvu za kiza, bali kwa kutumia mimea na miti inayotuzunguka. DKT.MAYALA ambaye kwa sasa amewahudumia wagonjwa mbalimbali ambao wanasumbuliwa na Kansa ya matiti ambao mwandishi wa Habari hizi amebahatika kuwaona na kuongea nao, na kumeleza jisi hali yao ilivyoimarika mara baada ya kukutana na DKT.MAYALA ambaye amesomea kazi hiyo. DKT.MAYALA ambaye amewahi kufanya kazi katika Hospital ya Mkoa wa Ruvuma kwa takriban miaka kumi,amesema yeye ameanza kujua miti dawa akiwa na miaka minane na kwa kupata nafasi kwenda kusomea udaktari kulimpanua akili na kuanza kufanya utafiti wa m

VIDEO-WAISLAMU WAOMBEA AMANI

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/6/2015 1:58:44 PM Waumini wa dini ya kiislam nchini  wamefanya ibada maalum ya kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani ambao unatarajiwa kufanyika  Oktoba 25   mwaka huu. Mkuu wa wilaya ya Kibaha, BIBI.HALIMA KIHEMBA kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Pwani, amesema kuwa viongozi wa dini wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na hali ya amani kabla ya uchaguzi,wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi. Mkuu huyo wa wilaya BI.KIHEMBA ameongeza kuwa serikali ina wajibu wa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu,haki na amani, ingawa serikali yenyewe haiwezi bbila kuwashirikisha wadau ambao ni pamoja na viongozi wa dini katika kuwahimiza waumini wao kufuata sheria na taratibu zilizopo.  Naye SHEIKH LIPAMBILA MUDHIHIR akielezea kuhusu uumbaji amesema kuwa Mungu akiombwa anasikiliza, ametoa mfano kuwa Mungu ameumba binadamu mwanaume na mwanamke, ameumba jua na mvua na mambo mengine chungu nzima akitaka binadam

VIDEO-CHADEMA YATISHA KIBAHA VIJIJINI.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/6/2015 2:35:57 PM Chama cha demokrasia na maendele-CHADEMA-kimezindua rasmi kampeni yake ya ubunge katika Jimbo la uchaguzi Kibaha vijijini kwa kutangaza vipaumbele vinne vilivyopo katika ilani ya uchaguzi wa chama hicho. Makamu wa mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, BW.SAID ISSA MOHAMED amesema kuwa mgawanyo wa ubunge kwa UKAWA ni kwamba katika Mkoa wa Pwani chama cha demokrasia kina nafasi ya ubunge tatu na CUF wa nafasi saba. BW.MOHAMED ameongeza hatua yoyote ya mwanacha mwingine kutoka umoja wa UKAW kugombea sehemu ambayo imetengwa kwa ajili ya chama shirika kingine ni usaliti ambao amesema utafanyiwa kazi ili kupata ufumbuzi. BW.MOHAMED amewataka wananchi wa Kibaha kutokubali kununuliwa na CCM, Katika uchaguzi mkuu ujao, ilihali hali ya mambo ikizidi kuwa mbaya kutokana na kukosekana utawala bora ambao u nathamini ustawi wa wananchi. Akimtambulisha mgombea Ubunge wa CHADEMA, BI.EDITHA BABEIYA amewataka wapiga kura kumchagua yeye ili

WAISLAMU WAOMBEA AMANI UCHAGUZI MKUU

Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/6/2015 1:58:44 PM Waumini wa dini ya kiislam nchini  wamefanya ibada maalum ya kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani ambao unatarajiwa kufanyika  Oktoba 25   mwaka huu. Mkuu wa wilaya ya Kibaha, BIBI.HALIMA KIHEMBA kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Pwani, amesema kuwa viongozi wa dini wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na hali ya amani kabla ya uchaguzi,wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi. Mkuu huyo wa wilaya BI.KIHEMBA ameongeza kuwa serikali ina wajibu wa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu,haki na amani, ingawa serikali yenyewe haiwezi bbila kuwashirikisha wadau ambao ni pamoja na viongozi wa dini katika kuwahimiza waumini wao kufuata sheria na taratibu zilizopo.  Naye SHEIKH LIPAMBILA MUDHIHIR akielezea kuhusu uumbaji amesema kuwa Mungu akiombwa anasikiliza, ametoa mfano kuwa Mungu ameumba binadamu mwanaume na mwanamke, ameumba jua na mvua na mambo mengine chungu nzima akitaka binadamu wa

CHADEMA KIBAHA VIJIJINI YAJIDHATITI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/6/2015 2:35:57 PM Chama cha demokrasia na maendele-CHADEMA-kimezindua rasmi kampeni yake ya ubunge katika Jimbo la uchaguzi Kibaha vijijini kwa kutangaza vipaumbele vinne vilivyopo katika ilani ya uchaguzi wa chama hicho. Makamu wa mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, BW.SAID ISSA MOHAMED amesema kuwa mgawanyo wa ubunge kwa UKAWA ni kwamba katika Mkoa wa Pwani chama cha demokrasia kina nafasi ya ubunge tatu na CUF wa nafasi saba. BW.MOHAMED ameongeza hatua yoyote ya mwanacha mwingine kutoka umoja wa UKAW kugombea sehemu ambayo imetengwa kwa ajili ya chama shirika kingine ni usaliti ambao amesema utafanyiwa kazi ili kupata ufumbuzi. BW.MOHAMED amewataka wananchi wa Kibaha kutokubali kununuliwa na CCM, Katika uchaguzi mkuu ujao, ilihali hali ya mambo ikizidi kuwa mbaya kutokana na kukosekana utawala bora ambao u nathamini ustawi wa wananchi. Akimtambulisha mgombea Ubunge wa CHADEMA, BI.EDITHA BABEIYA amewataka wapiga kura kumchagua yeye ili aen

VIDEO-SLAA AZONGWA KILA KONA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/3/2015 12:36:26 PM Wananchi Mkoa wa Pwani wametakiwa kutosikiliza maneno mbalimbali ambayo yanatolewa na viongozi ambao wameamua kujiweka pembeni kufuatia ujio Waziri mkuu mstaafu, BW. EDWARD LOWASSA. Katibu mwenezi wa CHADEMA wilayani Bagamoyo, BW.SADALLAH CHACHA amesema ingekuwa vyema kwa viongozi wanaoondoka CHADEMA waende kimya kimya badala ya kunyea kambi. BW.CHACHA ameongeza kuwa zoezi wa watu kujitoa kutokana na kushawishiwa na chama hicho hakijafa kwa hiyo ni sehemu ya mchakato wa kujenga demokrasia ndani ya chama na nje ya chama. Amefafanua kuwa wao kama wao walikodi gari kutoka Mlandizi kwenda Jangwani kutokana na umbali kutoka hapo mpaka Mlandizi Mtu hawezi kutembea na miguu kwa hiyo mtu kuchukulia ni kigezo cha kuweza kubadilisha maamuzi ya Watanzania hakina mantiki. Katibu Mwenezi huyo wa CHADEMA, BW.SADALLAH CHACHA amewataka wanachama na washabiki wa CHADEMA kutokubali kuyumbishwa na maneno hayo ya mtu ambaye angeweza kus

VIDEO-YANGA YAIMARISHA NGOME ZAKE

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/4/2015 1:10:38 PM Klabu bingwa ligi kuu ya Vodacom, Yanga Dar African inaendelea na mchakato wa kujenga kiwanja cha kimataifa cha michezo katika eneo la Jangwani katika suala zima la kuhakikisha wanajitosheleza kwenye miundombinu ya michezo. Mwenyekiti wa matawi ya Yanga nchini, MOHAMED MSUMI amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Tawi la Yanga Maili moja, Kibaha mjini ambapo amesema kuwa mpaka sasa hatua mbalimbali zimeshachukuliwa kuhakikisha mafanikio hayo yanafikiwa. MSUMI amebainisha kuwa mpaka sasa wameshawasiliana na mamlaka husika ili ikiwezekana waongezewe eneo la kiwanja chao ili waweze kujenga uwanja huo ambao unatarajiwa kuchukua mashabiki 40000 na kuwepo kwa vianja mbalimbali kwa ajili kuendeleza michezo. Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo mfanyabiashara na mshabiki mkubwa wa Yanga, LLYOD ATANAKA ameelezea kufurahishwa kwake na hatua hiyo ya wanachama wa Yanga kujiunga na kufungua Tawi hilo. Shabiki huyo wa Yanga,ATANAKA amewasi

VIDEO-BODABODA WAASWA WASITUMIKE VIBAYA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/4/2015 4:55:15 PM Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani limewatunuku vyeti madereva wa bodaboda ambao wamemaliza mafunzo ya usalama barabarani ambayo yametolewa na shirika lisilo la kiserikali la ANTI POVERTY AND ENVIROMENTAL CARE-APEC. Mkurugenzi wa shirika hilo, BW.RESPICIUS TIMANYWA ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha usalama wa vyombo hivyo linakuwa jambo la lazima kwa kutoa elimu ambayo ikizingatiwa itaweza kuokoa maisha ya wengi. Bw.TIMANYWA amefafanua kuwa mpaka sasa wameshafikia mikoa 15 katika kuhakikisha wanawajen gea uwezo madereva  kiuchumi na kijamii na kufanikiwa kupunguza ajali kwa asilimia 95 ya wale ambao wamepatiwa mafunzo. Mrakibu mwandamizi wa Jeshi la Polisi TABITHA MAKARANGA amewashukuru APEC kwa kutoa mafunzo hayo ambayo kwa njia moja au nyingine yataweza kupunguza ajali zinazosababishwa na bodaboda. Mrakibu mwandamizi MAKARANGA amesema kuwa takwimu mpaka sasa zinaonyesha waathirika wakubwa wa ajali za bar