VIDEO MGOMBEA AAHIDI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO


Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/17/2015 12:20:11 PM
Mgombea wa udiwani Kata mpya ya Kawawa katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha kupitia tiketi ya UKAWA ameawaahidi wananchi kulivalia njuga suala la ukosefu wa maji katika Kata hiyo pamoja na serikali kutoa fedha za utekelezaji wa mradi huo.

Mgombea huyo BW.OTTO KINYONYI amebainisha kuwa ameshawishika kuingia katika kinyang’anyiro hicho ili aweze kupambana na changamoto hiyo ambayo tayari serikali ilishatoa shilingi milioni 168 kwa ajili ya kusambaza maji katika kata hiyo

Bw.KINYONYI amebainisha kuwa mradi huo wa maji umetekelezwa chini ya kiwango ilihali kwa miaka mitatu sasa toka kukamilika kwa mradi huo ni takriban miaka mitatu na tatizo la maji linaongezeka kuwa sugu kutokana na idadi ya wahamiaji kuongezeka kila siku.

BW.KINYONYI amefafanua kuwa mradi huo ulikuwa unavihusu vijiji vya, Kimara, Matuga, Msongola na makazi mapya,lakini fedha hizo zilitoka lakini mkandarasi aliweka bomba dogo ambalo limeshindwa kukidhi mahitaji.

AIDHA mgombea huyo akizungumzia suala la afya serikali imesema fedha zimetengwa kuimarisha huduma ya afya,Lakini amesikitishwa na sheria ndogo inayomtaka mgonjwa kulipa shilingi 5000/= kabla ya kumuona Daktari, na ameitaja sheria hiyo ni kandamizi.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA