MGOMBBEA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/9/17/2015 12:20:11 PM
Mgombea wa
udiwani Kata mpya ya Kawawa katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha kupitia
tiketi ya UKAWA ameawaahidi wananchi kulivalia njuga suala la ukosefu wa maji
katika Kata hiyo pamoja na serikali kutoa fedha za utekelezaji wa mradi huo.
Mgombea huyo
BW.OTTO KINYONYI amebainisha kuwa ameshawishika kuingia katika kinyang’anyiro
hicho ili aweze kupambana na changamoto hiyo ambayo tayari serikali ilishatoa
shilingi milioni 168 kwa ajili ya kusambaza maji katika kata hiyo
Bw.KINYONYI
amebainisha kuwa mradi huo wa maji umetekelezwa chini ya kiwango ilihali kwa
miaka mitatu sasa toka kukamilika kwa mradi huo ni takriban miaka mitatu na
tatizo la maji linaongezeka kuwa sugu kutokana na idadi ya wahamiaji kuongezeka
kila siku.
BW.KINYONYI
amefafanua kuwa mradi huo ulikuwa unavihusu vijiji vya, Kimara, Matuga,
Msongola na makazi mapya,lakini fedha hizo zilitoka lakini mkandarasi aliweka
bomba dogo ambalo limeshindwa kukidhi mahitaji.
AIDHA
mgombea huyo akizungumzia suala la afya serikali imesema fedha zimetengwa
kuimarisha huduma ya afya,Lakini amesikitishwa na sheria ndogo inayomtaka
mgonjwa kulipa shilingi 5000/= kabla ya kumuona Daktari, na ameitaja sheria
hiyo ni kandamizi.
END.
Comments
Post a Comment