MGOMBEA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI BAGAMOYO.
Ben
Komba,Pwani-Tanzania/9/28/2015 10:59 AM
Mgombea wa
udiwani katika Kata ya Vigwaza wilaya ya Bagamoyo,Jimbo la uchaguzi Chalinze
amewataka wananchi wamuunge mkono katika uchaguzi mkuu ujao kwa kumpigia kura
ya ndio ili aweze kuwasaidia katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.
Mgombea
huyo, BW.SADALAH CHACHA amewahakikishia wapiga kura kuwa watakapomchagua
hawatajutia kura yao na hivyo amewasihi wamkopeshe kura zao ili aweze kuwalipa
maendeleo.
BW.CHACHA
amefafanua kuwa kwa muda mrefu wananchi wa Ruvu darajani wamekuwa kama yatima
na kila mwenye nguvu kuonyesha uwezo wake katika kijiji hicho na kutolea mfano
wa uvamizi wa ardhi unaofanywa na wageni ili hali wenyeji wakiwa hawana ardhi
ya makazi na kilimo.
Amepingana
na dhana ambayo serikali ya CCM inatumia ya kugawa maeneo kwa watu wanaovaa
joho la uwekezaji ikiwa wanajua sio wawekezaji na wanapofika vijijini
wanawalaghai wananchi kwa ahadi hewa ambazo mara nyingi hazitekel;ezwi ikiwa
kama nitawajengea shule au zahanati.
Naye mgombea
nafasi ya Ubunge kupitia tiketi ya UKAWA,BW.MATHAYO TORENGEY amesema kuwa yeye
ni mgombea anayewania kiti hicho akishindana na mtoto wa Rais ambaye biashara
anazofanya zinajulikana.
Amefafanua
kuwa anawaomba wapiga kura kufika
Chalinze na wajionee wenyewe jinsi gani familia ya mkuu wa nchi
inavyodharauliwa kutokana na wananchi kutoridhishwa na yanayofanywa na familia
hiyo.
BW,TORENGEY
amewaomba wapiga kura kumchagua yeye akawawakilishe Dodoma bungeni ili kuweza
kutatua kero zilizopo kama ujenzi wa Kituo cha afya kwa ajili ya kuwasaidia
wagonjwa na majeruhi wa ajali ambazo zinajitokeza mara kwa mara, ahadi ambayo
mbunge wa sasa ameshindwa kufanya.
END.
Comments
Post a Comment