VIDEO-BODABODA WAASWA WASITUMIKE VIBAYA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/9/4/2015 4:55:15 PM
Jeshi la Polisi
mkoa wa Pwani limewatunuku vyeti madereva wa bodaboda ambao wamemaliza mafunzo
ya usalama barabarani ambayo yametolewa na shirika lisilo la kiserikali la ANTI
POVERTY AND ENVIROMENTAL CARE-APEC.
Mkurugenzi
wa shirika hilo, BW.RESPICIUS TIMANYWA ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni
kuhakikisha usalama wa vyombo hivyo linakuwa jambo la lazima kwa kutoa elimu
ambayo ikizingatiwa itaweza kuokoa maisha ya wengi.
Bw.TIMANYWA
amefafanua kuwa mpaka sasa wameshafikia mikoa 15 katika kuhakikisha wanawajen
gea uwezo madereva kiuchumi na kijamii
na kufanikiwa kupunguza ajali kwa asilimia 95 ya wale ambao wamepatiwa mafunzo.
Mrakibu
mwandamizi wa Jeshi la Polisi TABITHA MAKARANGA amewashukuru APEC kwa kutoa
mafunzo hayo ambayo kwa njia moja au nyingine yataweza kupunguza ajali
zinazosababishwa na bodaboda.
Mrakibu
mwandamizi MAKARANGA amesema kuwa takwimu mpaka sasa zinaonyesha waathirika
wakubwa wa ajali za barabarani ni madereva wa bodaboda.
Comments
Post a Comment