VIDEO-SLAA AZONGWA KILA KONA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/9/3/2015 12:36:26 PM
Wananchi
Mkoa wa Pwani wametakiwa kutosikiliza maneno mbalimbali ambayo yanatolewa na
viongozi ambao wameamua kujiweka pembeni kufuatia ujio Waziri mkuu mstaafu, BW.
EDWARD LOWASSA.
Katibu
mwenezi wa CHADEMA wilayani Bagamoyo, BW.SADALLAH CHACHA amesema ingekuwa vyema
kwa viongozi wanaoondoka CHADEMA waende kimya kimya badala ya kunyea kambi.
BW.CHACHA
ameongeza kuwa zoezi wa watu kujitoa kutokana na kushawishiwa na chama hicho
hakijafa kwa hiyo ni sehemu ya mchakato wa kujenga demokrasia ndani ya chama na
nje ya chama.
Amefafanua
kuwa wao kama wao walikodi gari kutoka Mlandizi kwenda Jangwani kutokana na
umbali kutoka hapo mpaka Mlandizi Mtu hawezi kutembea na miguu kwa hiyo mtu
kuchukulia ni kigezo cha kuweza kubadilisha maamuzi ya Watanzania hakina
mantiki.
Katibu
Mwenezi huyo wa CHADEMA, BW.SADALLAH CHACHA amewataka wanachama na washabiki wa
CHADEMA kutokubali kuyumbishwa na maneno hayo ya mtu ambaye angeweza
kusababisha majanga makubwa kwa Taifa kutokana na usaliti ambao wameuonyesha.
END.
Comments
Post a Comment