VIDEO-CHADEMA YATISHA KIBAHA VIJIJINI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/9/6/2015 2:35:57 PM
Chama cha
demokrasia na maendele-CHADEMA-kimezindua rasmi kampeni yake ya ubunge katika
Jimbo la uchaguzi Kibaha vijijini kwa kutangaza vipaumbele vinne vilivyopo
katika ilani ya uchaguzi wa chama hicho.
Makamu wa
mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, BW.SAID ISSA MOHAMED amesema kuwa mgawanyo wa
ubunge kwa UKAWA ni kwamba katika Mkoa wa Pwani chama cha demokrasia kina
nafasi ya ubunge tatu na CUF wa nafasi saba.
BW.MOHAMED ameongeza
hatua yoyote ya mwanacha mwingine kutoka umoja wa UKAW kugombea sehemu ambayo
imetengwa kwa ajili ya chama shirika kingine ni usaliti ambao amesema
utafanyiwa kazi ili kupata ufumbuzi.
BW.MOHAMED
amewataka wananchi wa Kibaha kutokubali kununuliwa na CCM, Katika uchaguzi mkuu
ujao, ilihali hali ya mambo ikizidi kuwa mbaya kutokana na kukosekana utawala
bora ambao u nathamini ustawi wa wananchi.
Akimtambulisha
mgombea Ubunge wa CHADEMA, BI.EDITHA BABEIYA amewataka wapiga kura kumchagua
yeye ili aende kuwawakilisha bungeni na hasa ikizingatiwa yeye amekuwa mmoja wa
wanawake saba ambao wamebahatika kuteuliwa kugombea nafasi hiyo.
Mgombea
mbunge wa CHADEMA,Kibaha vijijini BI.EDITHA BABEIYA amesema kuwa anataka kwenda
bungeni kwenda kuwawakilisha wana wa Kibaha vijijini baada ya Chama kumpima kwa
kumpeleka kwa wananchi ili waweze kumpima ingawa tayari yeye ni Mbunge wa viti
maalum.
Akizungumzia
kuhusu tuhuma zinadai yeye anahusika na ufisadi alipokuwa DAWASCO, Amebainisha
kuwa yeye akiwa kama Meneja Biashara wa DAWASCO alijaribu kutoa ushauri wa
kitaalamu kwa wakubwa zake wakampuuza na matokeo yake yakawa upotevu mkubwa wa
fedha na ameahidi kushughulikia suala hilo atakapopata nafasi hiyo, kwani ana
taarifa za kutosha juu ya suala hilo.
END.
Comments
Post a Comment